Rashid Kitambulio, Mkurugenzi wa zamani wa Halmashauri asota gerezani kwa kukosa dhamana

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Mkurugenzi wa zamani wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha, mkoani Kilimanjaro, Rashid Kitambulio anaweza kuwa mmoja wa vigogo wa Serikali aliyefunga mwaka 2021 vibaya kwa kusota mahabusu kwa siku 7.

Kitambulio na wenzake wawili, Stanley Coola na Godson Lema walifikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi wiki iliyopita na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wakikabiliwa na makosa ya uhujumu uchumi.

Walishtakiwa kwa makosa wanayodaiwa kuyafanya wakati wa uchaguzi mkuu 2015, wakati huo Kitambulio akiwa msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Siha, huku Coola na Lema wakiwa wasimamizi wasaidizi na yalihusu matumizi mabaya ya fedha.

Hata hivyo, Mahakama hiyo chini ya Hakimu Mkazi mwandamizi, Sophia Masati haikuwa na mamlaka ya kusikiliza maombi ya dhamana kutokana na kiwango cha fedha wanachotuhumiwa kuisababishia hasara Serikali kuzidi Sh10 milioni.

Kupitia kwa wakili wao, Elia Kiwia waliwasilisha maombi ya dhamana Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Moshi, ambapo juzi Jaji Safina Simfukwe aliwapa dhamana kwa masharti ya kutoruhusiwa kutoka nje ya Kilimanjaro bila kibali.

Katika maombi yao, walisema kutokana na misingi ya haki ya asili, wanaamini kuwanyima dhamana watu wasio na hatia kama wao siyo sawa.

Upande wa Jamhuri ukiongozwa na wakili mwandamizi wa Serikali kutoka ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS), Kassim Nassir hawakuwa na pingamizi, isipokuwa waliomba izingatie masharti ya dhamana katika sheria ya uhujumu.
 
Wapi wameandika amekosa dhamana? Una copy na kupaste tu halafu macho yko Yana makengeza?
 
Mkuu wa Wilaya wilaya ya Tanganyika , Onesmo Buswelu naye ni mtuhumiwa kwenye sakata la wizi wa fedha za serikali huko siha Tanzania. Aunganishwe tu
 
Back
Top Bottom