Rashid Lema Afariki Dunia

Mambo Jambo

JF-Expert Member
Jul 11, 2008
1,100
81
Yule mshitakiwa wa 11 wa kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva teksi mmoja Rashid Lema amefariki dunia.

Huyu jamaa alikuwa ni miongoni mwa maaskari walioshitakiwa pamoja na Bw Zombe.
 
Last edited:
Yule mshtakiwa wa 11 katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva wa teksi, jijini Dar es Salaam, Koplo Rashid Lema, amefariki dunia leo katika hospitali ya Ocean Road, Dar es Salaam.

Koplo Lema ni mmoja wa washtakiwa tisa katika kesi hiyo, akiwemo mshtakiwa namba moja, Abdallah Zombe, ambaye alikuwa mkuu wa upelelezi wa Dar es Salaam na ambaye wakati wa mauaji hayo alikuwa akikaimu nafasi ya Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam.

Lema, ambaye ni shahidi muhimu wa utetezi kulingana na maelezo yake ya awali katika kesi hiyo, alilazimika kulazwa hospitali ya Muhimbili kabla ya kuhamishiwa Ocean Road. Kabla ya hapo alilazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke.
 
Yule mshtakiwa wa 11 katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva wa teksi, jijini Dar es Salaam, Koplo Rashid Lema, amefariki dunia leo katika hospitali ya Ocean Road, Dar es Salaam.

Koplo Lema ni mmoja wa washtakiwa tisa katika kesi hiyo, akiwemo mshtakiwa namba moja, Abdallah Zombe, ambaye alikuwa mkuu wa upelelezi wa Dar es Salaam na ambaye wakati wa mauaji hayo alikuwa akikaimu nafasi ya Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam.

Lema, ambaye ni shahidi muhimu wa utetezi kulingana na maelezo yake ya awali katika kesi hiyo, alilazimika kulazwa hospitali ya Muhimbili kabla ya kuhamishiwa Ocean Road. Kabla ya hapo alilazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke.


Duh sasa hakuacha ushahidi wake kimaandishi au amefariki ghafla?

Upumzike kwa amani Mzee Lema
 
Apumzike kwa amani!kwa hiyo kina Zombe wamepona naamini zombe anafurahia tu sasa hivi!du hii dunia hii sio fair kabisa
 
ilikuwaje akawekwa gereza moja na zombe? lazima alilishwa polium III
 
Kuna taarifa yule shahidi kwenye kesi ya Zombe Mr. Lema, amefariki dunia na kwa wataalamu wa sheria mwasema je?
 
Hii ndio tanzania...sijui sasa zombe atashidwa kwa ushahidi uup kwenye hali tata kama hii huyu mtu alitakuwa kuwa ameandika ushahidi wake kwa maandishi....sujui protol uko nyumbani zinakwendaje.
Mtu alikuwa anazidi kuwa na hali mbaya...kwa kesi ya mauaji madaktali walitakiwa wametoa taarifa kuwa mgojwa ana hali hii kwa kuwa ni shihidi muhimu....hatuwezi hata kuangalia na wenzetu wanafanya nini...backup plan zinakuwepo.
 
Kesi itaendelea na hukumu itatolewa. Tayari mahakama wana ushahidi wa kutosha wa nani mwenye kosa. Ushahidi wa Lema ni ushahidi kama ambavyo umeshatolewa na wengine pale na pia upelelezi ulikuwa umeshapata maelezo yake. Mojawapo ya maelezo yake ni kuwa LEMA ALIAGIZWA KWENDA MSITU WA PANDE NA KAZI YAKE KAMA DEREVA ALIBEBA ZILE MAITI. SASA AMRI HIYO ALIPEWA NA NANI, BASI NI HAPO UMMA ULISUBIRI ATAMKE HIVYO KWA KINYWA CHAKE. Pale ilikuwa ni kuutamkia umma tu na kwa record ya mahakama. Kama kuna anayefurahia kifo hiki (kati ya wahusika wa mauji) basi wajue si suluhisho la wao kuwa innocent. Of course, mlolongo mzima wa tukio la kuuawa wale innocent businessmen unaeleweka na wahusika pia, labda tu mahakama iweke pamba masikioni au kutotamka yale ya haki. Hata hivyo, namwanini sasa Mh. Masatti, hatakuwa na upendeleo!!!
 
Last edited:
ilikuwaje akawekwa gereza moja na zombe? lazima alilishwa polium III


Jamani gereza sio 'hall', kuna vyumba vinaitwa 'cells' ambazo wafungwa wanalala. Hivyo CPl Lema kuwekwa gereza moja na Zombe haimanishi kulala katika 'cell' moja. Hata hivyo pande zenye 'conflict of interest' haziwekwi katika 'cell' moja kwa sababu za kiusalama.
 
