Rasimu ya Katiba: WanaJF tutoe yetu

Mkodoleaji

JF-Expert Member
Apr 27, 2008
458
138
Jamani nimeona siku za karibuni kuna watu ambao wamejiunga katika mbio za kutoa maoni kuhusu umuhimu wa kuwa na Katiba Mpya. Na wengi ya viongozi hawa ni wa CCM ambao siku zilizopita hawakuona umuhimu wa Katiba mpya.

Kuhusu wao kujiunga na hizo mbio sina tatizo. Tatizo langu ni kwamba nina wasiwasi na nia zao. Inawezekana wanataka CCM iendelee kutawala na hivyo wanafanya njama ili CCM isimamie zoezi hili na kuleta katiba wanayotaka.

Wazo langu kwa sasa ni kwamba waJF tuanze mjadala na mwisho tutoe rasimu ya katiba.
Ninashauri tutoe maoni katika vipengele vifuatavyo (wengine wanaweza kuongeza vingine).
1. Aina ya serikali - Rais mwenye Mamlaka au Waziri Mkuu mwenye Mamlaka
2. Muundo wa Serikali - Mgawanyo wa Wizara, Serikali za Mitaa, Kutofautisha Wabunge na Mawaziri au Kutotofautisha
3. Mfumo wa Uteuzi wa nafasi nyeti - kwa mfano Gavana wa Benki, CAG, Mkurugenzi wa TAKUKURU nk
4. Taasisi nyeti ambazo zinatakiwa kuainishwa kikatiba
5. Mgawanyo wa rasilimali
6. Mfumo wa Uchaguzi - Suala la uundaji wa Tume ya Uchaguzi, Tarehe ya Kufanya uchaguzi na kuapishwa kwa viongozi (ikihakikisha kwamba inatoa muda wa kutosha kuthibitisha na kuhakiki matokeo)
7. Muundo wa Mahakama zetu ikiwezekana mahakama ya Katiba
8. Muundo wa Bunge - Kwa mfano kuwa na Mabunge mawili (kwa ajili ya check and balances) yaani Senate na Bunge la Kawaida au kuwa na Bunge moja (kupunguza gharama za uendeshaji)
nk

Naomba kuwakilisha
 
Wazo zuri nadahani bongo tz alisha ianza kazi hii nawashauri kufanya mawasiliano kuweza kuweka pamoja rasmu hii mpya halafu mtuleteee jamvini tutatoa mawazo then inapelekwa mwanahalisi, raia mwema, majira , the guardian on sunday na mwananchi. Tafadahali sana mtafute bongo tz alishapata point nyingi
 
Back
Top Bottom