Rasimu ya Katiba: 39 (3), je hakuna utata?

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
5,445
3,201
Ibara ya 39 (3) 'Raia wa Jamhuri ya Muungano hatapelekwa katika nchi ya nje yoyote kujibu mashtaka au kufanya mahojiano yoyote kinyume na ridhaa yake'.
Je Ibara hii haikinzani na sheria za kimataifa za makosa ya jinai? Siamini kama kuna mtuhumiwa atakuwa tayari kupelekwa nje ya nchi kwa ridhaa yake, hususani akifahamu ya kwamba kuna mapungufu makubwa katika mfumo wa Mahakama wa Tanzania, ambao utaweza kumweka huru.
 
Mkuu nakubaliana na wewe kabisa. Kuna vitu vingi vimekuwa overlooked in our proposed constitution in relation to the international laws which will bring chaos in future.
 
Ibara ya 39 (3) 'Raia wa Jamhuri ya Muungano hatapelekwa katika nchi ya nje yoyote kujibu mashtaka au kufanya mahojiano yoyote kinyume na ridhaa yake'.
Je Ibara hii haikinzani na sheria za kimataifa za makosa ya jinai? Siamini kama kuna mtuhumiwa atakuwa tayari kupelekwa nje ya nchi kwa ridhaa yake, hususani akifahamu ya kwamba kuna mapungufu makubwa katika mfumo wa Mahakama wa Tanzania, ambao utaweza kumweka huru.

kwel kuna utata
 
Sidhan kama kuna utata, kwasababu nchi yoyote ina wajibu wa kumlinda na kumtetea raia wake.. Kwa iyo basi ni vema vyombo vya kuamua hatima ya kosa alilofanya mshitakiwa akiwa kwao.
 
Fast jet ameshahisi the hague hapamuachi,ni kinga dhidi ya wabadhilifu(mbadala ya hiyo wangesema'tume inapendekeza mtanzania yeyote anayetumia cheo chake kutesa raia hadi kuwasababishia kifo,anayefuja mali za umma,atanyongwa mpaka kufa hadhari ili iwe fundisho''
 
Wameshahisi na kuona 2015 sio pao tena,wanajitengenezea maficho humu humu kwenye katiba
 
Ibara ya 39 (3) 'Raia wa Jamhuri ya Muungano hatapelekwa katika nchi ya nje yoyote kujibu mashtaka au kufanya mahojiano yoyote kinyume na ridhaa yake'.
Je Ibara hii haikinzani na sheria za kimataifa za makosa ya jinai? Siamini kama kuna mtuhumiwa atakuwa tayari kupelekwa nje ya nchi kwa ridhaa yake, hususani akifahamu ya kwamba kuna mapungufu makubwa katika mfumo wa Mahakama wa Tanzania, ambao utaweza kumweka huru.

kwani hata mwizi wa kuku au mdokozi wa mboga jikoni huwa anaridhia kuhojiwa? these people....
 
Ibara ya 39 (3) 'Raia wa Jamhuri ya Muungano hatapelekwa katika nchi ya nje yoyote kujibu mashtaka au kufanya mahojiano yoyote kinyume na ridhaa yake'.

Je Ibara hii haikinzani na sheria za kimataifa za makosa ya jinai? Siamini kama kuna mtuhumiwa atakuwa tayari kupelekwa nje ya nchi kwa ridhaa yake, hususani akifahamu ya kwamba kuna mapungufu makubwa katika mfumo wa Mahakama wa Tanzania, ambao utaweza kumweka huru.

Bila kuathiri mashariti ya.....
 
Imekaa vizuri, ni wajibu wetu kujenga mfumo tunaotaka. Imai kwa Mahakama itatokana na ridhaa ya wananchi kama tutaacha tabia ya kualalamika na kuttenda. Hii inalinda raia wa nchi na inalinda heshima yetu nje sio mnakuwa mazuzu mnashindwa kupaamini nyumbani au kupatengeneza paaminike badala yako mnaanza kuabudu na kuamini mifumo mingine ambayo hata haiwahusu.
 
sheria za kimatifa na zina utaratibu wake; kuwa na msingi wetu wa kisheria ulio imara kupitia kwenye Katiba ni jambo la msingi sana kuliko kukaa bila kuwa na pa kusimamia(locus stand) eti kwa vile Sheria za Kimataifa zipo, ni hatari na unaweza ukakuta watu tunatawaliwa mpaka ma vyumbani mwetu..
 
kwa mtizamo wangu jibu ni ndiyo kwa kosa la jinai tu nafikiri warioba yupo sawa ila labda liwe kosa la ugaidi hapo mtuhumiwa tena bila ridhaa yake lazima apelekwe kwa wanaojua haki,

hv wanasheria kesi ya ugaidi=kesi ya jinai?
Mfano kesi ya mh.Lwakatale wa CDM.
 
Ibara ya 39 (3) 'Raia wa Jamhuri ya Muungano hatapelekwa katika nchi ya nje yoyote kujibu mashtaka au kufanya mahojiano yoyote kinyume na ridhaa yake'.
Je Ibara hii haikinzani na sheria za kimataifa za makosa ya jinai? Siamini kama kuna mtuhumiwa atakuwa tayari kupelekwa nje ya nchi kwa ridhaa yake, hususani akifahamu ya kwamba kuna mapungufu makubwa katika mfumo wa Mahakama wa Tanzania, ambao utaweza kumweka huru.
jangala kajiwekea ka-immunity kidogo hapo
 
kwa mtizamo wangu jibu ni ndiyo kwa kosa la jinai tu nafikiri warioba yupo sawa ila labda liwe kosa la ugaidi hapo mtuhumiwa tena bila ridhaa yake lazima apelekwe kwa wanaojua haki,

hv wanasheria kesi ya ugaidi=kesi ya jinai?
Mfano kesi ya mh.Lwakatale wa CDM.

Wewe mbumbumbu wa sheria unarukia train kwa mbele. Ugaidi falls under penal codes. Hii ibara inapaswa iondolewe kuzingatia sheria za kimataifa ambazo nchi imeziridhia. Tazama USA haijaridhia ICC ndio maana raia wake hawawezi kushtakiwa huko. Sisi tumeridhia ICC, ibara hii haina maana yoyote. Lakini ni muhimu ibara hii iondolewe ili viongozi wanaouwa kwa kulinda maslahi binafsi kama ilivyofanyika Mtwara, Pemba na Mwembechai wawajibike kwa matendo yao ya kihalifu
 
Plz huwezi kumwelimisha mtu mpaka utukane?
 
Back
Top Bottom