Rakesh wa KULEANA – HAKI ELIMU na sasa TWAWEZA ni KIVULI cha nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rakesh wa KULEANA – HAKI ELIMU na sasa TWAWEZA ni KIVULI cha nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GHOST RYDER, Jul 26, 2011.

 1. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Rakesh wa KULEANA – HAKI ELIMU na sasa TWAWEZA ni KIVULI cha nani?

  Kwa siku Miezi kadhaa sasa nimejikita katika kusaka dondoo Muhimu sana zinazowahusu Ndugu Rakesh Rajani na Mustafa Kudrat waanzilishi wa Kituo cha Kulelea watoto Yatima cha KULEANA mwaka 1992 kilichopo huko Mwanza.

  Safari ya Rakesh Rajan ilianzia huko akiwa na lengo mahususi na ambalo lilionekana muhimu sana na la kipekee kwa Taifa kutokana na kushamiri kwa ongezeko la watoto wa Mitaani ambao baadye waliamua kulibadili jina hili kwa madai kuwa Mtaa hauwezi kuzaa Mtoto na hivyo kupewa jina rasmi watoto wanaishi katika mazingira magumu kama vile ilivyobadilishwa kwa Albino na kuwa wenye ulemavu wa Ngozi.

  Katika miaka hiyo ya 1992 – 1999 kuleana walifanya kazi kubwa na kuwa kituo ambacho kwa kiwango kikubwa kilisaidia kupunguza tatizo la watoto wanaosishi katika mazingira magumu na kuvutia watanzania wengine kuanzisha vituo kama hicho katika maeneo kwingineko Nchini ambapo tatizo hili lilinukuliwa kama moja ya matatizo ya msingi.

  Nimetathmini mafanikio ya Miradi aliyoianzisha Rakesh Rajani na Athari kwa umma wa Watanzania nimegundua Athari ni nyingi kuliko faida za miradi hii na hivyo nasukumwa zaidi kuandika katika upande huo nikiamini kama yupo mdau anayeweza kulinganisha mazuri hayo achukue jukumu ili kwa pamoja tusaidiane kubaini kama malengo ya Rajani na wafuasi wake ni kwa masilahi ya Taifa au Ni kivuli cha Mr. NO BODY??

  Mara zote ambapo amekuwa akiianzisha miradi hii na kuuhama amekuwa akifanikiwa pia kuwahamisha wafadhili wote ambao wamekuwa wakihisani miradi hii na kuhamia katika mradi huo mpya aliounzisha, kwa sasa kuleana ipo ICU, Huku haki elimu ipo maternity ward inasubiri mimba ya kifo iliyoachwa hapo na Rajani wajifungue na wao wakaungane na KULEANA kule ICU.


  Anguko la KULEANA

  Mwaka 1999 Rakesh Rajani kwa kushirikiana na Mustafa Kudrat walitoa kijitabu kilichojulikana kwa jina la THE STATE OF EDUCATION IN TANZANIA – Crisis and Opportunities. Moja ya eneo lilokaziwa zaidi katika Kitabu hiki lilikuwa to abolish corporal punishment in schools (Kukomesha adhabu za ukatili/viboko kwa wanafunzi)

  Katika Hoja hii ambayo kimsingi ndio ilikuwa hatima ya Rajani KULEANA kama ilivyo kule HAKI ELIMU amekuwa na kawaida ya kuwasha moto na akishafanikiwa anahama mradi na kukimbilia katika Mradi mwingine.

  Hakika katika uwanja wa siasa za Tanzania amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kama malengo yake ndio haya ambayo tunayashuhudia leo hii. Tuanze kuangalia hadidu za rejea katika mpango huu wa kumaliza Adabu za viboko mashuleni.
  Matatizo ya Adhabu za Viboko.

  Utafiti wa Rajani na Timu yake walijiridhisha kuwa:
  • Adhabu ya viboko imejikita kwenye kuadhibu kuliko kumuelekeza anayeadhibiwa.
  • Inafundisha kuwa Ukatili ni jambo la kawaida katika Jamii.
  • Wakubwa kuwapiga wadogo ni kielelezo kuwa wenye Mamlaka wanaruhusiwa kuwakandamiza walio chini yao.
  • Na kwamba adhabu za viboko zinasababisha uoga na hasira kuliko kujenga Nidhamu.
  • Inavunja mahusiano muhimu sana ya Kijamii kati ya mtoa adhabu na muadhibiwa.
  Mbadala baada ya kuondosha Adhabu za Viboko:

  • Watoto wapewe maonyo ya maandishi
  • Pia endapo watakosea jambo fulani kuliko kuadhibiwa wapewe nafasi ya kulirudia jambo hilo.
  • Wapewe makaripio ya mdomo
  • Wapewe nafasi ya kufanya shughuli za manufaa kama adhabu, mfano kusafisha darasa au kupalilia bustani ya shule.
  Matokeo ya Utafiti wa G.R
  • Baada ya KULEANA ya Rajani kufanikisha Kam[peni hii ambayo pia ilipata Baraka za Bunge baada ya kulob kwa kutumia mashirika ya utetezi wa Hai za Mtoto kitaifa na Kimataifa, Hoja yao ya msingi ikapenya, matokeo yake sasa:
  • Tazama ongezeko la Mimba kwa wanafunzi wa Shule za Msingi, sitaki kusema sekondari wanavyoziporomoa kila kukicha maana wao ni mazao ya awali ya azimio hili.
  • Leo ni jambo la kawaida kwa mwanafunzi kufanya mapenzi na Mwalimu baada ya kuondoa ombwe la kinidhamu lililokuwepo kati ya Kada hizi mbili.
  • Maadili na Nidhamu kwa wanafunzi imeporomoka kupita maelezo ya kawaida.
  • Mbaya zaidi kutoakana na kushuka kwa Nidhamu na Maadili kiwango cha Elimu kimepromoka kwa karibu asilimia 60%
  • Knowledge is no longer a power


  Safari ya Haki Elimu

  Baada ya kufanikiwa katika hilo na kuacha maumivu haya makubwa kwa Taifa Rakesh Rajani na Timu yake wakatimukia HAKI ELIMU baada ya kwenda kujipumzisha marekani kwa Likizo ya Masomo ya Juu.
  Haki Elimu wakaibuka na wito '' TAFAKARI, CHUKUA HATUA''

  Mradi huu mara kadhaa ulitoa takwimu nyingi ambazo ziliibana serikali kutokana na uozo wake katika kushughulikia Elimu licha ya kuwa wakati mwingine walizidisha chumvi na kusababisha baadhi ya matangazo yao kupitia Kamisheni ya Utangazaji Nchini kusimamishwa hadi yatakapofanyiwa marekebisho ili kuendana na Uhalisia wa mabo na si ushabiki na kuchochea uongo.

  Huu ndio ulikuwa mwisho wa Rajani Haki Elimu na kuamua kuanzisha Mradi mwingine wa TWAWEZA.


  Udhaifu wa Haki Elimu

  Fedha nyingi sana ilitumiak kutengeneza machapisho na kugharamia matangazo katika vyombo vya ahabari endapo kama ingeelekezwa katika kusaidia jamii moja kwa moja leo tungekuwa walau kwa kiwango fulani mikoa miwili mitatu ya mradi wananafuu katika matatizo haya ambayo Haki Elimu waliamua kutuaminisha kuwa ni Jukumu la Serikali tu na wananchi tunapaswa kulishwa kwa ncha ya Kijiko.

  Kenya wamefanikiwa sana kwa kuchangia katika Elimu kutokana na Nguvu za WANANCHI, Nilidhani juhudi za Haki Elimu zingelenga kuwaelekeza watanzania kuhusika moja kwa moja katika kuchangia na kushiriki shuguli za maendeleo maana tumekuwa maarufu wa kuchangia Harusi kuliko kutujaza ujinga kuwa kila kitu itafanya serikali.

  Wakatulazimisha kuamini kuwa serikali lazima itekeleze Majukumu hayo na sisi kazi yetu ni kutafakari na kuchukua hatua za kuibana serikali, hizi ni mbinu chafu zilizofanikiwa kuteka mawazo ya Watanzania.


  Twaweza

  Walau sasa anaonyesha kuwa social accountability ni muhimu katika chachu ya maendelo, licha ya kuwa kiitiko cha twaweza WANANCHI TWAWEZA NI SISI, Kina reflection kubwa na sina shaka kimebeba dhamira nyingine mbovu kama ilivyokuwa HAKI Elimu, Ninaendelea kuutathimini na mradi huu maana sijui akitoka hapa yeye na Timu yake wanaelekea wapi tena.


  My Take:


  • Hivi kweli huyu Jamaa ametathimini madhara aliyotuachia kufuatia Kampeni za KULEANA na HAKI ELIMU?
  • Yupo kwa masilahi ya Taifa au ni Kivuli cha nani hiki kinachowatesa Watanzania kwa sasa?
  • Usalama wa Taifa wanazitambua mbinu chafu za miradi kama Hii?
  • Tutaendelea kukumbatia miradi ya Aina hii mpaka lini?


  LATEST INPUT: 26th February 2013

  Wakati naandika Uzi huu wachache sana walielewa, hata leo tunapoendelea kupiga dandana za matokeo ya kidato cha nne ni bahati mbaya sana hakuna anayetaka kwenda kwenye botom course zaidi ya kushughulika na matokeo.

  Matokeo haya ya wadogo zetu leo hayajaja kama mvua za Vuli ambazo hazina dalili wala wakati maalumu, hapa tunamkuta mdau mwingine aliyekiingiza kizazi cha watanzania katika umagharibi ambao hatukuwa na uwezo nao na matokeo yake leo ZOMBI wamechorwa kwenye karatasi za mitihani.

  Tuendelee kujadili, pengine hizi Tume viini macho zikaja na majibu ya kina, Ila ukweli huwa mchungu sana daima.


  LATEST INPUT 08 April 2013

  Sasa Serikali inajadili kurudisha Adhabu za Viboko Mashuleni: Taratibu yaliyofichika tutayaona na Uzi huu utakamilika.  ADIOS
   
 2. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Yaani kuondoa adhabu ya viboko kwa watoto Mashuleni unaona kama iliacha maumivu makubwa kwa jamii ya kitanzania??? Umeandika mengi, ila nakosa hamu ya kuendelea baada ya kuona hiyo conclusion yako!! Uuuuhm, pole ndugu. Yaani unahusisha wingi wa mimba na kuondolewa adhabu ya viboko mashuleni?? Umefanya utafiti?? Rakesh huwa anafanya utafiti unaojisimamia wenyewe; lakini hili la kwako mtoa mada limeniacha mdomo wazi!!!
   
 3. T

  Technology JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 733
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  too much energy and time! Did you ever work under Rajani?
   
 4. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nakumbuka wakati niko primary mwalimu alikuwa anaongoza kwa kuchapa bakora, bahati mbaya alikuwa pia anakunywa gongo mitaani kwetu si unajua tena bush country,
  akishalewa akiwa njiani kurudi nyumbani tunalipiza kisasi kwa mawe, marungu hadi kumtoa ngeo.
  llikuwa swala la nani kwenye himaya ya nani.
   
 5. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hupaswi kubaki Mdomo wazi unapaswa kutafakari Hoja na soma maliza thread. Tatizo letu ni kupenda kusoma yanayotufurahisha. Kuna tatizo hapa la msingi.

  Ongezeko la Mimba kama eneo moja ulilolitaja linatokana na utovu wa Nidhamu na kushuka kwa Maadili. Katika maandiko matakatifu Biblia na Kuran tumeelekezwa kutoa mapigo kidogo yasiyodhuru kwa mtoto kwa lengo la kumrudi kimaadili.

  Kama tumeiga umagaharibi ambapo kwao wao abortion ni kama kwenda kupima maralia uansemaje hapa hakuna tatizo. Huwezi kuawa serious soma tena thread hii vema na wewe tafiti kwa muda wako
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Si bora hata Rakesh kaanzisha hizo initiatives, wewe umeendeleza vipi hapo ulipoona kashindwa?

  Na una ushahidi gani kuhusu idea nzima ya "kivuli"? Au ndiyo habari za kupakana matope?

  I was watching "Darwin's Nightmare" for yet another time, nilivyoona zile scenes za hawa watoto Mwanza nikamkumbuka sana Rakesh. If the only thing Rakesh had to his name was bringing this issue to light and helping these children he would have had an assured place in the virtuous Tanzanian soldiers, but he did much more.

  And this is the thanks he gets?

  I see nothing to impeach him from the above info, labda sema kingine.
   
 7. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Patriotism
   
 8. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Nasukumwa na Athari ambazo ni nyingi kuliko faida, na nimemaliza kwa hitimisho la swali ambalo halinifungi mawazo yangu. Takari zetu kwa pamoja tutadrwa suluhusho wala usinihukumu kwa mtazamo na tafsiri yangu kwa hatari hii ninayoina kwa Taifa
   
 9. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Yaan anakubaliana na wewe Mkuu hata hukom katika madrasa kuna wataoto wanagwaya kwenda kwa kuhofia bakora ambazo hazina malengo na unapiga mtoto kama unaua Nyoka, Hiyo hapana hata mie siungi mkono
   
 10. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Ni mjasiriamali anayetumia njia za kisasa zaidi.
   
 11. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Sasa yeye vision yake ndiyo hiyo, wewe kama una vision nyingine m-prove wrong kwa vitendo.

  Rakesh si mbunge au Waziri kusema anatumia public funds kihivyo, ana represent NGO kwa kutumia ubunifu wake. Huwezi kum knock kwamba analeta athari zaidi ya faida bila ya wewe kuamka na kufanya tuone tofauti. Especially katika mambo haya ambayo kupimika kwake si rahisi.

  Katika nchi ambayo imejaa kina Jairo na Chenge wa "vijisenti", nikitumia principle yako mwenyewe ya "proportionate effort for proportionate results" na kuepuka kuleta "athari nyingi kuliko faida" naona ni bora tuelekeze nguvu kuwamulika na kuwashutumu watu kama kina Jairo na Chenge, ambao uchafu wao si mgumu kuuona, kuliko kuanza ku split hairs kuhusu mtu kama Rakesh ambaye kwangu mimi namuona kama mtu mwenye uchungu na nchi na sijaona ubaya wake bado.
   
