Rambirambi zinazotolewa kwa wafiwa Arusha ziwafikie walengwa

falcon mombasa

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
9,186
9,287
Wakuu habari,
Jamani mi naomba kuikumbusha serikali rambirambi zinazotolewa kwa wafiwa wa msiba huu mkubwa basi moja kwa moja zielekezwe kwa walengwa tusisikie pesa zinaenda kufanya miradi ya maendeleo.

Pia nimeshangaa sana kuona serikali imepeleka lori la jeshi kubeba watoto hawa japokuwa najuwa wengi hamjaliona ila nitaweka picha, lori hili si hadhi kabisa ya kuwabeba malaika hawa ina maana serikali imekosa kabisa gari hadi iwaweke malaika hawa kwenye lori ambalo turubai limechanika? Naweka picha muda huu.ila ni bora ingesema wadau tujitolee magari watoto hawa waagwe kifalme

Lori lenyewe ndio hili ,nadhani hata kamera za TV bado hazijanasa

IMG-20170508-WA0043.jpg
 
Serikali yetu imekuwa na utamaduni wa kuteka rambi rambi

Nakumbuka kauli ya kibabe ya mkuu wa nchi kutokana na kuteka michango ya wadau waliojitolea katika Tetemeko kule Kagera na pesa zote kupangiwa matumizi binafsi ya serikali

Hili tukio la ajari iliotokea karatu wadau wa huzuni wamejitolea michango ya mamilioni kwa wahanga na mkuu wa nchi hajaenda lakini anafatilia matukio kupitia clouds TV na clouds redio naamini baada ya mwezi atakwenda Arusha sasa nakuomba Kamanda hiyo michango ya wadau wa huzuni imebaki kuwa ya hao warengwa ukizivuta hizo kutoka kwa warengwa kama ulivyo zivuta za Kagera amini Arusha sio Chato....
2020 watakupiga na chupa za maji ya Kilimanjaro
 
Kama mtanzania, mzazi wa watoto wanne, nimeguswa sana na ajali pamoja na vifo vya wanafunzi, walimu na dereva wa Shule ya Lucky Vicent ya Arusha. Natoa pole za kutosha.Nami nimekuja kujumuika nao wafiwa na waombolezaji hapa Arusha. Nitatoa mchango wangu wa hali na mali katika hili.

Tayari, viongozi wa kiserikali wakioongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, wameshaanza kukusanya rambirambi kufuatia msiba huu wa watanzania wenzetu 35. Rambirambi kutoka kwa watu binafsi, mashirika na taasisi zinamiminika. Ni uungwana kutoa na kupokea.

Ni uungwana zaidi kufikisha rambirambi hizo, kwa mgawanyo sahihi, kwa walengwa. Walengwa ni wazazi wa watoto waliofariki; familia za walimu na dereva na shule husika. Katika wepesi huo wa kukusanya rambirambi, zifikishwe kwa walengwa.

Minong'ono ya kule Kagera isijitokeze katika msiba huu wa Arusha. Bwana ametoa, Bwana ametwaa!

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (msibani Arusha)
 
Back
Top Bottom