Mbelwa Germano
JF-Expert Member
- May 7, 2011
- 789
- 289
Wakati ninasoma rasimu ya katika mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuna neno linakera: "Serikali ya Tanzania Bara". Sura ya kwanza, ibara ya kwanza ya rasimu hii inatamka kwamba:
"Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho lenye mamlaka kamili ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla ya Hati za Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi huru."
Sura ya sita ya rasimu hii ibara ya 57 (1).- kipengele (a),(b) na (c) inatamka kwamba:
Jamhuri ya Muungano itakuwa na muundo washirikisho lenye serikali tatu ambazo ni:
(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
(b) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; na
(c) Serikali ya Tanzania Bara.
Kwa mujibu wa rasimu hii:
"Tanzania Bara" maana yake ni eneo lote la Jamhuri ya Muungano ambalo zamani lilikuwa eneo la Jamhuri ya Tanganyika;
"Zanzibar" maana yake ni eneo lote la Jamhuri ya Muungano ambalo zamani lilikuwa eneo la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar;
Tatizo lipo hapa, Serikali ya Tanzania bara. Kwa kurejea neno Tanzania inamanisha kwamba:
Tudai Tanganyika yetu.

- Watu wa Tanganyika tumepoteza utambulisho wetu. Neno Tanzania bara haliakisi historia ya Muungano wa nchi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar.
- Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetulazimisha kuingia kwenye mfumo wa serikali tatu.
- Watanganyika tuna hofu kubwa ya kuvunja Muungano kuliko ilivyo kwa Wazanzibar.
Tudai Tanganyika yetu.