Rashid Matumla , Bingwa wa ndondi na shujaa wa Taifa aliyegeuka Janga.

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
82,212
2,000
Hakuna asiyeufahamu umahiri wa Rashid Matumla katika ndondi , huyu ni kati ya mabondia wachache sana walioliletea Taifa hili heshima kubwa sana .

Lakini kama ilivyo ada , katika kila jema kuna upande wa pili wa mabaya , Baada ya kupata umaarufu ule , Rashidi akaamua kuzaa watoto wasio na idadi , mithili ya kufyatua matofali kwenye mashine ya umeme .

Ana watoto zaidi ya 10 , ambao ameshindwa kuwatunza na wamegeuka WAKABAJI , ( Mkazi yeyote wa keko anaweza kuthibitisha )

Ukabaji ninaoumanisha hapa ni ile tabia ya vijana vibaka na mateja maeneo ya uswahilini , kuamua kuvizia na kuwakaba na kupora mali za wananchi , hadharani na gizani , kwa maana nyingine ni kwamba Rashid Matumla ameleta kundi la wakabaji kwenye mitaa ileile aliyokuwa akisifiwa kwa ushujaa wake , jambo linaloleta aibu kwake mwenyewe na kwa wote waliomsaidia kuwa bingwa .

Wito kwa wanamichezo wa Tanzania kuweni makini sana na umaarufu wa kupita , angalieni mbele zaidi , msije dhalilika kama Rashid
 
Pakawa

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
6,606
2,000
Hakuna asiyeufahamu umahiri wa Rashid Matumla katika ndondi , huyu ni kati ya mabondia wachache sana walioliletea Taifa hili heshima kubwa sana .

Lakini kama ilivyo ada , katika kila jema kuna upande wa pili wa mabaya , Baada ya kupata umaarufu ule , Rashidi akaamua kuzaa watoto wasio na idadi , mithili ya kufyatua matofali kwenye mashine ya umeme .

Ana watoto zaidi ya 10 , ambao ameshindwa kuwatunza na wamegeuka WAKABAJI , ( Mkazi yeyote wa keko anaweza kuthibitisha )
Ni kweli kabisa. Keko si mahali salama hata kidogo ukitembelea maeneo yale utatembea kwa woga sanaaa!
 
Sooth

JF-Expert Member
Apr 27, 2009
3,921
2,000
Hakuna marefu yasiyo na ncha. Enzi zake ilikuwa ukienda PTA au Diamond kwenye pambano la ngumi lazima ukute Matumla kama watatu wanapigana siku hiyo na wote wanashinda, mpaka unanuna. Ujio wa cheka kidogo ulileta upinzan kwa jamaa.

Nadhan kushuka umaarufu wa ndondi nchini kumechangia hao watoto wake kujiingiza kwenye uhalifu. La sivyo wote hao wangekuwa kwenye gym ya familia wanajifua na kusubiri siku ya mechi wapigani. Wapi Mbwana? Wapi Mkwanda?
 
Taarifa zinadokeza kwamba Mbwana tangu atoke jela nje ya nchi kwa kosa la kufanya biashara ya " Makinikia " , mentally hayuko vizuri sana .
 
Sooth

JF-Expert Member
Apr 27, 2009
3,921
2,000
Taarifa zinadokeza kwamba Mbwana tangu atoke jela nje ya nchi kwa kosa la kufanya biashara ya " Makinikia " , mentally hayuko vizuri sana .
Sure, nimekumbuka nilisikia yuko South kwenye ngumi. Kumbe ni makinikia! Alikuwa bondia mzuri sana kama kaka yake.
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
82,212
2,000
Hahah hahah kwa hiyo kaleta janga kulalamika haitasaidia tafakari namna yakuwasaidia
Hawana ujuzi wowote ule utawasaidiaje ? Ni hivi , vijana wengi wa Keko Magurumbasi , Keko Mwanga , keko Machungwa na Keko Torori mwisho wa elimu yao ni darasa la 7 tu .
 
Sooth

JF-Expert Member
Apr 27, 2009
3,921
2,000
Nchi hii inalostisha sana watu wanaofanya kazi za vipaji. Mimi naamini Rashid Matumla ni mkali kuliko Mayweather na angekuwa mbele huko angekuwa bilionea. Matumla hakimbii ulingoni, anamfuata mpinzani wake karibu kabisa. Alinichosha siku amekwepa ngumi 8 za Cheka point blank-ilikuwa anazama, anainuka. Hatari sana. Ngumi za hivyo hata ulaya huzioni, aliondoka nazo Tyson.

Nimemkumbuka na Chaurembo Palasa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom