Rasimu ya Katiba Mpya: Jina "Tanzania Bara" Linakera!

Mbelwa Germano

JF-Expert Member
May 7, 2011
789
289
Wakati ninasoma rasimu ya katika mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuna neno linakera: "Serikali ya Tanzania Bara". Sura ya kwanza, ibara ya kwanza ya rasimu hii inatamka kwamba:

"Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho lenye mamlaka kamili ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla ya Hati za Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi huru."


Sura ya sita ya rasimu hii ibara ya 57 (1).- kipengele (a),(b) na (c) inatamka kwamba:

Jamhuri ya Muungano itakuwa na muundo washirikisho lenye serikali tatu ambazo ni:

(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

(b) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; na
(c) Serikali ya Tanzania Bara.


Kwa mujibu wa rasimu hii:

"Tanzania Bara" maana yake ni eneo lote la Jamhuri ya Muungano ambalo zamani lilikuwa eneo la Jamhuri ya Tanganyika;

"Zanzibar" maana yake ni eneo lote la Jamhuri ya Muungano ambalo zamani lilikuwa eneo la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar;

Tatizo lipo hapa, Serikali ya Tanzania bara. Kwa kurejea neno Tanzania inamanisha kwamba:



  1. Watu wa Tanganyika tumepoteza utambulisho wetu. Neno Tanzania bara haliakisi historia ya Muungano wa nchi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar.
  2. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetulazimisha kuingia kwenye mfumo wa serikali tatu.
  3. Watanganyika tuna hofu kubwa ya kuvunja Muungano kuliko ilivyo kwa Wazanzibar.

Tudai Tanganyika yetu.
 
hata mimi nakwazika na hili jina! hivi akina warioba walipata ugumu gani kupachika jina tanganyika moja kwa moja?
 
Kama ni serikali tatu,Tanganyika itajwe badala ya Tanzania Bara.Wazanzibar walikataa kuitwa Tanzania Visiwani,nakumbuka Mh.Pinda alibanwa na wabunge wa Zanzibar kuhusiana na hilo.Sioni sababu ya kurusisha jina hilo kwa sasa baada ya muundo wa Muungano kubadilishwa.
 
nazani kila mtanganyika itakuwa inamuuma....ohh Tanzania bara.tunataka Tanganyika yetu
 
Kamanda umenena vema ujue hata wazanzibar wameanza kutucheka siku nyingi kwani tunaonekana kujipendekeza (kuutaka)zaidi muungano kuliko wao, rai yangu vijana wa Tanganyika tusikubali kuua historia yetu kwa manufa ya vizazi vya leo na kesho!
 
Ndiyo maana inaitwa rasimu,hivyo una nafasi ya kutoa mapendekezo ya rasimu hiyo na haya uliyoyaona ni miongoni mwa mapendekezo ambayo unapaswa kuyapeleka tume ya marekebisho ya katiba. Nje ya muungano hakuna Tanzania bara bali kuna Tanganyika.
 
Cjajua ni kikwazo gani kinatufanya tuung'ang'anie muungano na watu wasioutaka wasije ingia msituni waudai kwa nguvu
 
labda walihisi watakuwa wanamfagilia mtikila

hebu tushupalie hili jina libadilishwe wakuu! vinginevyo na zanzibar nayo isomeke tanzania visiwani ndo itakuwa imebalansi

Jiulize kwani nyerere imemshinda za'br kuigeuza tanzania visiwani?
 
Back
Top Bottom