Rasimu Mpya ya Katiba: Kazi za TAKUKURU sasa kufanywa na Jeshi la Polisi?!!

Kivumah

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
2,428
1,050
Ukisoma Ibara ya 220(1) ya Rasimu ya Katiba hii iliyotolewa juzi utaona TAKUKURU haijatajwa kama ni moja ya chombo cha Ulinzi na Usalama:

Lakini Pia Ibara ya 228(d) ya Rasimu hii utaona kuwa kazi zinazofanywa na TAKUKURU ambazo ni kuzuia Rushwa na Ufisadi sasa zitafanywa na Jeshi la Polisi

Swali la kujiuliza ni Kwanini rasimu hii haiitambui/kuitaja TAKUKURU kama chombo cha Ulinzi na usalama chenye majukumu ya kuzuia Rushwa na Ufisadi??!

Rejea:

220(1) Taasisi za Ulinzi na Usalama ni:
(a) Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(b) Jeshi la Polisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
(c) Idara ya Usalama wa Taifa

228. Katika Utekelezaji wa majukumu yake, Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano litazingatia:
(a) Viwango vya juu vya kitaaluma na nidhamu miongoni mwa wafanyakazi wake
(b) Ulinzi na ukuzaji wa haki za binadamu
(c) Kanuni za uwazi na uwajibikaji
(d) Kuzuia rushwa na ufisadi, na
(e) Kukuza mahusiano na jamii
 
MKuu Kivumah, ni sahihi kwamba TAKUKURU siyo chombo ama cha ulinzi ama cha usalama, na hii inathibitishwa na uhalisia wa shughuli zake ambazo ni kuzuia na kupambana na rushwa. Ila katika hali ya kawaida, ni chombo ambacho kwa kiasi fulani kinachanganya shughuli zake kwa nyendo za kiraia na kijeshi, ama "paramilitary apparatus." Japokuwa hakijatajwa, lakini Rais ana mamlaka ya kuunda chombo kama hicho kwa shughuli yoyote itakayoonekana inahitaji chombo.
 
Hizi idara zingine bwana tabu tuu!! Kwanza ajira zake haziko clear

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Wiki hii Dr. Hosea - Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari kusikitishwa kwake kwa masuala ya rushwa kutoingizwa katika rasimu ya katiba mpya!

Kwa namna ambavyo nchi yetu inatafunwa na rushwa, mikataba mibovu, utoroshwaji wa rasilimali za nchi nk ni dhahiri kuwa tunahitaji kuwa mwongozo wa kitaifa kukabiliana nalo. Mwongozo huu unapaswa kuwa ndani ya katiba kama sheria mama ili kuonyesha seriousness tuliyonayo katika kupambana na rushwa!

Shime wanajamvi tujadili!
 
Kwa rasimu hii ya katiba, majukumu ya TAKUKURU yamepelekwa Polisi na kwenye Tume ya maadili na uwajibikaji. Kwa kuwa TAKUKURU tangu mwanzo haikuwa chombo cha Muungano ndio maana haijawekwa kwenye katiba ya Muungano. Labda kama serikali ya Tanganyika itapenda kuendelea nayo kwa upande wake lakini kama ni vinginevyo ndio imefutwa hivyo. Lakini ukweli wenyewe ni kuwa kuendelea kuwa na vyombo vingi ambavyo wakati mwingine vinakuwa kama vinaingiliana kwani unakuta majukumu ni yale yale ni kuongeza mzigo kwa Taifa. Naunga mkono Kuimarishwa kwa Tume ya maadili na uwajibikaji na kuchukua shughuli zote za TAKUKURU lakini siungi mkono shughuli hiyo kupelekwa Polisi. Sote tunajua kuwa Polisi wetu wamekithiri kwa vitendo vya rushwa. Aidha kwa kuwa jeshi la Polisi ni sehemu ya vyombo vya Baraza la Ulinzi na Usalama ambalo Mwenyekiti wake ni Rais kunaipunguzia uhuru wake ambao ni muhimu sana katika suala Zima la kupambana na Rushwa. Hongera Tume ya Warioba kwa rasimu hii nzuri ingawa bado yako maeneo yanayotakiwa kufanyiwa marekebisho lakini kwa sasa mmetoa mwelekeo mzuri wa Kupatikana katiba bora ya nchi yetu.
 
Ni kweli uliyoyaandika! Lakini kwa taratibu za polisi kiutendaji hufanya uchunguzi pale wanapopelekewa tuhuma kwa uwazi au kificho na si kwa wao wenyewe kuibua tuhuma!

Kwa muktadha huo tunahitaji chombo ambacho kitakuwa na uwezo kufanya uchunguzi wake binafsi katika suala lo lote bila kizuizi cha sheria yo yote itakayotungwa na bunge! Kwa mfano kuchunguza kwa maslahi ya Taifa mikataba yote itakayoingiwa na serikali au taasisi zake, kufuatilia utendaji wa watumishi wa umma katika kusimamia miradi, manunuzi nk.

Chombo hiki kinatakiwa kuwa ndani ya ofisi ya rais wa muungano ili kiweze kushughulikia serikali zote mbili endapo rasimu ya katiba mpya itakubaliwa na wananchi!
 
Kwani kuweko kwa hiyo TAKUKURU kumetusaidia nini? Si hao hao ndiyo waliosema Richmond hakuna kosa, Visenti hakuwa na kosa? Kazi yao imekuwa ni ya kusafisha wakubwa.

TAKUKURU inafanya kazi kama idara ya ccm.
 
​Ndiyo sababu tunataka iwe ndani ya katiba mpya ili kuepuka kuwa chombo cha kulinda chama tawala!
 
Ni kweli uliyoyaandika! Lakini kwa taratibu za polisi kiutendaji hufanya uchunguzi pale wanapopelekewa tuhuma kwa uwazi au kificho na si kwa wao wenyewe kuibua tuhuma!

Kwa muktadha huo tunahitaji chombo ambacho kitakuwa na uwezo kufanya uchunguzi wake binafsi katika suala lo lote bila kizuizi cha sheria yo yote itakayotungwa na bunge! Kwa mfano kuchunguza kwa maslahi ya Taifa mikataba yote itakayoingiwa na serikali au taasisi zake, kufuatilia utendaji wa watumishi wa umma katika kusimamia miradi, manunuzi nk.

Chombo hiki kinatakiwa kuwa ndani ya ofisi ya rais wa muungano ili kiweze kushughulikia serikali zote mbili endapo rasimu ya katiba mpya itakubaliwa na wananchi!

Soma vizuri rasimu ya Katiba iliyotolewa Sura ya kumi na tatu TAASISI ZA UWAJIBIKAJI, SEHEMU YA KWANZA, TUME YA MAADILI NA UWAJIBIKAJI Ibara ya 188 hadi 193 utaelewa kile ninachomaanisha. Tume iko huru kabisa kwa mujibu wa rasimu hii na majukumu yake ukichunguza kwa umakini utagundua kuwa yote yaliyokuwa chini ya TAKUKURU yamepelekwa kwenye Tume hii. Tume hii ni ya Muungano kama ambavyo ungependa TAKUKURU iwe. Kwamba itakuwa chini ya ofisi ya Rais au la itategemea sharia itakayotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha Bunge la JMT litatunga sheria pia itayoainisha ni makosa gani ambayo yanakiuka maadili na uwajibikaji wa viongozi na watumishi wa umma. Baadhi ya mambo uliyoyataja kama vile mikataba mibovu, rushwa katika usimamizi wa miradi, manunuzi n.k yote ni makosa yanayotokana na ukosefu wa maadili. Tume hii ndiyo itakayokuwa inafanya shughuli hizi zote ndugu ILEJE.
 
​Ndiyo sababu tunataka iwe ndani ya katiba mpya ili kuepuka kuwa chombo cha kulinda chama tawala!

Hao walioko kwenye TAKUKURU kwa sasa, hawana moral standing ya kutetea uwepo wa chombo chao kikatiba. Kwa kukubali kusafisha wapokea rushwa wakubwa serikalini, wamethibitisha hawafai. Tutawasikilizaje watu kama hao? Waache wakose kazi.
 
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Ni chombo nyeti sana ktk kusimamia haki na utawala bora licha ya kuwa na nguvu ndogo kutekeleza majukumu yake hapa nchini.Wakati tume ya mabadiliko ya KATIBA ikipita maeneo mbalimbali kwa wananchi na makundi maalumu, Tume ilipata fursa kupokea maoni toka Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ndugu Dkt. Edward Hosea ambapo kubwa Ni kutambuliwa na KATIBA mpya ikiwa Ni pamoja na kupewa mamlaka huru kuwashughulikia wale wote wabadhilifu Mali za umma na matumizi mabaya ya madaraka.Lakini katika hali isiyo ya kawaIda, maoni yake yametiwa kapuni, na bado tume hiyo haijaonyesha mbadala wa chombo hicho kama TAKUKURU haitokuwa na nafasi ya kupambana na vita hiyo
 
Mkuu hapa tunaongelea katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania!

Jiulize utawala bora ni suala la muuungano?

Uoni kwamba jambo hili litawekwa kwenye katiba za washirika wa muungano yaani katiba ya tanganyika na ile ya zanzibar?
 
Mkuu hawa hawajaiweka kwa makusudi
na wana maana yao ambayo iko wazi
maana ndiyo wanaoweka pesa Uswis kila
muda. Yaani hili haliingii akilini kwamba
wamesahau kama huu si mpango wa makusudi.
 
Maana nilisikia Dkt. Hosea akiongelea suala hili juu ya Taasisi anayoipngoza Rasimu kutozungumzia mahali popote pale
 
Kama moja kati ya maadui wakubwa wa nchi yetu Ni Ufisadi, ukiachilia mbali na Umaskin, maradhi,ujinga, KATIBA mpya ilipaswa kuonyesha japo nia au mwelekeo wa kutafutia mwarobaini adui huyu wa nne, kwa uhai wa taifa letu
 
Back
Top Bottom