 12. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Halafu wewe bado una imani na usalama wa taifa inayoendeshwa na huyo pimp wa Kikwete?

  Usalama wa taifa inaongozwa na huyu pimp ambaye kazi yake ilikuwa kumtafutia Kikwete mabibi akija London?

  Hivi sisi tuna "Usalama wa Taifa" bado? Usalama wa taifa au usalama wa wakubwa?

  Au ndiyo washaanzisha vita kwa kila mtu anayewabana korodani?
   
 13. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  At least tunaanza kuelewana Mkuu, Sina chuki na Rakesh Rajan wala sijawahi kufanya naye kazi naomba haya yaeleweke wazi lakini nimekuwa nikisoma machapisho na makala nyingi ambazo zinahusu Taasisi yake nikavutika kufuatilia chimbuko lake.

  Na haya ndio nimeyabaini katika kutathmini Kampeni zke na Athari zake, am stand to be corrected with justifiable facts maana Hali ni mbaya kufuatia sumu inayoachwa na miradi ya Rajan

  Kuleana nimekwambia ipo ICU

  Kuna Kijana anaitwa Joanathan ambaye katika kitabu hicho Rakesh anamtaja kama rasilimali ambazo taifa limezitelekeza kutoaka na kipaji cha uchoraji alichonacho kijana huyo.

  Kijana huyu ambaye Rakesh anamtaja hata kuwa seriakli imewasahau hata yeye kamsahau licha ya mafanikio aliyoyapata sasa. Jonathan sasa ni mwehu wa kuokaota katika mapipa baada ya kutumia sasa dawa za kulevya.

  Jonathan huyu ni yule aliyetumiwa na Herbet Sauper katika documentary ya Darwin Nightmare iliyozua kizaa cha aina ya kipekee Nchini. Na vijana waliohusika ni wale kutoak KULEANA ambao Rakesh aliwaacha baada ya Kuitosa kuleana.

  Wengi wao leo ni wakora sugu huko Mwanza

  Hebu tusaidiane mawazo hapa huyu ni KIVULI au awatanzania tumeshindwa kutambua hasa dhana yake ni nini?
   
 14. Junior. Cux

  Junior. Cux JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 5,305
  Likes Received: 1,226
  Trophy Points: 280
  iki ni kitu muhimu sana hasa kwa mustakabari wa taifa letu lakini nachelea kuchangia mada hii mpka ntakapojua interest yako mtoa mada kwenye tasnia ya elimu.. upo kama nani kwnye elimu ya tanzania.??
   
 15. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Nimesikitika sana kusoma hii post yako.

  Nilisema hapo juu kwamba ni juzi tu nilikuwa naangalia tena "Darwin's Nightmare". Nimemuona huyo kijana.

  Nilikuwa namwambia mtu, huyu kijana ana akili sana. Kwanza kakulia mazingira hafifu sana, halafu anajua kiingereza vizuri sana, anajieleza vizuri, anafuatilia current affairs, anaweza ku relate mambo - alikuwa anaeleza mambo kwa ufasaha uliozidi sana umri wake-, as if that was not enough, ana kipaji sana cha uchoraji. Nilikuwa namwambia mtu ningeweza kumsaidia huyu kijana ningemsaidia.

  Halafu nikajiuliza, hii filamu ina miaka kadhaa, sijui huyu yukoje sasa.

  Kusikia mwehu sasa inanihuzunisha sana.

  Lakini huwezi kumlaumu Rakesh, mimi naweza kusema Rakesh anaonekana kama "lone warrior" katika vita inayohitaji wengi wamuunge mkono, na pengine ndiyo maana anashindwa.

  Ndiyo maana nikakuuliza, wewe umesaidiaje kuhakikisha vision yako inafanikiwa na kuendeleza elimu na ustawi wa jamii Tanzania?
   
 16. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hii ni doasari nyingine kwa Taifa hata juzi umesikia wadau wakihoji hadi wabunge wanapata barua ya Jairo na Kuphotocoy Rais hauju wala PM kwa kuwa usalama wa Taifa hawakufanya vema kazi yao.

  Na sie tunaendelea kuhoji kwani tunajua hii ni dhamana yao na hawajakiri kushindwa watuambie wapo wapi na haya yanakuwaje kwa masilahi ya Umma
   
 17. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Bora uendelee kusikitika
  kama Hoja zimekwisha
   
 18. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #18
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mdadisi wa Mambo na Critical analyst
   
 19. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #19
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  I like this one.
   
 20. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #20
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  No comments
   
Loading...