Ras Makunja Mnatumaliza Sheria Inawaruhusu Kuua?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ras Makunja Mnatumaliza Sheria Inawaruhusu Kuua??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Feb 23, 2012.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hivi hawa kina ras makunja wanaruhusiwa kuua au wanachotakiwa kuvunja mguu au mkono sijui sheria inasemaje hapa maana kila maandamano unakuta wanaua raia kwa risasi za moto ubinadamu upo kweli hapo??kwa mfano hawa raia wanaouawa ingekua wanavunjwa miguu au mkono tu mie nadhani lawama na uadui kati ya raia na wao vingepungua.....hii sheria kuua ingeangaliwa upya Mungu aliyetuleta hapa duniani sidhani kama anapendezwa na hili wasiwasi wangu kitakachofuata ni laana........viongozi tunao na ishu zenyewe ndogo sana na zinaweza kufanyiwa ufumbuzi kirahisi tu tatizo akili tulizopewa na mungu hatuzitumii kabisa kwa maslahi ya tunaowaongoza bali tunatanguliza umimi mbele na nguvu juu ishu ya songea inasikitisha sana haikuangaliwa mwanzoni tatizo lilipoanza tumefanya mzaha ona sasa watu wamepoteza maisha kizembezembe tu.Angalia migogoro ya kwenye migodi wanaua,maandamano ya Arusha waliua yaani sijui hiki kipengere cha kuua wamekitoa wapi kama kipo napendekeza kifutwe vinginevyo uadui na chuki dhidi ya hawa jamaa vitaendelea kuwepo.....na kukua
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Hawa kina Ras Makunja wanapenda sifa hasa wakibeba magitaa yao ndio wanajifanya wana nguvu na ndio maana wanaweka urasimu kwa raia kumiliki mguu wa kuku.
   
 3. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Bora hata majambazi wenyewe uwa wanapga juu watu mnalala chini askari wanaroho mbaya kuliko ibilisi wakatili elimu finyu weng walifeli shule na upeo wao wa kufikiri ni mfinyu.jambaz akiuwa mtu ujue walidhamiria au mapambano yalikuwa makali
   
 4. mshana org

  mshana org JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 2,102
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  Tatizo wanatuzarau na nch imeshakua yao kwakua hata wakiua raia kizembe serikal haichukui action yoyote.katiba iko wazi polisi hana kibali cha kuua mt kama mtuhumiwa nae hana silaha ya moto mimi nashindwa kuelewa uwezo huu wanaupata wapi?ila ninachokiamini ni kua serikali wanatulisha sumu ya chuki na ujasiri zaidi kwakutuzoesha silaha na mabom.siku ambayo watz wote watakua wamezoe kutoogopa hizo silaha zao kama ilivyo kwa mikoa ya arusha mbeya na kanda ya ziwa.inch hii haitatawalika tena.
   
Loading...