Ras Nas aka Nasibu Mwanukuzi ndani ya Trondheim, Norway | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ras Nas aka Nasibu Mwanukuzi ndani ya Trondheim, Norway

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Rungu, Dec 8, 2008.

 1. Rungu

  Rungu JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2008
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 3,873
  Likes Received: 999
  Trophy Points: 280
  Mwanamuziki mkongwe wa miondoko ya muziki wa dansi na reggae, Ras Nas aka Nasibu, yuko tayari kufanya vitu vyake katika jiji la Trondheim, Norway, usiku wa Ijumaa tarehe 12 Desemba. Ukumbi unaitwa Dokkhuset.

  Kwa wabongo mliopo huko msikose kuhudhuria onyesho hilo la mwaka ambapo Ras Nas ametayarisha kikosi kikali chenye wanamuziki toka Congo Brazzaville, Ivory Coast na Sweden.

  Kwa tahadhari, asiye na mwana itabidi aelekee jiwe! Shoo itaanza saa nne na nusu usiku. Kabla ya hapo maDJ Roar Lund na Kristin Skjervold watakuwepo uwanjani kufyeka msitu.

  Kwa maelezo zaidi www.rasnas.kongoi.com (kiinglish)

  [​IMG]
  Ras Nas aka Nasibu Mwanukuzi

  WWW.KONGOI.COM
   
Loading...