Ramzan Kadyrov (shujaa na mbabe wa kivita) aonekana kwenye video ya ajabu akipigana na UFC Champion wa Kiswidi

Sikirimimimasikini

JF-Expert Member
Dec 27, 2019
2,919
15,604
Ramzan Kadyrov ameonekana kwenye video ya kustaajabisha na isiyo ya kawaida akipigana na kumgaragaza mswidi Khamzat Chimaev ambaye ni mtaalamu (professional) wa mieleka na mpiganaji wa staili mchanganyiko za martial arts ambaye ni Champion wa UFC (Ultimate Fighting Championship).

Khamzat Chimaev hapo kabla amewahi pia kupambana ktk Brave Combat Federation. Ktk mieleka, Chimaev ni mswidi ambaye amewahi kuwa champion kwa mara tatu.

Khamzat Chimaev amewahi pia nyakua ushidi wa UFC kwenye mapambano dhidi ya John Phillips, Rhys McKee, Gerald Meerschaert na Li Jingliang

Japo sina mafunzo.lakini nadhan naeza pigana zaidi ya hapo...labda ndio maana ukaiita "video ya ajabu"
 
Siku ingine ukiandika jina la huyo mwamba ramzan kadyroz mwisho malizia mujaheed huyo mtu ni tatizo America wanamjua vzr balaa lake slogan yake asema anapenda kufa kama watu wengine wanavyopenda kuishi
 
Muongo tu huyo, kama anapenda kufa angeshajifungia bomu kiunoni akajilipue huko Ukraine.
 
khamzat chimaev na huyo mvaa vipedo ramzan kadyrov ni washkaji wa mda mrefu sana hata page ya instagram ya khamzat keshampost sana kadyrov vilevile page nyingi za serikali ya hilo jimbo la chechen wamempost sana khamzat na kadyrov pia kadyrov ni mpenzi wa michezo hio lakini kwa uhalisia itamchukua khamzat chimaev sekunde 127 kumpeleka karyrov kaburini
 
Siku ingine ukiandika jina la huyo mwamba ramzan kadyroz mwisho malizia mujaheed huyo mtu ni tatizo America wanamjua vzr balaa lake slogan yake asema anapenda kufa kama watu wengine wanavyopenda kuishi
Chechniya walikua na Dudayev kama sikosei, huyu ndo alitaka kujitenga na Russia,, akaanzisha jihad dhidi ya Russia,,
Huyu Ramzan ni chechniya ambae alipigana upande wa Russia dhidi ya Mujahid, akina Dudayev,,
Dudayev aliwachachafya sana warusi,, lakini walikuja kunasa mawasiliano yake akitumia satelite phone kuwasiliana na makamanda wake ,, warusi walituma kombora, satelite guided missiles kwa kufuata coordinates za ilipokua simu ya Dudayev,, na ndo ukawa mwisho wa Dudayev,
Huyu Ramzan ndio sasa kiongozi wa chechniya,,
 
Back
Top Bottom