Ras Mtimanyongo: Kimsingi Kariakoo ni eneo la sokoni (Wamachinga) tangia Uhuru, Wafanyabiashara kwao ni Samora na Kitumbini

Machinga ni social chaos, inapigiwa debe na wanasiasa waliofilisika kisiasa na wamejikuta wana madaraka but they cant think of the future of Tanzania.
Chadema ndio waliwatumia wamachinga kupata kura za ubunge Dar es salaam 2015.

CCM inashughulika na wamachinga kisayansi zaidi ndio maana inawapanga " vizuri "
 
Msanii Ras Mtimanyongo anasema kamwe Wamachinga hawawezi kuondoka Kariakoo kwa sababu ndio sokoni kuanzia nchi hii ijitawale.

Mtimanyongo anasema Wafanyabiashara kwao ni Samora zamani Independence avenue na Kitumbini na ndio maana hadi sasa hata vijiduka vya kariakoo ni vya ujanja ujanja tu.

Mtimanyongo anasisitiza kuwa kifuatacho kiwe TRA kusaka maghala ya hao wajanja wajanja wa kariakoo huko Vingunguti na Buguruni kama kweli wanataka kukusanya kodi.

Mungu ni mwema wakati wote!
Hiki alichoandika ndiyo wimbo wake mpya? Haya wenye biti mtengenezeeni.
 
Nakubaliana na Ras, tangia nimeijua kariakoo ni eneo la umachinga na biashara za ujanja ujanja.......hakuna bishara rasmi kule, kwa hiyo kariakoo kwa wamachinga ni kwao.
 
Nchi hii kuna watu wa ajabu sana, yaani siku maisha yenu yakiguswa ndio mnapata akili? Nyakati za uchaguzi hata kupiga kura hamuendi hayawahusu, Watu wanatiwa mageza kwa kuvaa T-Shirts zilizoandikwa katiba mpya ninyi mnasema katiba haiwahusu. Tulieni dawa iwaingie mjisaidie wenye nkwani mambo yenu hayatuhusu sisi.

Mnashindwa kuelewa kwamba tungekua na katiba mpya tungepata viongozi wazuri ambao wangetii sheria wasingewaruhusu mfanye biashara kiholela, wangewajengea masoko mazuri. Sasa amekuja kiongozi mwingine,yeye anataka kufuata sheria mnatakaje? Acheni unafki unganeni na wanaharakati mbali mbali nchini kudai katiba mpya itakayowapa mwongozo mzuri wa kuendesha biashara zenu kiutaratibu mpate faida
 
Acha kuendeshwa kisiasa tii sheria na miongozoo iliyowekwa usihamasishe wamachinga wakaingia barabarani shame in you
 
Matatizo ya watu ndio mitaji ya wanasiasa.

Kwahiyo kukiwa na katiba mpya ndio machinga wanakuwaje 🤣🤣 ???
 
Back
Top Bottom