Rasilimali zetu,wanyamapori wetu,umasikini wetu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rasilimali zetu,wanyamapori wetu,umasikini wetu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mchambakwao, Oct 7, 2012.

 1. m

  mchambakwao Member

  #1
  Oct 7, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wadau Habari zenu!
  Open Areas ambazo ziko chini ya Halmashauri zetu hutumika kama njia ya utorosheaji wa wanyamapori,kuua pasipo taratibu za uwindaji kufuatwa rejea Wilaya za Monduli na Simanjiro.Vile vile kumekuwapo na watendaji wabovu na wapenda rushwa wanaodili (kufanya dili) na waarabu katika vitalu vya uwindaji.

  Kwa mfano lile sakata la utoroshaji wanyamapori hakuna hata mmoja alitoka katika Mapori ya akiba,bali wanyamapori wale wametoka katika Open Areas zilizoko katika Halmashauri za Wilaya zetu.Swali ni je,District Game Officers wamefanya na wanafanya nini katika kudhibiti uvunjaji wa taratibu,sheria na kanuni za uwindaji wa kitalii kama si wao ndio wahusika wakuu katika mambo haya?

  Mfano mwingine Hifadhi za Tarangire na Ziwa Manyara wamekuwa wakililalamikia uwindaji usiofaa na kufuata taratibu katika wilaya zinazopakana nazo hifadhi hizi,hakuna hata mkuu wa wilaya,mkurugenzi wa halmashuri anayediriki kuchukua hatua,ama hawajui au wako mbali na watendaji hawa?.

  Mwisho,suala la kupambana na ujangili katika hifadhi zetu na mapori ya akiba itakuwa kazi bure kama hawa watu wanao simamia rasilimali hizi walioko Halmashauri kama wataachwa waendelee kujisimamia kama wafanyavyo sasa,kwani Wilaya zingine hata doria hazifanyiki na hata projects za kuendeleza rasilimali hasa wanyamapori hazipo ikiwemo faida kwa wananchi,hususani 25% itokanayo na uwindaji wa kitalii wananchi hawafaidiki nazo.

  Nawasilisha!
   
Loading...