Rasimu ya katiba: Ikulu itakuwa ya Tanganyika au muungano?

Fugwe

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
1,676
656
Kufuatia kukamilika kwa Rasimu ya kwanza ya Katiba ya Muungano wa Tanzania, mambo kadhaa yanaendelea kujitokeza ambayo yanahitaji kutolewa ufafanuzi. Moja ambalo mimi naliona ni kwamba kama tutaunda Taifa la Tanganyika na hakuna ubishi lipo njiani linakuja je, IKULU yake itakuwa wapi?? Serikali ya Muungano IKULU yake itakuwa wapi?????

Historia inatuonyesha kuwa pale MAGOGONI ni IKULU ya iliyokuwa Serikali ya Tanganyika. Sasa inarejea kwa kishindo na kukuta kuna Kiongozi wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano, je, Rais wa Serikali ya muungano atampisha mwenye nyumba yaani Tanganyika?? au mwenye nyumba aende Chamwino???

Scenario nyingine, Kama EL atagombea urais na kushinda kwa upande wa Tanganyika na Samweli Sitta akagombea ule wa muungano na akashinda, je EL atamwachia Sitta IKULU ya Magogoni yeye aende Tegeta?? Tunahitaji kuelezwa IKULU itakuwa ya nani, Tanganyika au Muungano? Lakini vilevile Tanganyika iko tayari kupokwa IKULU yake ya kihistoria??? Haya wanaJF
 
Hongera kwa kuleta hoja nyeti kama hii mheshimiwa! Historia ipo wazi kabisa kwamba ile ikulu ya magogoni ni ya serikali ya Tanganyika ila ilipangishwa tu kwa serikali ya Muungano kwa sababu Tanganyika ilizimia tangu mwaka 1964! Sasa Tanganyika imezinduka hivyo si halali mpangaji kuendelea kutumia hii nyumba wakati mwenye nyumba anaihitaji kuitumia. Mi nashauri kwamba Ijengwe ikulu nyingine ya Jamhuri ya muungano ambayo gharama zake za hujenzi zitatolewa na serikali zote mbili (na huo ndio muungano hasa) yaani serikali ya tanganyika na serikali ya zanzibar. Kama wataona bado wanapenda kuitumia hiyo ikulu ya magogoni basi hiyo mpya itakayojengwa ipewe tanganyika lakini kwa mkataba maalumu wa matumzi ili tusipoteze histolia ya ikulu yetu ya magogoni!
 
IKULU-MAGOGONI ilikuwa ya Tanganyika,hakuna mjadala hapo!!!!!!!!!!!!!!

Ni kweli kabisa. Tangu enzi na enzi za kina Von Bismark, Governor Horace Byatt na watawala wengine wa kikoloni Magogoni imekuwa Ikulu ya Tanganyika. Hata wakati Price Phillip anamkabidhi Mwalimu nyaraka za Uhuru wa Tanganyika yote hayo yalifanyikia Magogoni. Hilo halina mjadala hata chembe.

Kinachoweza kufanyika ni kuchagua kakisiwa fulani katikati ya bahari kuleeee mpakani mwa nchi hizi mbili, maeneo ya Chumbe, na kujenga Ikulu ya huo Muungano. Vinginevyo, hatutaruhusu Magogoni yetu inajisiwe na wageni. Magogoni atapangishwa Kiongozi wa Jamhuri yetu tukufu ya Tanganyika na sio vinginevyo
 
Nadhani itakuwa vyema Rais wa Tanganyika moja kwa moja aanzie Chamwino, maana wakishanogewa na Dar es Salaam ule mpango wa Makao Makuu Dodoma utaendelea kuwa hadithi mpaka kiama. Rais wa Muungano apangishwe kwa muda mchache pale Magogoni karibu na eno lake la Utawala la Zanzibar, by the way sidhani ata kama Rais huyo wa Muungano ataweza kudumu ata kwa miaka 5...
 
hoja ya msingi hii,..hawa wakina baregu wanatuletea balaa na serikali zao tatu..na wanavyopenda kuweka ikulu kando mwa bahari,ya muungano lazima ijengwe ntwara kuwapoza kwa gesi watakayowaibia!!!
tuikatae rasimu hii,kwanza inaitaja nchi ambayo haipo duniani katika historia,..tanzania bara..WTF
 
magogoni ndyo kila kitu wasituzingue kabisa.
mwisho wa siku tutengane waanze kusema
hata wao ni yao.
nooooooooooooooooooooooooooooooo
lazima ibaki kuwa ya tanganyika kwa gharama yoyote.
 
Halina ubishi itakuwa ya Tanganyika kwani hata kabla ya muungano ilikuwa inatumiwa na rais wa Tanganyika. Ila napendekeza ikulu ya serikali ya muungano iwe Zanzibar kwakuwa kwa miaka 49 mambo ya muungano yamekuwa yakifanyika kwa kutumia ikulu ya Tanganyika
 
Kwani makao makuu ya Tanzania si yapo Dodoma jamani, Ikulu mpya ya nchi itajengwa katikati ya Tanzania yaani Dodoma
 
Makao makuu ya Tanganyika yawe Dodoma na serikali nzima lazima ihamie Dodoma.
 
Serikali ya jammhuri ya Muungano makao makuu Dodoma, na serikali ya Tanganyika makao makuu magogoni.
 
Ikulu ya Magogoni ilikuwa ni ya Tanganyika na ni vizuri ibaki kuwa ya Tanganyika (Tanzania Bara). Ikulu ya Muungano haiyumkiniki kuwa ni ile ya Chamwino, Dodoma.
 
Magogoni ni Ikulu ya Tanganyika. Dodoma ni Ikulu ya JMT.
 
Makao Makuu ya serikali ya JMT yawe Dodoma. Zile Wizara zinazohusika na yale mambo 7 ya Mwungano makao yake makuu yawe Dodoma.

Serikali ya Tanganyika Makao yake Makuu yatakuwa Dar es Salaam.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom