Rasimu ya katiba: Kila raia wa Tanzania lazima alipe kodi. No zero rate tax

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,694
787
Huwezi kujenga uwajibikaji na uzalendo... kama wapo wanaolipa kodi na wapo wasiolipa... Nadhani it is very wrong to have zero rate kodi kwa Raia yeyote wa Tanzania. Ni bora hata iwe 1% Lakini Lazima kila mmoja achangie kidogo....
 
Si ndio maana wanapiga meza tu kupongeza chochote kinachokuja mbele yao katika bajeti, mtu anaondoa kodi ya bajaji na bodaboda alafu anapandisha bei ya mafuta jamaa wanapiga meza kupongeza. Sasa hizo bodaboda zitaendeshwa kwa maji, hao vijana wanaowalenga wengi hizo bodaboda sio zao kwani dereva ndio anaelipa kodi ya chombo au mmiliki?
Inabidi walipe kodi hawa ili wapate akili nzuri na mbinu bora za kutusaidia kupunguza makali ya kodi ambazo miaka nenda rudi wanategemea pombe sigara, mafuta na magari. Utajenga vipi viwanda
 
Huwezi kujenga uwajibikaji na uzalendo... kama wapo wanaolipa kodi na wapo wasiolipa... Nadhani it is very wrong to have zero rate kodi kwa Raia yeyote wa Tanzania. Ni bora hata iwe 1% Lakini Lazima kila mmoja achangie kidogo....

Hakika mawazo yako kama yangu. Leo tunalalamika uzalendo umeshuka, uwajibikaji umeshuka, wananchi kuto jitambua, nk. Kwa kiasi kikubwa mambo yote haya ni kutokana kuwa na kundi kubwa linaloshuhudia kuona mambo yakienda huku hawashirikia kwa namna yoyote kuchangia uendeshaji wa nchi na uchumi kwa jumla.

Najua baadhi wanaweza kuja na mawazo rahisi kuwa raia wote wanalipa kodi (VAT). Nakubaliana na watakao kuwa na fikra hizo. Hata hivyo, kodi hii haina maumivu ya moja kwa moja kiasi kwamba mtu anajisahau na kuhisi kuwa halipi kodi.
Kodi inayouma ni income tax.

Nitolee mfano, leo tulikua tunabishana na mfanyakazi mwenzangu akisifia kuondolewa kodi kwa bajaji na boda boda. Kimsingi alinikera kwani nchi hii ni yetu sote. Mzigo wa kuiendesha nchi hii ni yetu sote, badala ya kutugawa kwenye matabaka huku matunda yanayopatikana kutokana na jasho la wachache yanawanufaisha wote.

Niliwahi andika uzi kuhusu jambo hili siku za nyuma kuelekea uchaguzi wa mwaka 2010, kuwa kwa maoni yangu ni muhimu kila mtu kulipa kodi hatakama itakua 2000/= ama 5000/= kwa mwaka. Hii itasaidia kurejesha akili timamu kwa wananchi ambao wameweka rehani akili zao kwa kofia, vitenge na ubwabwa. Aidha, itawapa wananchi na serikali legitimacy ya kuwajibishana.

Kodi ya kichwa licha ya kuwa ilionekana kuwa kero kwa wananchi lakini ilisaidia ku-impose a sense of belonging to the nation. Kama mfanyakazi wa umma, nalipa 14% ya income yangu (say TGS D) ambapo take home yangu is around 420,000/= halafu mwendesha bodaboda anaye earn wastani wa 10,000/=*30=300,000/= kwa mwezi halipi hata senti moja. Kibaya zaidi, bodaboda hizi kwa sehemu kubwa ni za wenye vipato vya kati halafu unawa exempt kulipa kodi. Mimi nilifadhaishwa sana kwa uamuzi huu wa serikali.

Kufutwa kwa kodi za bodaboda, kumefanyika kisiasa kuliko kimantiki. Namalizia kwa kusema hivi, sisi sote tunawajibu wa kuendesha nchi hii na si kundi la watu wachache kubebeshwa mzigo huu. Kinachonikera ni pale ambapo hawa wasiolipa kodi za maana ndo wapigakura wengi wanaotuletea viongozi kama akina Fastjet!
 
Kila raia ni lazima alipe kodi isipokuwa makundi maalumu ambayo ni watoto walio na umri chini ya miaka 18, wazee wenye umri zaidi ya miaka 60 na ambao hawana ajira, walemavu wa viungo ambao pasipo shaka ulemavu wao hauwawezeshi kufanya kazi yeyote inayoingiza kipato. Zaidi ya hao, yeyote atakaye acha kulipa kodi ni Kupe
 
suala dogo tu hapo mkuu,
nawewe nunua bodaboda kwani huzioni?au wanaangalia wakuwauzia?
ts nonsense.....
Au acha kazi alaf uone joto lake kama hyo buku5 ya kodi utaipata,
unafikiri wasio na kazi wamependa iwe hvyo?
Brainwashed
 
Kila raia ni lazima alipe kodi isipokuwa makundi maalumu ambayo ni watoto walio na umri chini ya miaka 18, wazee wenye umri zaidi ya miaka 60 na ambao hawana ajira, walemavu wa viungo ambao pasipo shaka ulemavu wao hauwawezeshi kufanya kazi yeyote inayoingiza kipato. Zaidi ya hao, yeyote atakaye acha kulipa kodi ni Kupe

nakupa"LIKE" mkuu,safi sana
 
Watu wasiolipa kodi ndio wengi wao utawasikia wakisema "mie sipigi kura au mie sijiandikishi kupiga kura kwani wanasiasa wote sawa" Sababu halipi kodi it doesn't pain him/her .Kiukweli kodi huleta huwajibikaji.
 
Mtoa uzi atakuwa Mwualimu tu,mana kwa kulalamika hao,kama dondora mhuu mhuu mlitumwa mfeli?
 
None sense,lazima kila mtu alipe kodi misamaha ya kisiasa haifai...wamegundua boda boda wengi vijana...wamelenga mbali kwenye uchaguzi!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom