Ramani ushahidi: Mbuga ya Burigi ipo pia Chato

state agent

JF-Expert Member
Jul 1, 2019
1,764
2,511
Nani anabisha kuwa haifiki chato ,hivi macho yenu yanaona sawasawa
FB_IMG_1562872377887.jpeg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 09 Julai, 2019 amezindua Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato iliyoundwa baada ya kuunganishwa kwa Mapori ya Akiba ya Burigi, Biharamulo na Kimisi yaliyopo katika Wilaya za Biharamulo, Ngara, Karagwe na Muleba Mkoani Kagera na Chato Mkoani Geita.

Hifadhi hiyo inakuwa ni ya 3 kwa ukubwa hapa nchini ikiwa na jumla ya kilometa za mraba 4,702, ikitanguliwa na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (kilometa za mraba 20,300) na Serengeti (kilometa za mraba 14,763).

Sherehe za uzinduzi wa hifadhi hiyo zimefanyika katika Kijiji cha Katete, Wilaya ya Chato Mkoani Geita na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri na Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Mabalozi wanaoziwakilisha nchi mbalimbali hapa nchini, Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Viongozi wa Dini, Viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Kabla ya kuzindua hifadhi hiyo Mhe. Rais Magufuli amekagua gwaride la Jeshi Usu la Wanyamapori na Misitu, ameshuhudia Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangallah akiwavalisha vyeo Makamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), amepokea tuzo ya Hifadhi ya Serengeti iliyopata ushindi wa kuwa hifadhi bora Barani Afrika kwa mwaka 2019 na tuzo ya Mlima Kilimanjaro ulioshinda kwa kuwa kivutio bora Barani Afrika kwa mwaka 2017 na pia amekabidhi vyeti kwa wawekezaji 6 waliotayari kuwekeza katika Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato.
 
kwa hizi evidence zilizoshushwa hapa sidhani kama utakubali tena kutumiwa na polepole kuja kupotosha hapa
 
Back
Top Bottom