Rasilimali zinazopatikana wilaya ya mbozi mkoani songwe

TULIMAJE

Member
Jun 14, 2017
92
51
Wilaya ya mbozi ni miongoni mwa wilaya zilizopo mkoa mpya wa songwe uliogawanywa kutoka mbeya.Wilaya hii inakadiliwa kuwa na wakazi wasiopungua laki 6 na asili ya wakazi wa wilaya hii wengi ni kabila la WANYIHA kwa asilimia 70% huku makabila mengine kama WANDALI,WANYAKYUSA,WANYAMWANGA na makabila mengine madogodogo wakikadiliwa kuwa asilimia 30% tu.


Upande wa mashariki imepakana na mkoa wa mbeya,kaskazinii imepakana na wilaya ya songwe,magharibi imepakana na wilaya ya momba na kusini imepakana na wilaya ya ileje.

Wilaya ya mbozi ina majimbo mawili yaliyogawanywa kwenye uchaguzi mkuu 2015,jimbo la vwawa lenye kata 18 na jimbo mama la mbozi lenye kata 11..jumla ni kata 29 nazo ni KATA YA nambinzo,itaka,bara,igamba,magamba,halungu,isansa,itumbi,shiwinga,mlowo,mlyovizi,iyula,idiwili,hezya,nyimbili,mlangali,nanyala,ruanda,isandula,kilimampimbi,ihanda,ipunga,wasa,msia,hasanga,hasamba,vwawa,ichenjezya na ilolo.
wilaya ya mbozi ina vijiji 127.Wakazi wengi wa mbozi ni wakulima na mazao wanayolima ni kahawa na mahindi zaidi kwa kuwa hayo ni mazao ya biashara na mazao mengine kama maharagwe,ndizi,karanga n.k.

Bofya linki kusoma zaidi
Ijue Wilaya ya Mbozi, Rasilimali zinazopatikana huko na asili ya jina 'MBOZI' | MWANANCHI24
 
Back
Top Bottom