Raisi Mtarajiwa Dr. Slaa apania kuteua Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Raisi Mtarajiwa Dr. Slaa apania kuteua Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Rutashubanyuma, Oct 21, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Moja ya mifupa ambayo imeishinda CCM kuitafuna ni kumteua mwanamke kuwa Waziri Mkuu. Mfupa huo kaka yetu Dr. Slaa ambaye tunatarajia kumvika joho la Urais wetu hivi karibuni nimepata tetesi ameamua kuhakikisha anautafuna huo mfupa kwa kumteua mwanamke wa kwanza katika historia yetu ya nchi yetu kuwa Waziri Mkuu.

  Kwenye hili, CCM wao wamekuwa magwiji wa ngebe na porojo tu na hakuna utekelezaji wa vitendo. Sasa mchapakazi Dr. Slaa atakapotinga Ikulu atafuta hii aibu kwenye taifa letu la kutokuwa na mwanamke kwenye ngazi za juu za uongozi wa taifa hili.

  Mimi ninapendekeza ayafikirie majina haya matatu kwa sababu nitakazozitaja hapo baadaye kidogo:-

  1) Prof. Anna Tibaijuka........................CCM

  2) Ms. Anna Makinda............................CCM

  3) Dr. Asha Rose Migiro........................CCM

  Sababu zangu za kuwapendekeza akina mama hawa kutoka CCM ni:-

  Kwanza, kupunguza misuguano iliyojionyesha kwenye chaguzi hii kati ya CCM na Chadema,

  Pili, ni matarajio yangu kuwa CCM bado itakuwa na wabunge wengi zaidi Bungeni na hivyo kutowashirikisha kabisa italeta ugumu katika kupitisha miswada ya serikali bungeni,

  Tatu, ni mahitaji ya kikatiba ya kuwa kwa vile kama matarajio yangu yatakwenda saawia basi CCM ndiyo itakayoongoza kwa wabunge wengi Bungeni na hivyo ni haki yao kutoa Waziri Mkuu na kuteua mwanamke kuwa Waziri Mkuu kutoka CCM Dr. Slaa atakuwa kawafunga CCM bao la kisigino kabisa.......chuki zitoke wapi baada ya kuwaenzi hivyo?

  Nne, akina mama ni viongozi wazuri na huona mbali sana na kwenye kipindi hiki cha mpito kutoka utawala wa kiimla kwenda kwenye utawala wa kidemokrasia busara zao tutazihitaji sana. Wanawake wana subira na ni wa vumilivu na wengi wao siyo waroho wa madaraka au kujiingiza kwenye aibu za kusaka mali na mara nyingi wapo tayari kujinyima ili kulinda uhai wa jamii.

  Hatutagemea kati ya hawa niliowapendekeza kuhusishwa na tuhuma za wizi na ubadhirifu wa mali ya umma kama baadhi ya wanaume ilivyowatokea siku za karibuni...

  Ni vyema nanyi wanajamvi mkatumia nafasi hii kuiangalia nafasi hii ya uwaziri Mkuu imwangukie nani yule.....sote tunajua hakuna kama mama.........au vipi?........
   
 2. F

  Fikra Pevu Senior Member

  #2
  Oct 21, 2010
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hii ni tetesi au matamanio yako
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Oct 21, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Waziri mkuu ni lazima atoke chama tawala ili Chadema wapate usimamizi mzuri wa sera zao...
   
 4. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Not Anna Makinda Please. I hope you remember the way she tried to suffocate opposition in the Prliament. Also find out the appartments under her name does it march with her income. She is a CCM fanatic not a politician.
   
 5. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hii hoja ilianzia huku:

  <LI class=g>NCCR yaahidi uhuru vyombo vya habari

  - [ Translate this page ] 30 Ago 2010 ... *Rais wao kuteua waziri mkuu mwanamke. Na Godfrida Jola. CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimezindua Ilani yake ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ...
  www.majira.co.tz/index.php?option=com...view... - Cached
   
 6. senator

  senator JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Kwanza silahaa hashindi uchaguzi huu..pili mama anna mpaka pinda atolewe na jk ambayo itakuwa ni moja ya tukio zito nchini ,...
  naona ni bora mama tiba akawa kwenye nafasi ya membe mana anaupeo mkubwa kwenye tasnia hiyo
   
Loading...