Rangi Nyekundu kwenye bendera ya CHADEMA ina maana gani?

jov

Senior Member
Aug 20, 2012
121
170
eri...hivi unaelewa tatizo humuJR watu hampotiari kuelewa unanipa uzi ambao umejaa marumbano na nembo ya tanzania mtu anauliza mbona ipo nyekundu nani kauliza nyekundu tu .mzee jipange hujatoa suruhisho hapo
 

bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,702
2,000
jamani watu tupo serius kwanini bendera ya chadema ina rangi nyekundu?
rangi ile inamaabisha nini?
 

Nicholas J Clinton

Verified Member
Mar 13, 2014
859
500
Bendera hii ni ya pekee miongoni mwa vyama vya siasa barani Afrika na kwa macho inavutia inasemekana ilibadilishwa na kamanda wa anga MBOWE katika mfumo na mpangilio wa rangi zake. Sasa naomba kujua rangi zake ambazo ni Nyekundu, Nyeusi, Nyeupe na rangi ya Bahari zina maana gani each colour kwa rangi nyekundu imekuwa ikutumika vibaya hasa kwa vijiji kuwa inaashiria damu na mwisho naomba kujua vazi la gwanda ambalo lina rangi ya kaki ni maana yake ni nini?
 

MUSSA ALLAN

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
18,932
2,000
- Rangi nyekundu inamaanisha damu, ndio maana kila penye mkusanyiko wa CHADEMA lazima damu imwagike.

- Combat ni ishara ya vita.
 

The hammer

JF-Expert Member
May 17, 2011
2,308
2,000
Bendera hii ni ya pekee miongoni mwa vyama vya siasa barani Afrika na kwa macho inavutia inasemekana ilibadilishwa na kamanda wa anga MBOWE katika mfumo na mpangilio wa rangi zake. Sasa naomba kujua rangi zake ambazo ni Nyekundu, Nyeusi, Nyeupe na rangi ya Bahari zina maana gani each colour kwa rangi nyekundu imekuwa ikutumika vibaya hasa kwa vijiji kuwa inaashiria damu na mwisho naomba kujua vazi la gwanda ambalo lina rangi ya kaki ni maana yake ni nini?

Unaweza ukagoogle ukapata jibu,ila kwa kuwa mnapenda kutafuniwe ninyi Watanzania ngoja nikuwekee.

BENDERA MPYA YA CHADEMA
​Muundo wa Bendera

1. Bendera ya CHADEMA ina rangi nne: Nyeusi, Bluu isiyokoza (light blue), nyeupe na nyekundu.
2. Bendera ya CHADEMA ina nembo ya kiganya cha mkono kilichonyoosha vidole viwili katika mfumo wa V kama ishara ya USHINDI. CHADEMA ni chama kinacholenga kushinda kidemokrasia na hatimaye kuleta ushindi wa maendeleo ya taifa.
3. Rangi ya BLUU ISIYOKOZA iko juu ya rangi NYEKUNDU kama ishara kwamba kama taifa tumevushwa na mashujaa kuelekea katika jamii yenye haki, na wakati wote CHADEMA imevuka hatua kama chama cha siasa na sasa inasimamia haki.
4. Rangi nyeupe iko mbele ya rangi zote kama ishara kwamba chama kinatanguliza UKWELI NA UWAZI katika nyanja zote. Pia rangi nyeupi imebeba nembo ya chama kwa kuwa UKWELI NA UWAZI ni misingi muhimu sana kwa chama. Nembo ya chama iko mbele kama kama ishara ya CHADEMA kuwa chama kiongozi katika kuchochea misingi muhimu katika kuleta mabadiliko na maendeleo katika Taifa.
5. Rangi zingine zinatenganishwa na ufito mweusi ambao unaumbo la “T” ikiwasilisha kifupi cha jina la taifa la Tanzania.

Rangi za Bendera
NYEUSI
Rangi hii inawakilisha WATU WA TANZANIA. Hii ni rangi ya wazawa asili wa nchi yetu. Ni rangi ambayo inabeba pia falsafa ya NGUVU YA UMMA.
BLUU ISIYOKOZA (LIGHT BLUE)
Hii ni rangi ya asili ya CHADEMA. Ni rangi ambayo inawasilisha HAKI. Lakini pia rangi hiyo inawakilisha BAHARI kama ishara ya maliasili/raslimaji na Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar.
NYEUPE
Rangi nyeupe inawasilisha UKWELI, UWAZI na AMANI. Huu ni msingi muhimu wa CHADEMA. CHADEMA ni chama ambacho kitasimamia uadilifu kwa njia ya demokrasia.
NYEKUNDU
Rangi nyekundu inawakilisha MASHUJAA. CHADEMA inathamini historia ya nchi yetu ambayo inawasilisha kumbukumbu ya mashujaa waliotupitisha katika michakato ya mbalimbali ya demokrasia na maendeleo ikiwemo harakati za kuondoa ukoloni. Rangi hii ni chimbuko la uzalendo wetu.

Miaka mingi iliyopita,Jemedari wa vita toka Urumi(Roma) Julius Caiser aliwavamia maadui zake na kuwapga kwa kusafil umbali mrefu,alipofika ktk himaya ya adui aliua na kuteketeza kila kilicho cha adui..kufikisha ujumbe kwa walio Rome na Senator J.Caiser alisema "Veni,Vidi,Vici" = "I came,I saw,I conquered".. Hii ndo ikawa alama ya ushindi,na J.Caiser alipopita mbele za watu alikunja vidole kwa alama ya V kama tafsiri ya ushindi,na askari wote waliopgana ktk vita hvyo waliwekewa alama ya "V" tatu ktk mabega yao kama alama ya ushujaa,na t oka hapo V ikawa alama ya cheo ktk jeshi...
 

tofyo

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
2,696
2,000
- Rangi nyekundu inamaanisha damu, ndio maana kila penye mkusanyiko wa CHADEMA lazima damu imwagike.

- Combat ni ishara ya vita.

mkuu na kwanini waliiweka mwaka 2004'

combat ni ishara vita basi kumbe ichi chama cha wanamgambo au waasi.
 

masopakyindi

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
15,352
2,000
Napenda kusikia maoni yenu juu ya rangi nyekundu kwenye bendera ya CHADEMA inayotumiwa kuandika signature ya Chadema huku ikiwa bolded na jina la chama hicho likiwa na muendelezo wa "aaaaaa" mwishoni.

Kuna lolote la ziada au ni ushabiki umekolea?

Naomba kujua kwa sababu maandishi na alama mara nyingi huashiria jambo hasa katika majukwaa ya kidini au siasa.
Chadema+flag.jpg
Mkuu inasemekana wazazi wa Mtei waliwapigania waingereza vita kuu ya pili, na wakamwaga damu zao kwa ajili ya mwingereza.
Ndo maana Kameruni anawapenda sana!!!!!!
 

NO EXCUSE

JF-Expert Member
Sep 10, 2012
417
250
Chadema+flag.jpg
Mkuu inasemekana wazazi wa Mtei waliwapigania waingereza vita kuu ya pili, na wakamwaga damu zao kwa ajili ya mwingereza.
Ndo maana Kameruni anawapenda sana!!!!!!

Raia toka makoloni ya nchi za ulaya kama vile Common wealth walikuwa askari kupigana na adui wa mkoloni wao. Je unalijua hilo au una jamba jamba tu hapa?
 

kirikuu10

JF-Expert Member
May 4, 2014
249
0
- Rangi nyekundu inamaanisha damu, ndio maana kila penye mkusanyiko wa CHADEMA lazima damu imwagike.

- Combat ni ishara ya vita.

kwani siku ya wapendanao huwa zinavaliwa ngua za rangi gani?? Nenda kasome tena shule uelewe maana ya rangi nyekundu maana hata kijana inatumika sana ICU.MOTUARY NA HOSPITALINI.
 

MAHORO

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
7,594
2,000
rangi nyekundu ina maana ya upendo, chama kinahamasisha upendo kila kukicha ili watz wawe wazalendo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom