Ramadhan Kabwili: “Simba walinifuata, nitafute kadi ya njano, wanipe IST mpya”

magnifico

JF-Expert Member
Jan 14, 2013
7,373
13,041
”Simba walinifuata, nitafute kadi ya njano,
wanipe IST mpya”, hayo ni maneno ya mlinda
mlango wa klabu ya Yanga, Ramadhan Kabwili
ambapo amesema kuwa uongozi wa Klabu ya
Simba umewahi kumlaghai ukimtaka atafute
kadi ili asiweze kucheza katika mchezo wa
watani wa jadi na kimuahidi akifanya hivyo
kumpatia garia iana ya IST.

Mlinda mlango huyo amesema hayo wakati
akifanya mahojiano na EATV Radio katika
kipindi cha Kipenga Extra mapema leo
Jumatatu ya tarehe 27, 2020.

“Simba waliwahi kunifuata kipindi tupo na
kocha Zahera, nilikuwa na kadi 2 za njano na
kwenye mchezo wa Yanga na JKT Tanzania,
walitaka nitafute kadi ya njano makusudi ili
wanipe gari ya IST mpya na nikose mchezo
ujao wa watani” – Ramadhan Kabwili.
Amesema kuwa tukio hilo lilitokea kipindi
ambacho Zahera akiwa kocha wa klabu hiyo ya
Yanga.

Amesema kuwa siku hiyo Yanga ilikuwa
inaelekea kucheza na JKT Tanzania na yeye
alikuwa na kadi mbili za njano, hivyo Simba
walimfuata na kumuambia kuwa atafute kadi
moja ya njano ili akose mchezo uliokuwa
unafuatia wa watani wa jadi huku wakimuahidi
kumpa IST mpya, wakiamini kuwa angekaa
Klaus Kindoki golini wangemfunga kirahisi.
Katika mchezo huo dhidi ya JKT Tanzania,
Yanga ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 ambapo
Ramadhan Kabwili ndiye alikuwa golikipa wa
Yanga siku hiyo.

Aidha Kabwili amesema kuwa kwa sasa ahitaji
meneja yoyote atakayemtafutia timu ya
Tanzania akitamani meneja ambaye atamtafutia
timu Ulaya, “mimi nataka meneja ambaye
atanipeleka kucheza soka la Ulaya, sitaki
meneja wa kunichezesha hapa nchini kwa
sababu kama ni hapa nchini sasa hivi nipo
katika klabu kubwa Tanzania na inashinda
mataji”.



Pia Rejea..




Source : Dar24
 
Kama tunataka kuondoa rushwa michezoni hapa ndio TAKUKURU wanapaswa kuanzia. Kabwili ni mtu mzima na kama kweli ametamka maneno hayo akiwa hajalewa au anatania ni wakati sasa wa TAKUKURU kufuatilia kwa Kabwili ili awape majina ya watu waliotaka kumhonga na wao wafanye uchunguzi wao kisha watuhumiwa wafikishwe mahakamani iwapo ushahidi utaptikana. Bila kuondoa vitendo vya rushwa michezoni hatutaweza kupiga hatua kuelekea kwenye mafanikio.
 
MO anapotishia kujiondoa Simba maanayake anaona anatumia fedha nyingi kwa mambo ya kipuuz. Timu anasajili kwa fedha ndefu,mishahara mikubwa bado na mechi anunue, marefa ahonge mwishoe anaona atafilisika bila sababu.
Mechi ya hivi karibun ya Simba na Mwadui, Mwamuzi msaidizi akinyoosha kibendera cha offside wakati mshambuliaji wa Mwadui katoka katika msitu wa mabeki wa Simba na kumlamba chenga kipa wa simba ili onyesha jinsi fedha inavyo udhalilisha mpira wetu.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
mtateseka sana mwaka huu kama Kabwili angekuwa kipa mzuri kama anayojisifu yanga wasingesajili makipa wazuri wawili na yeye kuwa kipa wa tatu
Kwanini hakuripoti hilo tukio sasa hivi anatafuta kick kwa sababu hakuna mtu anayemzungumzia tena
 
Hao takukuru washapelekewa kesi kama hizi za kuwahusu mikia na rushwa michezoni na nsa job na shaban kado hadi ushahidi alikua nao wa pesa alizopelekewa na ulimboka mwakingwe ili aifungishe mtibwa,tena hii kesi ilifika hadi mahakamani morogoro lkn hata ilivyoisha isha,takukuru kwenye kana hizi uwaoni
Kama tunataka kuondoa rushwa michezoni hapa ndio TAKUKURU wanapaswa kuanzia. Kabwili ni mtu mzima na kama kweli ametamka maneno hayo akiwa hajalewa au anatania ni wakati sasa wa TAKUKURU kufuatilia kwa Kabwili ili awape majina ya watu waliotaka kumhonga na wao wafanye uchunguzi wao kisha watuhumiwa wafikishwe mahakamani iwapo ushahidi utaptikana. Bila kuondoa vitendo vya rushwa michezoni hatutaweza kupiga hatua kuelekea kwenye mafanikio.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom