Program Manager
JF-Expert Member
- Aug 6, 2018
- 2,513
- 3,437
Namnukuu
Tukiacha ushabiki, kwa sasa Simba ina kikosi imara ndani ya uwanja na nje ya uwanja. Yanga hawana kikosi imara ndani ya uwanja wala nje ya uwanja.
Yanga kutaka kushindana na Simba kwa sasa ni uongo! Kwa mtazamo wangu, usajili wanaofanya Yanga sio kwa ajili ya kushindana na Simba kwa maana ya kuchukua ubingwa.
Yanga bado haijafanya vibaya kwa msimu ulioisha, imeshika nafasi ya pili kwenye ligi, imeishia nusu fainali kwenye Kombe la TFF huku ikiwa imetolewa na Bingwa wa ligi na amekuwa bingwa wa Kombe la TFF.
Yanga ipo kwenye process ya kujenga timu labda ili wapiganie nafasi ya kwenda kushiriki kombe la Shirikisho lakini sio kupigania ubingwa wa ligi.
Wachezaji ambao Yanga imewasajili hadi sasa bado watahitaji muda, sio mwezi mmoja au mitatu, huenda ikawa msimu mzima waweze kuelewa tamaduni za mifumo ya uchezaji wa Yanga. Hawezi kuipa Yanga kile inachotaka kwa haraka.
Wachezaji wote wamefanya vizuri kwenye vilabu walivyotoka, wanapokuja Yanga usitegemee viwango vyao vitakuwa vilevile kama kwenye vilabu walikotoka.
Yanga ni tofauti na Kagera Sugar, Mbao na Polisi, Yanga kuna presha ya mashabiki, watu wanataka ushindi asubuhi, mchana na jioni. Kwa hiyo itabidi wachezaji hao wapate muda.
Sitashangaa wachezaji ambao wanasajiliwa sasa hivi 80% wakaja kuachwa baada ya msimu ujao.
Mwisho wa kumnukuu