Raisi Mtarajiwa Dr. Slaa kuwatendea ubinadamu akina CCM-damu kaitka uongozi wake..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Raisi Mtarajiwa Dr. Slaa kuwatendea ubinadamu akina CCM-damu kaitka uongozi wake.....

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Oct 17, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  Kwa sababu Raisi mtarajiwa Dr. Slaa ni mcha Mungu sana kamwe hatawabagua au kuwanyanyapaa wanachama wa CCM wajiitao "CCM damu, damu" Katika kulijenga upya taifa hilli, Raisi mtarajiwa atatumia nafasi hii kuwapa mafunzo ya vitendo makada wa CCM ya jinsi gani kuiendesha nchi bila ya kuwagawa wananchi kwenye makundi ya udini, kiuchumi na kiukabila. Nyenzo ambazo zimeisaidia CCM kutesa kwa miaka takribani 49 hivi...........

  Utawala mpya wa Dr. Slaa utaheshimu haki za binadamu na kuweka mbele utu wa mtanzania ambao CCM wamekuwa wakiuongelea kwenye majukwaa tu lakini siyo kwa vitendo.

  Jamaa zetu wa CCM-damu hawatabaguliwa kwenye ajira na utoaji wa zabuni serikalini kwani vigezo vya tija tu ndivyo vitakavyozingatiwa. Hapatakuwa na suala la kujuana tena katika kugawa rasilimali za taifa.

  Hivyo CCM-damu waondoe hofu na waanze kujiandaa kukubali mabadiliko haya ya kidemokrasia ya kweli ambayo sasa hayakwepeki................
   
Loading...