RIP Lema, ila kwa watu makini na wanaofikiri beyond capacity, hii kesi sasa imeharibika, tena imeharibiwa makusudi kabisa kuwalinda polisi wauaji. Mimi bado ninaamini kuwa pamoja na usemi wa kifo ni mapenzi ya mungu, ila hapa kwa huyu shujaa inanifanya niamini kuwa huyu bwana alipewa sumu, slow poison, na ndiyo maana wakaamua kuahirisha mashitaka ili wasubiri afariki, kama mahakama huwa zinahamia hospitali kuwasomea mashitaka madereva waliosababisha ajali, kwa nini ilishindwa kufanya hivyo kwa Lema kipindi kilekile alichokuwa anatembea mwenyewe kwa kuchechemea kwenda mahakamani?, Tanzania x 110e110!
 
Last edited:
Hapa kesi imekwisha!maana wale mashahidi wanaofatia walikuwa wanategemea ushahidi wa lema "RIP"
 
ilikuwaje akawekwa gereza moja na zombe? lazima alilishwa polium III

Hatuna sana uhakika na hili kwa kuwa awali kabisa watuhumiwa hawa waliwekwa magereza tofauti (Keko na Ukonga). Baadaye wengine walitoka Ukonga na kujumuisha Keko. Ukonga wapo waliobaki. Natumaini mtuhumiwa Jane atakuwa Segerea (ambako kuna cells za wanawake). Hata hivyo, baada ya Lema kuwa Keko ni kwamba kwanza watuhumiwa hawa wanaishi tofauti na mahabusu wengine, wana cells zao special ambazo haziingiliani kabisa na mahabusi wengine. Zombe anakaa cell ambayo inamtenganisha kwa kiasi kikubwa na watuhumiwa wengine. (nikimaanisha hawakutani katika sitting room, only tu wakati wanakutana na ndugu zao kuchukua chakula hapo si rahisi kuwatenganisha na si rahisi kuweza ku temper na chakula cha mwenzako (wanachungwa sana). Watuhumiwa wengine wanakaa cells ambazo wana share a sitting room (ambayo ina TV na wana sehemu za kuchezea vitu kama karata, etc). Cells hizo ni self contained with a bed and a toilet. Kuna wengine wanashare a room ( four of them).

Hata hivyo, Lema na ndugu zake walikuwa wanalalamika kuwa ugonjwa wa ndugu yao si wa kawaida, pengine kuna mkono wa mtu. Ni vema tukubali majibu ya vipimo vya wataalam kuliko speculations and hearsays, kitu ambacho Lema mwenyewe na ndugu zake walikikataa kukubali!!!!

R.I.P Rashid Lema.
 
Apumzike kwa Amani,ila imenisikitisha sana sana,Nawapa familia yake pole,Mungu awafariji katika kipindi hiki cha majonzi ya kuondokewa na mpendwa wao.
 
Kwa kifupi tumuombee apumzike kwa AMANI, lakini inatia shaka, kama vile njama!
 
Tatizo hapa litakuwa ni kusema nani anahusika lakini mazingira ya kuugua hadi kifo yanaonesha pasipo hata shaka lolote kwamba jamaa ameuawa ili kujaribu kupoteza nguvu za ushahidi wake wa maandishi/maungamo. Ila natumai Jaji atatumia busara kuupa umumuhi ushahidi wa Lema kwani aliamua mwenyewe kuungama kwa mlinzi wa amani. Na kama hilo litatokea basi Zombe na wenzake itabidi watafute tundu jingine la kutokea. RIP Rashid Lema. Kazi uliyoifanya ya kusema ukweli, nina hakika Mungu atakusamehe.
 
Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake tutarejea. Sasa yule mshitakiwa aliyesema hawezi kujitetea mpaka huyu marehemu aseme maneno fulani wakati wa kujitetea sasa itakuwaje?.
 
Mwenyezi Mungu ampuzishe salama. (R.I.P)

Tusitafute mchawi hapa; Kila nafsi itaonja maiti, huyu naye siku yake imefika kesi itaendelea na wenye hatia tutaona matokeo yake.

Kwa mfumo wa mahakama zetu, haihitaji kumuua shahidi ili ushinde kesi, kiasi kidogo tu cha rushwa kinatosha kulainisha mambo.
 
Kalale pema Lema. naamini kuwa yule mwenzako bado ana ujasiri wa kueleza kilichotokea
 
Back
Top Bottom