raisi magufuli wafanyakazi tumekukosea nini? -2

CK Allan

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
2,781
6,065
niliandika humu kipindi kilichopita nikiwa na uzi wenye kichwa kama hiki hapa Rais Magufuli wafanyakazi tumekukosea nini?
niwe mkweli kuwa sikuona dalili za uzi ule kumfikia mheshimiwa raisi maana hali ilizidi kuwa ngumu kwa wafanyakazi..

Raisi wangu mimi ni mtumishi wa uma na sina namna nyingine ya kueleza hisia zangu zaidi ya njia hii, mheshimiwa raisi,
1. suala la kukaa kimya kuhusu stahiki za watumishi ikiwemo nyongeza za mishahara, uhamisho, kupanda madaraja n.k linanipa ukakasi kuamini kuwa mheshimiwa kipo kitu pengine hutaki kukiweka wazi, hivi ni kosa gani sisi tumekufanyia ambalo unakataa kata kata kutusamehe?
2. Mheshimiwa Raisi, suala la uhakiki ni "kiteseo" kingine cha wazi cha kunyima haki zetu! kwa namna ninavyokujua mheshimiwa Raisi usingekubali hadi leo haki za watumishi kuendelea "kulaliwa" kwa kigezo cha uhakiki, naomba tena tusamehe baba..hebu huu uhakiki ufike mwisho!
3.mheshimiwa Raisi, wenzetu wa Zanzibar wanaongezewa 100% hebu tuhurumie sisi nasi, juzi ukiwa mahali fulani ulisema huwezi lipa madai yoyote mpaka hizi "hewa" ziishe... mimi nimehakikiwa mara nne mkuu, mpaka picha nilipigwa, hizi hewa zimebakia wapi?
4. mimi sina uhakika ila nilisikia eti mheshimiwa Raisi ulikuwa mwalimu! naomba jaribu kuvaa viatu vya walimu walau kwa nusu saa tu uone jinsi hali ilivyo na vuta picha ingekuwa ni wewe!! ni kosa gani hili lisilosamehewa? juzi umeongeza makato ya wanufaika wa mkopo kwa 15% hata kile kidogo tulichokuwa tukipata umeamua kukichukua! kama lengo ni kutuonyoosha nadhani sasa kichwa kinataka kukutana na magoti..tuhurumie
5.mwisho kwa leo, (maana nitakuja na part 3) naomba ukiwa katika hizi ziara zako mbali na kuhamia dodoma,n.k hebu sema kitu kuhusu sisi wafanyakazi na nina imani nitasikia ukisema kuwa umetusamehe, kama kipo kitu na Mungu atakubariki....
 
Back
Top Bottom