Raisi Samia angalia tena sifa za Juma Aweso, Kilichopo Morogoro ni aibu

Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
2,044
2,000
Ukweli ni kuwa watu wanaweza kuishi bila uwepo wa vitu vingi tu, lakini sio maji.
Watu wanaweza kuishi bila umeme, bila barabara lakini hawawezi kuishi bila maji.
Mkoa wa morogoro ni moja ya mikoa yenye vyanzo vingi vya maji lakini huwezi amini kuwa maji ni shida kubwa sana.
Watu wananunua maji kutoka kwa wasambazaji wanaotumia zile water Bowser. Suala la kutokuwepo maji limehalalishwa kabisa mkoa wa morogoro.
Bado najiuliza sifa zote ulizompa waziri aweso ina maana hii shida iliyopo morogoro hamuijui?
Kuna mkoa nilitembelea kiukweli kwenye suala la maji wapo vizuri sana, maji yanatoka masaa 24 tena kwa kasi kubwa sana. Hawaijui kabisa shida ya maji. Inawezekana imesababishwa na kukamilika kwa ule mradi wa ziwa Victoria.
Wananchi wanachotaka hizi huduma ziwe za uhakika na hapo malalamiko yatapungua sana, Ila ikiwa maji tu ni tatizo basi tegemea watu kila Mara kulalamika.
Mama Samia naomba rejea tena sifa zako kwa aweso, kwa maana yaliyopo morogoro ni aibu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom