Rashid Othman ndiye Boss wa Usalama

Status
Not open for further replies.

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Wakuu,

Naona kuna Rashid hapa TISS ndiye mkuu sasa. Naamini huyu alikuwa ni naibu wa mzee aliyeondoka. Mimi sina CV yake hebu ES na wakuu wengine naomba tupe data hapa tujue huyu ni mtu wa aina gani.
 
Huyu jamaa alikuwa London, afisa ubalozi yaani agent wa kawaida wa usalama pale, sasa nilishawahi kumuongelea kule BCS, kwani kazi yake kubwa ilikuwa kumfixia mzee JK, vimwana pale,

recently list ilikwenda down to kati yake na mzee mmoja yuko Zaire, ambaye ni kabila la mzee, kwa hiyo tulitegemea kuwa ndiye angeingia, kwa kweli baada ya uchaguzi huu, nimenyoosha mikono na mzee wangu JK!

Huyu ndiye jaamaa aliyekuwa akifanya kazi ya ziada na mzee Salva Rweyemamu kumuondoa Kibello, pale London. Zile kelele zote za magazeti juu ya Kibello na habari za mfanyakazi wake wa ndani zilikuwa zinakuwa engeneeered na huyu jamaa, akishirikiana na mama mmoja pale ubalozini London anayeitwa Amina(mdogo wa mama Migiro), jamani!

Mungu aibariki Bongo, kama kweli huyu kijana Othmani anaweza kuchukua nafasi ya Apson! Sina nguvu tena!
 
I have no comments on him. I don't know this guy. Ila nadhani tumefika wakati nafasi nyeti kama hizi ziwe zinapitishwa na wawakilishi wa wananchi.
 
Mzee Sam,

Kama unakumbuka huyu jamaa, mara ya mwisho Mkapa alipofanyia mkutano na wabongo kule NY nyumbani kwa balozi, kulikuwa na jamaa mmoja mrefu amevaa miwani meusi sana kutoka London aliyekuwa akijisheua sheua pale na suti nyeusi, by the time mkutano umeisha at least kila mtu pale alijua kuwa jamaa mwenye miwani meusi amtoka London!,

yaani all his childish acts ilikuwa tu kujionyesha kuwa yeye ni secret services au angalau ukimuna tu unapata feeling kuwa huyu jamaa sio wakawaida!,
anyway JK ni rais wa nchi aliechaguliwa kisheria, kwa hiyo ni uamuzi wake kuvhagua yoyote anayetaka,

tatizo langu na uchaguzi huu ni kwamba huyu jamaa ni very junior kwa wazee wengi huko kwenye hiyo department, je ataweza kupata heshima? Unajua katika dakika za mwisho Kombe alikuwa amekosa heshima kabisaaa na wazee wa huko kabla hayajamkuta, na wewe Sam unajua jinsi hesima ilivyo muhimu huko kwenye usalama!
 
kama wana-forum mnakubuka Mama Mongela alishawahi kugusia issue hii bungeni wakati fulani, kipindi cha Mkapa. Kama sikosei alishauri kuwa uteuzi wa viongizi wa nafasi ungekuwa unafanyiwa scrutiny bungeni(Rais angependekeza). Umuhimu wa mawazo ya huyu mama yetu sasa nafikiri kila mtu anauona. By then wengi walim-ignore.

Taarifa binafsi (CV) ya mtu kama huyu- Bosi wa usalama wa Taifa ni muhimu kufahamika kwa wananchi. Kama yaliyoongelewa na Mzee ES hapo juu ni ya kweli, basi, tungojee madudu mengi katika serikali hii. Naamini wa-TZ wengi wako macho na mwelelekeo wa uongozi wa JK. Katika nchi nyingi, taarifa za mtu kama huyu huwa zinzwekwa wazi, ili kuwapa imani wananchi.

OOh, Mungu ibariki TZ.
 
Mzee ES
Yule dada wa London anaitwa Radhia. Sijui kama Amina ni jina lake la pili
 
Wazee Jasusi na Mafuchila,

Huyo mwanamama alipokuwa Mlimani alikuwa akijiita Amina Mtengeti, sasa hivi hujiita Radhia Msuya, pia naye hujimwaga na mzee!, maana safari kibao za London mzee akiwa waziri, alikuwa akipotea airport na kutoonekana hata kwa siku mbili na kuwaacha mafisa wa ubalozi na wajumbe aliofuatana nao wakiwa wanahaha!, waziri yuko wapi! waziri yukowapi!

Lakini wote mko sawa, pia ana mdogo wake anayeitwa Amina na Fatuma, tena huyo wa mwisho fununu zinasema ana ngoma, kwa hiyo mzee Jasusi angalia vizuri anga zako kwani yuko huko kwako!

Ni kweli kabisa wakati umefika kuwa na kamati maalumu ya taifa, yenye wajumbe independent ianzishwe kuangalia majina ya viongozi wa kuteuliwa na rais, mbona tunafanya hivyo kwa Waziri Mkuu, kwa nini hiyo system isishuke mpaka chini?
 
Bwana Mzawa,

Hakuna ubishi kabisaa na point zako, Mama mongella hakusikilizwa kwa sababu alikuwa amewaudhi wazee wa CCM, pale alipotoka kuwa katibu wa wanawake kule Beijing, alirudi bongo na kusema anataka kugombea urais,

kama utakumbuka, ilibidi Mzee Mang'ula amjie juu publicly na kusema Tanzania haiko tayari kuongozwa na mwanamke, can you imagine angeyasema hayo huko majuu, si angeliwa mzima mzima kisiasa?

Na ndio maana CCM ikafanya jitihada za hali ya juu, ikiwa ni pamoja na kumuomba rasmi Mzee Madiba, amuondoe spika wa bunge la huko bondeni ambaye alikuwa akigombea urais wa bunge la Afrika na alikuwa na nafasi zaidi, na kumpa huyu Mama ili aondoke kwenye uchaguzi wa rais uliopita, kwa sababu kumbuka kuwa huyo mama sio mchezo ni moto mkali huo tena wakuotea mbali!
 
1.Ni wakati muafaka kabisa, kuwa nafasi nyeti nyingi serikalini inabidi zipitishwe na wawakilishi wetu. isipokuwa najiuliza, hawa wawakilishi ni wale wale wabunge wetu au????????. katika hili tutahitaji timu HURU, MAKINI na ya UWAZI.......if at all its going to happen!!!! i don't know, huenda ndio ikawa mwisho wa dunia.

2.Huyu RO niliyemuona mimi, ni mtu very social(Mwinyi type) na alikuwa mkurugenzi wa utawala kabla hajapewa huo u-DG, hapo jana. atakuwa kwenye early/mid 50s hivi.

Im just asking myself is it a "coincidence trend" au ni ule ubashiri wa mwanabodi mmoja aliyewahi kusema nafasi nyeti zote zitaenda kwa akina..............., sijui ndio unabii huo unatimia??
 
Mzee Es,

Taratibuuuuu-:) unajua unamuongelea mmoja wa wanachama wa Bcs times (huyo Fatma)....... sijui kama sio member humu... Ofcourse ukweli unabakia ukweli!

Jasusi, Nadhani unamjua huyo mtu sina haja ya kukutajia ni mwanachama pia kule kwa akina mafuchila,Sir na DG. Ila siku hizi amepotea, alikuja juu kidogo kwenye uteuzi wa mawaziri kisha akapotea.

Siku njema

FD
 
Nimepitia kwenye forum nyingine watu wanazungumza vitu ambavyo sisi tulishaongelea udini na upendeleo, kuna watu wamekimbia humu kwa kushindwa ku-support point zao na kudai wametukanwa.

Nadhani serikali ya awamu ya nne inachukulia haya mambo kimzaha sana. Nadhani wanafikiria kuwa hawa watu watachonga mwishowe watanyamaza kitu ambacho kinawezekana kuwa siyo kweli. Hii nadhani ni challenge kubwa kwa viongozi wetu. Lazima wafikirie jinsi ya kufanya. Wasije wakafanya maamuzi kwa kuangalia Nyerere alifanya nini.

For God's sake, kuna wanabodi wengine humu walikuwa hawajazaliwa Nyerere alipokuwa rais. Wasije wakaja na sera ya 50/50 kwani hiyo italeta matatizo makubwa kama Mkwawa alivyoelezea 50/50 kwa wanaume na wanawake.

Tunaishi kwenye generation nyingine kabisa, nadhani hii ni mara ya kwanza kwa watanzania kujadili uteuzi wa mkuu wa usalama, huko nyuma sidhani hata kama kuna mtu alikuwa ana care nani ni mkuu wa usalama. Kuna mambo mengi ya kufanya, idea ya kutumia chombo maalumu kupitia uteuzi wa nafasi muhimu kwenye jamii ninauunga mkono. Hata tukianza na bunge ingawa tunajua uwezekano wa kumpinga rais kwa sasa ni mdogo lakini we have somewhere to start with na kuondoa mawazo ya uteuzi wa udini au ukabila.

