Rasimu ya katiba: Hivi akishinda mgombea binafsi akifa mrithi wake nani?

Rose Mayemba

JF-Expert Member
May 7, 2012
721
1,017
Ndugu wanajf,
kuna jambo linanitatiza na yeyote mwenye tafsiri nzuri ya hili asisite kunitafsiria
Kwenye rasimu ya katiba ya Mheshimiwa warioba kuhusu chaguzi ndogo majimboni,rasimu hii imeonekana kutokuafiki uwepo wa chaguzi ndogo na badala yake kama itatokea mfano mbunge akafariki basi chama chake kitaweka mtu mwingine badala yake.

Sasa swali langu ni kwamba je ikitokea mbunge hakutokana na chama chochote cha siasa mrithi wake atatoka wapi?.na je hilo litakuwa ndilo chaguo la wananchi?(hapa ninagusa hata wale wenye vyama).mimi nafikiri hapa kutakuwa na mgogoro mkubwa sana kati ya wananchi na yule atakayeteuliwa.

HILI NI WAZO LANGU
 
Back
Top Bottom