Raisi wetu akutana na mfalme wa Ashanti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Raisi wetu akutana na mfalme wa Ashanti

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngambo Ngali, Jul 11, 2011.

 1. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  [h=3]MFALME Otumfuo Osei Tutu wa Pili wa Ufalme wa Ashanti[/h]
  [​IMG]
  Mfalme wa Ashanti akiingia ikulu kwa staili ya aina yake, huku akikaribishwa na Rais Kikwete.

  *TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI*

  MFALME Otumfuo Osei Tutu wa Pili wa Ufalme wa Ashanti nchini amewashauri
  baadhi ya Waafrika kuacha kuitumia demokrasia vibaya kwa kutowaheshimu
  viongozi wa nchi na Serikali za Bara hilo ambao amesema kuwa anaamini fika
  kuwa wamedhamiria kuimarisha demokrasia katika Bara hilo.

  Mfalme huyo pia amewaambia Waafrika kuwa hali ya baadaye ya Bara la Afrika
  ni nzuri lakini mafanikio yote ya Afrika yatategemea jinsi Waafrika wenyeji
  wanavyoendesha nchi zao na wala siyo kutokana na sera za mashirika ya fedha
  duniani.

  Aidha Mfalme huyo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
  Jakaya Mrisho Kikwete wamekubaliana kuwa Afrika ndilo Bara ambalo dunia
  nzima itakuwa inalikimbia katika siku zijazo.


  Mfalme Otumfuo Osei Tutu wa Pili na Rais Kikwete amekutana leo, Jumapili,
  Julai 10, 2011, Ikulu, Dar es Salaam, mara baada ya Mfalme huyo kuwa
  amewasili nchini kuanza ziara ya siku 10 kwa mwaliko wa Rais Mstaafu,
  Mheshimiwa Benjamin William Mkapa.

  Mara baada ya mazungumzo yao, viongozi hao wawili wamekula chakula cha
  mchana pamoja na Rais Mkapa na wawakilishi wachache wa familia zilizokuwa za
  kichifu nchini.

  Mfalme amemwambia Rais Kikwete kuwa ni vizuri kuona maendeleo makubwa ya
  demokrasia katika Afrika na ari ya viongozi wa sasa kuimarisha demokrasia
  hiyo, lakini ni jambo la kusikitisha kuwa baadhi ya Waafrika sasa wameanza
  kuitumia vibaya demokrasia kwa kutoheshimu, na wakati mwingine, kudharau
  viongozi wa Afrika.

  “Kiongozi wa nchi huchaguliwa na wananchi wote. Hivyo, ni muhimu kuwa baada
  ya uchaguzi kufanyika na kumalizika, wananchi wote, waliompigia kura na wale
  ambao hawakumpigia kura kuonyesha heshima inayostahili kwake kwa sababu yeye
  sasa ndiye kiongozi wa nchi,“ amesema Mfalme.

  Katika mazungumzo yao, Mfalme na Rais kikwete pia wamekubaliana kuwa miaka
  ijayo dunia itakuwa inalitegemea Bara la Afrika katika kudumisha mafanikio
  ya kiuchumi duniani.


  “Hali ya baadaye ya uchumi wa dunia itakuwa mikononi mwa Afrika. Changamoto
  ya Bara letu, kwa hiyo, ni jinsi gani ya kuweka akili yetu pamoja ili kuweza
  kubuni sera nzuri zinakazoendeleza matunda ya kiuchumi na kijamii ya Bara
  letu na zitakazoleta maisha bora kwa wananchi wetu. Mpira uko uwanjani mwetu
  lakini hali ya baadaye ya uchumi wa dunia ni katika Afrika,” amesema Rais
  Kikwete.

  Mfalme amekubaliana na Rais akisema: “Afrika ndilo Bara linaloangaliwa na
  dunia nzima kwa sasa na katika miaka ijayo. Lakini mafanikio ya Afrika yako
  mikononi mwa sisi Waafrika wenyewe na wala kwenye mikono ya IFM (Shirika la
  Fedha Duniani) ama Benki ya Dunia.”

  Viongozi hao wawili pia wamekubaliana kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania
  na Ghana, uhusiano ambao ulijengwa katika miaka ya mwanzo ya uhuru wa nchi
  hiyo kupitia viongozi wa mwanzo wa nchi hizo mbili, Mwalimu Julius Nyerere
  na Osagyefo Kwame Nkurumah ambao wote ni marehemu sasa. Nchi ya Ghana
  ilikuwa nchi ya kwanza Kusini mwa Jangwa la Sahara kupata uhuru, kutoka
  ukoloni wa Kiingereza, mwaka 1957.

  “Nimefurahi sana kufika Tanzania. Nimesikia mambo mengi mazuri kuhusu nchi
  hii tokea wakati wa viongozi wetu Julius Nyerere na Kwame Nkurumah. Naamini
  kuwa ziara yangu itaanzisha jitihada kubwa zaidi za kuimarisha uhusiano kati
  ya nchi zetu mbili. Nimefurahi sana kufika Tanzania,” amesema Mfalme Otumfuo
  Osei Tutu wa Pili.

  Source:lukwangule.blogspot.com

  My take:

  Je ilikuwa lazima kwa watu hawa kukutana na kupata full coverage, mbona wasaidizi wa raisi wanamuoverwork na shughuli na ratiba ambazo hazina tija kwa wananchi anaowangoza?


  Wamekubaliana vitu vya msingi sana ambavyo vinaonyesha ukoloni mpya ambao upo afrika je wamechukua hatua gani kuondokana nao? Kukubaliana tukama inavyoonekana kwenye red haitoshoi, wanahitajika wachukue hatua zaidi kama walivyofanya akina mkwawa, milambo, nyerere, nkurumah, Osei Tutu wa enzi za Anglo Ashanti wars walilivyowafukuza wazungu.
   
 2. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  Wamekubaliana? chief ainunue Zanzibar na pwani yote ya Africa Mashariki
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hii tabia ya viongozi wa Africa kujidai 'victims' nadhani umefika muda sasa iogopwe kama ukoma. Leo utasikia wanalalamika kuhusu ukoloni, kesho IMF, kesho kutwa World Bank! Hivi nani kasababisha nchi kuwa kwenye giza? Ni mataifa ya nje? nani kaandika CHEQUE ya Rada? Malkia wa Uingereza? au nani kaanda mikataba ya madini? - IMF?

  Kwa nini hatusikii Malaysia au Singapore wakilalamika kuhusu ukoloni? Ni lini viongozi wa Afrika wataacha kutuhadaa sisi wananchi kuwa hali mbaya tuliyo nayo inasabibishwa na mataifa makubwa? Mbona wao viongozi hawana hali mbaya?
   
Loading...