- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Salaam wakuu,
Leo nimekutana na hiikuhusu jua naomba kupata uhalisia wake.
Je ni kweli kwamba jua lina rangi nyeupe ilihali asubuhi tunaweza kuona rangi kama ya njano, chungwa, nyekundu na kadhalika.
Leo nimekutana na hiikuhusu jua naomba kupata uhalisia wake.
Je ni kweli kwamba jua lina rangi nyeupe ilihali asubuhi tunaweza kuona rangi kama ya njano, chungwa, nyekundu na kadhalika.
- Tunachokijua
- Jua ni nyota kubwa ambayo ipo umbali wa kilometa milioni 150 kutoka katika sayari ya dunia, likiwa ni chanzo muhimu zaidi cha mwanga duniani na hata kuchochea mabadiliko ya hali ya hewa, misimu, tabia ya nchi, lakini kuchochea ukuaji wa mimea kupitia kitendo kinachojulikana kama “Photosynthesis”
Kumekuwepo na hoja mbalimbali juu ya uhalisia wa rangi halisi ya jua ikitajwa kuwa rangi ya jua kuwa ni nyeupe na wakati mwingine kuwa njano, nyekundu, chungwa na kadhalika.
Je uhalisia wa jambo hili ni upi?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck uliopitia vyanzo mbalimbali umebaini kuwa rangi halisi ya jua ni nyeupe ambayo inahusisha mchanganyiko wa rangi mbalimbali na kuonekana nyeupe.
Inaelezwa kuwa ni dhana potofu kwamba Jua lina rangi ya njano,chungwa au nyekundu. Hata hivyo, Jua linahusisha rangi zote zilizochanganyika, ambazo zinaonekana kwa macho yetu kama nyeupe.
Dkt. Christopher S. Baird, professa aliyebobea katika masuala ya fizikia katika chuo cha West Texas A&M University, ambaye pia ni mwandishi wa kitabu cha maswali 50 ya sayansi yenye majibu ya kushangaza anaeleza kuwa rangi ya jua ni nyeupe. Jua linatoa rangi zote za upinde wa mvua kwa kiwango sawa, mchanganyiko huo kuitwa nyeupe (white) Ndio maana tunaweza kuona rangi nyingi tofauti katika ulimwengu wa asili chini ya mwangaza wa jua, Kama mwanga wa jua ungekuwa wa kijani basi kila kitu kingeonekana ni cha kijani.
Tunaweza kuona rangi ya kijani na nyekundu kupitia mabawa ya nzi yanapopigwa na miale ya jua kwa sababu linahusisha mchanganiko wa rangi hizo kadhalika kwa rangi zingine.
Wakati wa mawio na machweo kuenea kwa bluu na zambarau kunaweza kuonekana kiasi kwamba jua linaweza kuonekana kuwa na rangi ya njano, machungwa, au hata rangi ya shaba. Lakini uhalisia ni kwamba jua lenyewe ni jeupe. Jua ni jeupe linapotazamwa kutoka angani na pia ni jeupe linapotazamwa kutoka uso wa dunia (isipokuwa muda mfupi wakati wa alfajiri na machweo). Hata likitazamwa kutoka uso wa dunia, jua halionekani kuwa lenye rangi ya njano.
Asubuhi na jioni jua huonekana kuwa na rangi nyekundu, kwa sababu miale ya mwanga wa jua husafiri umbali mrefu zaidi angani ambapo husababisha kusambaa kwa rangi ya njano pia.
Tovuti ya National Aeronautics and Space Administration ya nchini Marekani inabainisha kuwa Mtazamo wetu wa rangi unategemea, urefu wa wimbi la mwanga unaotolewa, nguvu ya mwanga unaotolewa, sababu za kimazingira, uwezo na ukomo wa macho yetu kukusanya mwanga.
Aidha wataalamu wanaonya kulitazama jua moja kwa moja ila vifaa maalumu kuwa ni hatari kwani kunaweza kusababisha kupofuka kwa macho.