Raisi, Mawaziri, Wabunge na Madiwani wadanganya umma wa Tanzania! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Raisi, Mawaziri, Wabunge na Madiwani wadanganya umma wa Tanzania!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MsandoAlberto, Feb 5, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  WanaJF,

  Kila kiongozi anatakiwa ajaze form maalumu ya kutaja mali zake kwa mujibu wa sheria ya Maadili ya Umma.

  Taarifa zilizothibitishwa ni kwamba mara zote viongozi hao wanapojaza form hizo hakuna hata mmoja anayejaza kwamba anadaiwa na Bodi ya Mikopo!!

  Kiongozi anatakiwa ndani ya muda maalumu awe ametaja mali zake na madeni pamoja na kutoa akaunti namba zake za benki! Lakini ni dhahiri kwamba viongozi wamekuwa wakijaza uongo form hizo na tume ya maadili haifuatilii kwa karibu kuthibitisha taarifa zinazotolewa na viongozi kuhusu mali zao!

  Kutokana na hali hiyo ndio sababu hata mikopo iliyotolewa kisheria kwa viongozi mbalimbali kwa ajili ya elimu ya juu hairudishwi! Viongozi hawahesabu kama hilo ni deni ambalo linastahili kulipwa!!

  Huu ni udanganyifu kama sio uzembe wa viongozi!

  Viongozi wote walioshindwa kutaja deni hilo wawajibike kwa kuwaomba radhi wananchi na wajaze upya form za maadili na kuikabidhi tume!

  Nawasilisha!
   
 2. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Well said mkuu,

  Kwa ufupi tu niseme kwamba, tunahitaji katiba mpya, uongozi mpya, viongozi wapya na mtazamo mpya ili kurudisha maadili ya viongozi.

  Tukiwa na katiba mpya na viongozi wapya, katiba itaiwezesha ama kuipa mamlaka tume ya maadili iweze kuwashughulikia wale wote watakaoshindwa kujaza fomu na hata wale watakaojaza fomu lakini hawakutoa taarifa sahihi ama kuficha baadhi ya taarifa.Na viongozi wapya watahakikisha kwamba maadili kwa viongozi yanazingatiwa kwa kuanza na kiongozi mkuu mwenyewe.

  Chini ya katiba hii hakuna lolote linaloweza kufanyika kwakuwa simuoni kiongozi mwenye maadili anayeweza kusimama na kudemand utekelezaji wa maadili ya uongozi wa umma.
   
 3. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mwita, uko sahihi sana. Bado nchini kwetu mtu anaweza kufanya jambo lolote kama kiongozi na asiwe held responsible. Kwa wenzetu kauli pekee inatosha kumsababisha mtu ajiuzulu!
   
Loading...