Ramani Ya Helligoland Treaty: Ziwa Nyasa Lote Liko Malawi

Plato

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
420
94
SAM_2666.JPG

Msije mkasema mimi ninakinyongo na msimamo wa serikali. Nimeona ramani hii inayoonyesha mipaka ya ziwa nyasa. Sasa nashindwa kujua ugumu unatokea wapi wakati kumbe mambo yako wazi kabisa.

Imetoka blog ya Mjengwa
 
Ni ukweli mchungu sana. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Ziwa lote ni la Wamalawi.

Watanzania hatutaki vita wala ugomvi na majirani zetu, kama tuna hoja tuwahi mahakamani sheria ichukue mkondo wake.
 
Ungeweka na hiyo treaty yenyewe inayotambua hivyo na saini zilizopigwa kuitambulisha ramani. Vinginevyo hata na wewe unaweza chora yako safari hii ziwa nyasa uliweke Tanzania halafu umwambie huyo mjengwa hiyo nayo ni ramani inayotambulika na helligoland treaty aibandike kwenye blog yake.
 
Treaty of 1890 between Great Britain and Germany concerning the border. A wrinkle in this dispute occurred when the British colonial government, just after they had captured Tanganyika from Germany, placed all of the waters of the lake under a single jurisdiction, that of the territory of Nyasaland, without a separate administration for the Tanganyikan portion of the surface. Later in colonial times two jurisdictions were established.[12] In 1954 an agreement was signed between the British and the Portuguese making the middle of the lake their boundary with the exception of Chisamulo Island and Lokoma Island which were kept by the British and are now part of Malawi.
 
..ramani inaonyesha Rwanda na Burundi ni eneo la Tanganyika.

..pia ramani inaelekeza kwamba Msumbiji nayo haina haki na maji/eneo la ziwa Nyasa.

..mwisho, ramani haionyeshi jinsi Tanganyika, Kenya, na Uganda, zinavyo-share ziwa Victoria.

..je, ina maana na sisi tuanze kudai Rwanda na Burundi ziwe ni mikoa ya Tanganyika??
 
Hatuwezi kufuata ramani zilizochorwa ulaya na watu ambao hawakuwahi kutia mguu Afrika. Ushahidi wa haraka ni kwamba Rwanda na Burundi si Tanganyika tena. Kama itatokea kuwa ziwa Nyasa ni mali ya Malawi pekee, basi litakuwa ni ajabu jingine la dunia.
 
Wee mzushi tu kwani mtu hawezi akaichora akatuwekea humu? Kwanza ramani yenyewe inaonesha imechorwa siku za karibuni wakati Heligolland ilisainiwa zamani.

W
 
Hapa nahisi kuna suala la kujadili, wanajamvi leteni mawazoyenu; Ramani ya Heligoland inaonyesha ziwa nyasa <malawi> liko malawi, je tuendelee kulidai kwa kutumia utashi wetu au mikataba ilyoingiwa na wakoloni?....hii inafanana sana na suala la maji ya ziwa victoria. Ofisi ya Membe ilisha wahi kuliona hili kama ni tatizo au imeshtulizwa?
 
Sasa hiyo ramani mbona ya kiduwanzi?
Wewe tuliza boli, kesi taenda mahakamani.
Watanzania walilitumia, wanalitumia na wataendelea kulitumia ziwa Nyasa.
Hakuna mahakama duniani itayowanyima wakazi wa pembezoni mwa ziwa Nyasa utumiaji wa ziwa hilo.
Swali ni asilimia ngapi ya ziwa itakuwa Tanzania, tuwape 60/40 au 70/30 tumalizane.
 
Tumevamiwa na Wamalawi humu. Tatizo ni ule tunaoita upendo wetu, mpaka tumewakaribisha vijana wa kimalawi kama vibarua wa kututengenezea bustani nyumbani na kusimamia mashamba yetu. Sasa washajua kiswahili na kuwa informers kwa serikali ya malawi.
 
Jamani haiwezekni nchimoja ichukue maji yote halafu wananchi wa nchi jirani wasipatemaji hivyo wakitaka maji waende kununua njeyanchi haiwezekeni hata ukimuuliza mtoto mdogo nilazima maji tugwane katikati w0te tunywemaji kwani wamewekwa na m/mungu hayakuwekwa na wamalawi unanisoma mtoa mada?.
 
Hii Ramani imechorwa Jana,
Ramani ya Mwaka 1885 haiwezi kua safi namna hii!!
 
Time will tell. Treaty ya Zanzibar-Heligo, na makubaliano ya Berlin Conference hayagawi ziwa lile kwa upande wowote; ningeshukuru sana kama ungeleta na articles za Berlin Conference Accord alongside hiyo Zanzibar-Heligoland treaty.
 
CHANGANYA NA ZAKO. Mbona husemi kwa mujibu wa hiyo ramani yako BURUNDI NA RWANDA ZIPO TANZANIA?
 
Ni ukweli mchungu sana. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Ziwa lote ni la Wamalawi.

Watanzania hatutaki vita wala ugomvi na majirani zetu, kama tuna hoja tuwahi mahakamani sheria ichukue mkondo wake.

Ziwa lote? Kwa hiyo hata Msumbiji hawana ziwa Nyasa?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom