Rasimu ya Katiba: Tuwape fursa kuwasikiliza wa Serikali mbili pia.

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,694
787
Hivi Katika Muungano tuliona nao sasa tukipunguza hayo mambo ya muungano na kuwa 7 kutoka kwenye 22+ ya sasa kama ilivyopendekezwa na tume ya Warioba na kubaki na Serikali mbili... Hii iko je?

Kwa sababu mzigo wa Serikali tatu utaiangukia Tanganyika ndio maana wenye uzoefu wanaona ita-wa-cost Tanganyika zaidi kwa kuwa practically wao ndio watakuwa wana-i-finance serikali ya muungano... alafu tena ya kwao ya Tanganganyika ambayo in reality zitakuwa zinakaribiana kwa ukubwa.

Toa Hoja, Usipige Kelele.
 
Sio suala la kuwasikiliza, miaka yote tumeishi katika serikali mbili kwa gharama yautambulisho wetu Tanganyika,
Waliunda Kamati ya Kushughulikia KERO za Muungano, sasa kwa miaka yote hii kero zimeisha? Alianzisha Katibu Mkuu Makamba, akaja Mukama, na sasa Kinana lakini hakuna lolote ni ahadi tu tuwasikilize nini tena? Tume ya Warioba imewasikiliza tena kwa kina lakini wananchi wameamua ziwe serikali tatu.

Waache wafuwazike wafu wenzao,

TAFAKARI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Ila ukumbuke hizi kamati zilitakiwa zisibadilishe katiba au sheria yoyote ya Muungano.... na sasa ni tofauti... kwamba hayo yote ambayo yalizungumziwa yana kero... Zanzibar inakuwa na mamlaka nayo!
 
hebu tutajia kwanza hizo serikali mbili, usijekuwa umetumwa na chichiemu kupima upepo, maana ndo sera yao!!
 
Ninakuliana na wewe wale wa serikali 2 watushawishi.Hata wa serikali 3 bado hawajatushawishi vya kutosha
 
hebu tutajia kwanza hizo serikali mbili, usijekuwa umetumwa na chichiemu kupima upepo, maana ndo sera yao!!

Hhahahahah "toa hoja, usipige kelele"

Let think aloud hili ni taifa letu... It is clear Waziri Mkuu wa Tanzania sio wa Muungano... hivyo kumbe already tuna serikali ya Tanganyika... kama waziri mkuu sio wa Muungano... Then already tunayo Serikali ya Tanganyika.. inaongozwa na waziri mkuu. Kwa sasa Kayanza Pinda... Mtoto wa Mkulima.
 
hivyo vya kujificha ficha ndo hatuvitaki mkuu
 
Hawa watanganyika hawafikirii na wana mawazo mgando
Tume imependekeza serikali 3 wao wanasema serikali ya tanganyika itabebe mzigo mkubwa ku ifinance serikali yao na ya shirikisho na wao wameshaona zanzibar ni mzigo lakini huo mzigo(ZENJI) Umechoka kubebwa unataka uwekwe chini na yule mbebaji (TANGANYIKA) wanaung'ang'ania hataki kuuweka chini japo kua analalamika anaumia je huu mzigo una siri gani?
 
Wandugu wa pande zote; Mnadanganyana na kuongopeana nini? Yawe yasiwe Muungano hautavunjika kwa kuwa Wabara hawatakubali kutoa TALAKA kwa sababu zao wenyewe, Na waZanzibari wanaususa muungano kwa kuamini wao hufanyiwa ya Uraia wa kambo (2nd citizens) ! Sasa danganyatoto ya nini? (hapa kila mmoja anaficha siri nzito) Nia na Ari hamnazo Mtajengaje serikali ya UMOJA ? Ifanyike referendum (kura za raia) bila kuogopana. kila la heri na Matokeo yawe TOTALY FINAL.
 
Back
Top Bottom