Kama mawazo ya udini yakiamia bungeni basi hapo itakuwa wazi viongozi wetu wameshindwa kazi itabidi waachie madaraka na sisi tuanze kupigana bunduki wenyewekwa wenyewe tufe nchi itawaliwe na nyani na ngedere. Lazima tubadilike jamani, kama tunaanza kuongelea matatizo ya kisiasa, uchumi tutaongelea lini? Tumeshuhudia jinsi vyombo vya habari vinavyokufa kwa sababu ya wana habari kungojea kuteuliwa kuwa wakuu wa wilaya. Do we real need wakuu wa wilaya kuteuliwa na rais kwenye karne hii, do we need them? Kwa nini tusiziimarishe halmashauri za miji na kuamisha madaraka ya wakuu wa wilaya huko?

Jamani tusiendeshe nchi kama Nyerere alivyokuwa anaindesha, that was ok on his time. Wakati ule ukinunua redio bendi mbili ni hasara kubwa kwani stesheni ilikuwa moja tu na tulikuwa tunalazimika kusikiliza idea ya mtu mmoja at a time.
 
Mzee FD,

Huyo mwanamama alikuwa NY wakati mmoja,na tayari amemletea madhara mshikaji wangu mmoja kule kwa wewe ndiye ufanye taratibu, uanachama wa mtu hapa haubadili kitu au una maana rais Kikwete akiwa mwanachama hapa basi tuache kumuongelea? Na unajuaje kuwa sio mwanachama hapa? Mzee mbona huelewi tunapokwambia ufikiri kabla ya kuandika humu?

Mzee Ogah,

Ndio nilisema huko nyuma kuwa baada ya Mtandao kupewa vyeo, kinachofuatia ni vyeo nyeti na watakaopewa ni kina Mapuri's type, yaani Said Mwema ( Shemeji wa Rais wetu), Najeer (Kimwana), Makamba, na sasa Othman, sasa subiri Mkuu wa majeshi!

Mzee Sam,

Ninaziona emmotions kwenye posting yako, mzee yanayoendelea sasa hivi ni ukweli sio ndoto, au hadithi, ni lazima tukubali ukweli kwamba tumechagua a popular rais, with no record. Lakini at the same token ni lazima tukubali kwamba JK alishinda urais kutokana na kuziweza mbinu za wakati huu, yaani everything he did ni what was neeeded kwa wakati huu, yaani our time, kule US wanaita time ya Baby boomers! Ninakumbuka the shock ya baadhi ya wananchi na viongozi pale JK alipopitishwa kule Dodoma, unafikiri ni kwa nini walipata shock?

Ni kwa sababu walikuwa wanajua what was coming!, We have another 10 years of this, so fasten your belt!
 
Mzee,

Usiwe na shaka, ndio maana nimeweka ka smiley mbele ya sentesi, yaani sikuwa serious!!

Sam, Ukiwa rais lazima uteuwe watu wenye uwezo wa kazi na at the same time watasema ndiyo mzee!!, sidhani hata wewe kama utamteuwa mtu huku ukijua wazi hakupendi!

Tukirudi kwa JK, tumpe benefit of doubt, tunyamaze na kuona utendaji wa hawa watu kwanza!, tukubali (kwa sasa) kuwa jamaa ameteuliwa kwa uwazi na sio udini. Kama ulivyosema udini na ukabila ukituingia saaana kichwani tutaanza kuuwana wenyewe kwa wenyewe!!! No body wants to go that far!

Kwanini hamuhoji uwezo wa mkuu wa PCB ambaye Mahalu karudi humu nchini na hamna lolote lilofanyika?, wala hamna updates?

Tujaribu kulalamikia hawa waliopo lakini hawana wanachofanya, hawa wapya tuwapeni MUDA.

Asanteni

FD
 
Mzee ES na FD

Mimi sina matatizo na uteuzi anaoufanya. He got to do what he got to to kulingana na sheria na taratibu zilizopo. Tatizo langu nimepita kwenye forum nyingine nimesoma mawazo ya watu na kujiuliza where are we going? Are we ready for these ideas from hell? Kwa mfano hao watu wa usalama wakisoma comments watu wanazotoa kuhusu bosi wao ni heshima gani watajenga kwa bosi wao kitu ambacho ni muhimu kuliko kitu kingine chochote.

Mzee ES, hebu tuambie ni viongozi wangapi wanamheshimu JK, na viongozi wangapi aliowateua wanaheshimika. JKN alikuwa na uwezo wa kuongea na kujenga heshima na utii kwenye jamii. Je, kwenye jamii ya leo unaweza kuongea tu na watu wakakusikiliza? Nilimuonea huruma sana JK kwenye issue ya "mapanki" watanzania walikuwa wala hawaijui hata hao wabunge walikuwa hata hawajaiona ameenda kuiongelea na kushindwa kujieleza lawama zote zikamgeukia yeye mpaka ikafika kiwango ambacho yeye ameonekana kama mhusika mkuu na wakulaumiwa. Mimi namshauri hii issue ya watu kuwa na mawazo ya udini wala asiiongelee ila anatakiwa aifanyie kazi.

Kwa kweli napenda kumpongeza EL kwa kukubali kuwa rais wa nchi, JK alitumia akili sana kumteua yeye sidhani kama kuna mtu mwingine angekubali kufanya kazi ya u-PM na urais at the same time. Baada ya kipindi chake cha urais kwisha EL sidhani kama atakuwa ana haja tena ya kugombea urais.
 
Sijui kama mmeiona ile kideo ya JK akizungumza na VOA??? na kama kuna kitu kinachonishangaza, anazungumzia legacy yake. Kwa Rais ambaye hajamaliza hata mwaka kuanza kuzungumzia legacy yake sasa ni kujipa mzigo usio wa la zima na kujaribu kuandika legacy yake. Yeye kama Rais ajitahidi kutimiza majukumu yake kwa uadilifu na nguvu zote na aache legacy ijichonge yenyewe kwenye historia (let his legacy curve itself from history) siyo aanza kuchonga legacy yake ili atakapoondoka watu wamsifie!! Kwa Rais wa muhula wa kwanza legacy is the last thing he has to worry about!! Hayo ni ya Kina Bush, Blair, Mugabe, Castro, Putin n.k... yeye ndo kaanza tu....!
 
Kuna mtu mmoja alisema kwamba kila kundi lina viongozi wake hata wezi wana viongozi kwamba wakisema basi wanajua mkuu kasema .Mimi kuteuliwa kwa JK nilijua kwa tabia ya CCM basi lazima awe Rais leo kesha ukwaa ufalme ambao yeye alitumia nguvu nyingi na maandalizi mengi kuufikia .Naamini JK kuna wakati alisema kwamba anakwenda Dodoma kwenye vita .Aliyasema haya alipo ulizwa swali maeneo ya Chuo Kikuu kabla ya kuteuliwa kuwa mgombea.He was desparate na hakuwa na raha maana anajua yangalitokea yale BM na yeye lakini kwa maneno yake yale alionyesha kuwa alikuwya tayari kuua hata mtu ili aukwae ukuu ule .

Sasa leo kesha kalia kiti cha Enzi kama kawaida kila kundi na watu wake anaweka wenzake . Kuna mtu kasema jamaa wa Usalama ni mzinzi maana huwezi ku fix watoto kwa mkuu wako kama wewe si mwizi . Wezi wakiwa wakiwa kwenye kundi la watu 100 hawajuani baada ya muda utawaona wameanza maongezi . JK anawalipa fadhila watu wake wa kila mchezo alio shiriki na anao shiriki yeye .

Leo nimemsikia Betty MKswa anasema chini yake mambo yataenda nikacheka sana . JK kampa huyu jamaa Unusaji mkuu.Huyu jamaa hakuna mtu anayetoa CV yake hata magazeti. Na yeye kaanza na kuimba na Majambazo lakini kero kwenye Nchi ile ni nyingi. Ikiwemo Usalama kushiriki kuiba kura , kubadil habari ziende kwa mtindo wao nk , haki za watu yeye kaona Ujambazi tu . Nasema jamaa tunataka CV yake kwanza .

Juu ya Chombo maalumu kupitia majina ya watu na hata teuzi zao iwe Bunge ama Chombo binafsi ni nyimbo tu hizi. CCM hawako tayari kwa mabadiliko ya kweli na wataumbaumba kila kitu waonekane wamefanya . CCM wanawaogopa wasomi wacheche nikiwemo mimi maana unafiki sitaki na nitasema kweli popote .Wanatumia kila aina ya unyama kupitia Usalama nk kuwaziba midomo wasomi ambao leo hii wanafumbia macho mambo mengi sana .

Nahitimisha kwa kusema si Bunge wala independent body ama zaidi inaweza kuja na habari za ukweli juu ya teuzi za Urais .kwanza hiyo tume ama kamayi itaundwa na nani kwa powers zipi ? Lazima wa submit kwa mkuu wao maana vinginevyo hawatakuwepo kwenye tume ama ulaji . Shida ni kwamba hatuna Wazalendo wala Uzalendo . Watu wana amini katika mimi na Umimi na si sisi na Tanzania na Katiba yetu . Ndiyo maana Mzee Es na CCM wote wanaogopa Mgombea Binafsi kumbe na JK anaiogopa zaidi ya Mzee Es .
 
Muganyizi

Umetoa maelezo mengi bila solution ya tatizo. Sasa unataka atuletee CV yake hapa then what? Tutaongea mwishowe tutanyamaza. Ndiyo maana ninaunga mkono tuanzishe utaratibu wa kamati maalumu ya kuwahoji hawa viongozi na huko ndiko atakopeleka CV yake na kuchunguzwa kama anafaa kupewa kazi.

At least tuna sehemu ya kuanzia na kama kuna matatizo na hiyo kamati tutayatafutia ufumbuzi huko mbeleni. Kama tungekuwa wastaarabu zaidi tunaweza kukipa chama cha upinzani chenye wabunge wengi kura ya VETO. Na hiyo kamati itokane na viongozi wanaochaguliwa na wananchi kama wabunge siyo kuteuliwa na rais. Hayo ni mawazo tu siyo lazima iwe hivyo kama Mzee Muganyizi una mawazo mengine toka hapa lengo ni kuondoa matatizo ya kisiasa na kuanze kupambana matatizo ya kiuchumi yanayotukabili zaidi.

Muganyizi umenikumbusha huko nyuma tulipokuwa tunazungumzia matatizo ya vyama vya upinzani, utasikia oh CCM haijafanya kitu miaka zaidi ya 40, wezi, wala rushwa, n.k mwishowe wananchi wanabaki wanajiuliza then what do you want us to do? Hawaelezi ni kivipi watafanya tofauti na CCM. At least Mbowe anaelezea jinsi atavyobadilisha the government structure anatakiwa aangalie ni kivipi atawaelezea wananchi wakamuelewa.
 
Sam
Kwa sasa tunaelezea mawazo yetu na kuonyesha mahangaiko yetu juu ya utendaji wa Serikali . Baada ya hapo naamini tunaweza sasa kuanza kutafuta suluhu hapa hapa maana si JK wala Serikali yake itakuwa tayari kupokea na kuyafanyia kazi mawazo haya . Hawawezi kuunda chombo na kikiundwa bado hakitakuwa jibu nimesha sema kwamba wote watakuwa wanateuliwa ama na Rais ama katiba itatoa nafasi kwa 3wao kuwepo.Lakini bado watakuwa wanajibu kwa mkubwa wao na wako tayari kukutosa na kuendelea kujikita .

Jibu la haya ni watu kwanza kuwa Wazalendo kwamba waipende Tanzania kwa dhati na kuheshimu Katiba ya Nchi , kwa sasa ndilo naomba na hii ndiyo solution. Leo JK anamchagua rafiki yake wanaenda sote msikitini ama kama huyu Bos wa unusaji ambaye alikuwa namfikisia vimwana tutaishia kusema kama anachapa kazi tumwache then wanavurunda mbeleni na inakuwa hali mbaya zaidi then what ? Ni uzalendo unatakiwa kwanza . Uiweke Tanzana mbele na si zaidi ya hapo then tutaweza kuwa na kamati ama chombo cha kuweza kuwahoji hawa wateuliwa .

Tuna PCB in place lakini haina Wazalendo na inaendesha kisiasa sana na matokeo yake Waziri Mkuu juzi katangaza Bungeni kwamba walio kula siku hizo wamepona ila atakaye anza kula sasa atakiona.What does it mean ?
 
Muganyizi,
Yote hii ni danganyatoto. Nani asiyejua mali alizo nazo Waziri Mkuu? Na alizipataje? Kama kweli tunataka tatizo la rushwa likomeshwe lazima iundwe Tume ya Ukweli nchini ambayo itakuwa na mamlaka ya kuwahoji viongozi wote walipataje mali zao. Siyo kusema wale walioiba siku hizo wamepona na watakaoanza sasa ndio watakaokiona.
 
Status
Not open for further replies.
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom