Raisi Magufuli, Unalo deni kwa Mkapa na Kikwete

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
3,337
4,664
Kuna watu hawanielewi bado. Ninapoandika hivi kuna watu wanakwazika.Wengine wanafuta maandiko yangu.Tuendelee tutafika mahali tutaelewana tu.Mimi kwa Ubatizo wangu ni Nabii,ni Kuhani na ni Mfalme. Sijipendekezi kwa Magufuli na wala haijawahi kuwa ndoto yangu kujikweza. Nina deni kwa jamii yangu:upendo kwa Tanzania yangu na kwa watu wa Imani yangu na kisha kwa hao wasiokuwa bado Wa Imani Katoliki.

Leo kupitia Mwinjili Matayo 18:15-20, Yesu anatupatia Falsafa na Teolojia ya kumaliza migogoro katika jamii.Anatufundisha jinsi ya kujenga upya mahusiano ya jamii inayokuwa imemomonyoka tokana na migogoro na kutoelewana kwa namna fulani. Ni kama anatufunulia jinsi yeye Kristu alivyofanya kwetu wanadamu pindi tulipomkosea Mungu, pale Bustanini,Edeni.Yesu anatung'amurisha kuwa ilibidi achukue uamuzi Wa kuja kuongea nasi uso kwa uso badala ya kubakia na Umungu wake huku akituangalia jinsi ambavyo tungedumu katika uovu wetu.

"Ndugu yako akikukosa,enenda ukamwonye wewe peke yako na yeye,akikusikia umempata ndugu". Katika simulizi hili la Matayo katika Teolojia hii ya "kuponya" mahusiano yaliyopooza na au kuvunda,Matayo anasema Yesu anatoa njia tatu: kwanza ni mazungumzo kati ya aliyekosewa(aliyekwazwa) na mkosaji.Katika hatua zote tatu aliyekosewa ndiye mtu anayepaswa kutafuta suluhu na sio mkosaji.Mungu alichukua hatua ya kujipatanisha nasi yeye mwenyewe;hakusubiria sisi tumuendee.Kwa nini? Sababu ya upendo. Mwenye upendo kila mara ana macho ya kuona uhusiano wowote unapochafuka na hivi kujinunulia "sabuni" ya kuufua uhusiano huo.

Yesu Kristu kupitia Mwinjii Matayo anasema,ikiwa mazungumzo kati ya Wawili,hayakufua dafu,basi aliyetendwa amtafute mtu mwingine ili Wawili hao pamoja na mkosaji wayazungumze. Na hatua ya tatu ikiwa mkosaji amepungukiwa bado kuelewa udhaifu wake,basi jirani ahusishwe pia.Ndio kusema jamii nzima ihusike katika kumrekebisha mhusika.Yesu anatufundisha kutumia subira katika kujipatanisha.Ni kama kwa njia hii anarejea ile busara ya kutong'oa Magugu miongoni mwa ngano hadi wakati Wa mavuno.

Njia hizi tatu zote anazotupatia Yesu ni kutaka kuturudisha kwenye chimbuko la uelewa Wa mwanadamu.Anatufundisha kuwa mwanadamu ni kiumbe complex na hivi mang'amuzi yake katika jambo lolote lile ni mchakato.Sio jambo la wakati mmoja tu. Ni kama anatuonyesha hata yeye,alitanguliza kwanza Manabii (hatua ya kwanza) kisha ndo yeye akafika pia (hatua ya pili) Na kwamba bado hata yeye hakumaliza kazi hiyo ya kuunda upya uelewa wa mwanadamu na ndiyo kisa aliliacha Kanisa kwa msaada wa Roho Mtakatifu(hatua ya tatu) limalizie kazi hiyo ya majiundo ya nafsi ya mwanadamu kumuelekea Muumba wake. Kwamba ni Kanisa leo linawajibika ku-repair mahusiano baina na miongoni mwetu wanadamu.

Msisitizo wa Wajibu huo Wa Kanisa "kuosha na kufua " mahusiano umeelezwa katika Injili hiyo hiyo ya Matayo,pale Yesu anaposema kuwa: "...Basi nawaambieni wowote mutakaowaondolea dhambi wameondolewa...na wowote mutakaowafungia dhambi wamefungiwa..."

Kanisa ni jamii pana katika Imani.Katika familia (ndoa) unafanyaje pale unapokosewa na mwenza wako ili kurejesha mahusiano? Unakimbilia Instagramu,JF au FB kumuanika mwenzio? Unafanyaje katika uchumba pale mwenzio anapoghafilika? Je, unamuanika kwenye mitandao ya kijamii eti kuomba ushauri kabla ya kuongea ninyi wawili? Jirani yako munapokwaruzana unajipatanisha naye vipi? Je,unamualikia ngoma ya mchiriku (na wamama waliochagua kusomea matusi badala ya Bailojia) ili wakamchambe Mtesi wako? Au unajialika katika kipindi cha uhondo cha Clouds na kuanza kumshambulia jirani yako?

Na kama Taifa tunapoharibu kisiasa,kiuchumi,na au kimaadili tunaunda vipi hayo mahusiano? Najua tunayo Katiba na Sheria za kutusaidia kuponya madhara yoyote yatokeayo katika nyanja mbalimbali za maisha yetu kama watanzania. Lakini,inakuwaje pale ambapo Katiba na Sheria zetu hazitoi nafasi ya kuwarekebisha wenzetu wanaokuwa wameliumiza Taifa?

Vita ya kiuchumi inayoendelea sasa chini ya "Kamanda" Magufuli imetuonyesha wazi kuna baadhi ya "makamanda na maaskari" waliomtangulia Magufuli walifanya uzembe mkubwa sana ama kwa kupotoshwa au kwa makusudi! Kuibiwa kupindukia kwa rasilimali zetu kumewabainisha watu waliozembea sana:Mkapa na Kikwete kama watu waliokuwa na kila aina ya nyenzo ya kujua lolote katika nchi hii lakini hawakuchukua hatua stahiki.

Mtu kufikia kupewa zawadi ya jiwe la Almasi lenye thamani ya dola 200,000,000 na ukachekelea ni kielelezo cha ubinafsi uliokuwa umeota sugu. Ni kana kwamba ubinafsi huo ungekuwa unaweza kujitokeza nje ya miili yao kama yafanyavyo majipu basi miili ya ya viongozi hao ingelikuwa sasa imeenea makovu na madonda kila mahali.

Raisi Magufuli, Hatuwasakami viongozii hao Wawili na hatuna nia ya kudharau ombi lako la kuwaacha wastaafu hao wapumzike kwa Amani. Kwa ujumla wake, vita hii isingelikuwepo na au kuwa ngumu kiasi hiki(kama ambavyo inafikia hata kutuchonganisha sisi kwa sisi,kwa serikali yako kuhisiwa na jaribio la kutoa uhai wa wapinzani wako) kama watangulizi wako hao wangekuwa wamewajibika kikamilifu kama unavyofanya.

Sasa kama Injili inavyotualika leo kwa kututaka kuungamiana dhambi zetu sisi kwa sisi,kuelezana madhaifu yetu baina na miongoni mwetu, kama njia ya kutibu madonda ya Taifa letu yaliyosababishwa na watangulizi wako,nasi tunakualika ujue unalo deni kwa wakosaji hao wa watanzania.Unalo jambo la kufanya zaidi ya kuwatakieni mapumziko mema na yenye amani.

Watanzania wamepinda migongo huko mashuleni kwa kukaa chini na kwenye mawe.Watanzania wamekufa kabla ya umri wanaotakiwa kuuishi sababu ya umaskini. Wapo Watanzania pengine wameenda motoni sababu ya kuwaibia wenzao au kuwa na husuda kwa wenzao sababu ya tu umaskini uliowazunguka. Wamama walipoteza maisha wakati Wa kujifungua kisa hakukuwa na huduma bora za kujifungulia.Wako watanzania walipoteza Maisha kwa njia ya ajali za majini na nchi kavu sababu ya miundombinu mibovu.

Raisi Magufuli, kwa madhila hayo waliyoyapata watanzania huoni kama kuna jambo la ziada la kufanya kwa hao watangulizi wako? Huoni kama "repair" ya Kikatiba na Kisheria inayowawaruhusu kupumzika kwa amani haitoshi? Huoni kama watangulizi wako wanaugua nafsini mwao kwa haya madudu yanayoibuka dhidi yao kwa kila hatua ya vita yako hii katika uchumi? Hivi huoni kama Watangulizi wako wanateseka sana nafsini mwao wanapogundua jinsi walivyochangia uhai wa watanzania wenzao "kunyofoka" hata pale ambapo haikuwa lazima au haikutokea wakati muafaka?

Raisi Magufuli, mimi naiona shida mbeleni kwa watangulizi wako na familia zao. Ni bora mtu ukaugua kuharisha utatibiwa na kupona kuliko kuugua nafsi.Nafsi isononekayo muda wote huishia Kudhoofisha mwili na hata mauti huja kucheza karibu na mhusika. Haya ndio nayaona hapo mbele ikiwa hukuchukua hatua zaidi ya hii ya kuwaacha watangulizi wako wapumzike kwa Amani. Amani ni tunda la utulivu Wa kiakili na kisaikolojia.

Hebu sasa uazime Teolojia ya Injili ya Leo: watanzania waliokosewa na watangulizi wako wanatamani wazungumze na watesi wao.Watanzania wanataka kutibu majeraha ya mahusiano mabovu kati yao na hao watangulizi wako.Sote ni nchi moja.Sote ni watoto Wa Mama Tanzania.Wametukosea watanzania.Wametukosea sana.Watoke waje waungame mbele ya watanzania.Waje tusemezame.

Hebu zungumza nao na uwaambie waangalie namna ya kuwataka radhi watanzania.Haitoshi kujuta tu mioyoni mwao kimya kimya.Waje watueleze jinsi walivyoteleza katika kuwatumikia watanzania wenzao na watugawie mang'amuzi yenye mafundisho kwa ajili ya viongozi Wa vizazi vijavyo.

Raisi Magufuli,njia hii ya watangulizi wako kuja mbele ya watanzania wenzao kuridhiana pengine kwa Tume Maalumu italiacha Taifa limeshikamana.Maridhiano ndio OMO ya kuifua Tanzania baada ya kuchafuka na "kuharishiwa" namna hii.Maridhiano ndio njia ya kudumu ya watangulizi wako kuishi kwa Amani.

Unayo masikio,nadhani umenisikia na waelewe watanzania.
 
Hapa ndipo, ninaposema; Fidel Castro wa Cuba hajawahi kuwa dikteta, aliposema, "You can judge me it's not important ; the history will justify me"

Kila la Heri Tanzania. Hakika, Hii Vita Tutaishinda.
 
Hapa ndipo, ninaposema; Fidel Castro wa Cuba hajawahi kuwa dikteta, aliposema, "You can judge me it's not important m; the history will justify me"

Kila la Heri Tanzania. Hakika, Hii Vita Tutaishinda.
Cuba ni moja ya inchi maskini kabisa America kusini
 
Dah!! Nilikua nasoma nukta 2 nukta hadi hapo ulipoanza kumsifia Yohana at n m2 makin kwa taifa le2....
Nimeshindwa endelea wacha nikojoe nikalale....
Anyway u had a point lakin umezdsha mahaba yako kwa bwana yule.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hutaelewa nilichoandika.

Na siwezi kushangaa , ila mfumo wa elimu ndiyo ninaoushangaa uliofanya uelewa wako uwe ivyo ulivyo.

Any way, Kwa nini umeandika hivyo kuwa Cuba ni masikini huko SAmerica!?
 
Dah!! Nilikua nasoma nukta 2 nukta hadi hapo ulipoanza kumsifia Yohana at n m2 makin kwa taifa le2....
Nimeshindwa endelea wacha nikojoe nikalale....
Anyway u had a point lakin umezdsha mahaba yako kwa bwana yule.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kama ambavyo haizuiliki kuongea madhaifu yake ndivyo isivyozuilika pia kuongea mazuri yake. Unaweza kuwa adunje kwa kimo lakini ukawa mrefu kwa wema,akili,kujitoa,ujasiri na kadhalika.Unaweza kuwa dikteta kwa watu fulani lakini ukafanyika nguvu ya kuwasukuma mbele na kuwanyoosha wale ambao pasi na nguvu hiyo wasingesogea kokote.
 
Kuna watu hawanielewi bado. Ninapoandika hivi kuna watu wanakwazika.Wengine wanafuta maandiko yangu.Tuendelee tutafika mahali tutaelewana tu.Mimi kwa Ubatizo wangu ni Nabii,ni Kuhani na ni Mfalme. Sijipendekezi kwa Magufuli na wala haijawahi kuwa ndoto yangu kujikweza. Nina deni kwa jamii yangu:upendo kwa Tanzania yangu na kwa watu wa Imani yangu na kisha kwa hao wasiokuwa bado Wa Imani Katoliki.

Leo kupitia Mwinjili Matayo 18:15-20, Yesu anatupatia Falsafa na Teolojia ya kumaliza migogoro katika jamii.Anatufundisha jinsi ya kujenga upya mahusiano ya jamii inayokuwa imemomonyoka tokana na migogoro na kutoelewana kwa namna fulani. Ni kama anatufunulia jinsi yeye Kristu alivyofanya kwetu wanadamu pindi tulipomkosea Mungu, pale Bustanini,Edeni.Yesu anatung'amurisha kuwa ilibidi achukue uamuzi Wa kuja kuongea nasi uso kwa uso badala ya kubakia na Umungu wake huku akituangalia jinsi ambavyo tungedumu katika uovu wetu.

"Ndugu yako akikukosa,enenda ukamwonye wewe peke yako na yeye,akikusikia umempata ndugu". Katika simulizi hili la Matayo katika Teolojia hii ya "kuponya" mahusiano yaliyopooza na au kuvunda,Matayo anasema Yesu anatoa njia tatu: kwanza ni mazungumzo kati ya aliyekosewa(aliyekwazwa) na mkosaji.Katika hatua zote tatu aliyekosewa ndiye mtu anayepaswa kutafuta suluhu na sio mkosaji.Mungu alichukua hatua ya kujipatanisha nasi yeye mwenyewe;hakusubiria sisi tumuendee.Kwa nini? Sababu ya upendo. Mwenye upendo kila mara ana macho ya kuona uhusiano wowote unapochafuka na hivi kujinunulia "sabuni" ya kuufua uhusiano huo.

Yesu Kristu kupitia Mwinjii Matayo anasema,ikiwa mazungumzo kati ya Wawili,hayakufua dafu,basi aliyetendwa amtafute mtu mwingine ili Wawili hao pamoja na mkosaji wayazungumze. Na hatua ya tatu ikiwa mkosaji amepungukiwa bado kuelewa udhaifu wake,basi jirani ahusishwe pia.Ndio kusema jamii nzima ihusike katika kumrekebisha mhusika.Yesu anatufundisha kutumia subira katika kujipatanisha.Ni kama kwa njia hii anarejea ile busara ya kutong'oa Magugu miongoni mwa ngano hadi wakati Wa mavuno.

Njia hizi tatu zote anazotupatia Yesu ni kutaka kuturudisha kwenye chimbuko la uelewa Wa mwanadamu.Anatufundisha kuwa mwanadamu ni kiumbe complex na hivi mang'amuzi yake katika jambo lolote lile ni mchakato.Sio jambo la wakati mmoja tu. Ni kama anatuonyesha hata yeye,alitanguliza kwanza Manabii (hatua ya kwanza) kisha ndo yeye akafika pia (hatua ya pili) Na kwamba bado hata yeye hakumaliza kazi hiyo ya kuunda upya uelewa wa mwanadamu na ndiyo kisa aliliacha Kanisa kwa msaada wa Roho Mtakatifu(hatua ya tatu) limalizie kazi hiyo ya majiundo ya nafsi ya mwanadamu kumuelekea Muumba wake. Kwamba ni Kanisa leo linawajibika ku-repair mahusiano baina na miongoni mwetu wanadamu.

Msisitizo wa Wajibu huo Wa Kanisa "kuosha na kufua " mahusiano umeelezwa katika Injili hiyo hiyo ya Matayo,pale Yesu anaposema kuwa: "...Basi nawaambieni wowote mutakaowaondolea dhambi wameondolewa...na wowote mutakaowafungia dhambi wamefungiwa..."

Kanisa ni jamii pana katika Imani.Katika familia (ndoa) unafanyaje pale unapokosewa na mwenza wako ili kurejesha mahusiano? Unakimbilia Instagramu,JF au FB kumuanika mwenzio? Unafanyaje katika uchumba pale mwenzio anapoghafilika? Je, unamuanika kwenye mitandao ya kijamii eti kuomba ushauri kabla ya kuongea ninyi wawili? Jirani yako munapokwaruzana unajipatanisha naye vipi? Je,unamualikia ngoma ya mchiriku (na wamama waliochagua kusomea matusi badala ya Bailojia) ili wakamchambe Mtesi wako? Au unajialika katika kipindi cha uhondo cha Clouds na kuanza kumshambulia jirani yako?

Na kama Taifa tunapoharibu kisiasa,kiuchumi,na au kimaadili tunaunda vipi hayo mahusiano? Najua tunayo Katiba na Sheria za kutusaidia kuponya madhara yoyote yatokeayo katika nyanja mbalimbali za maisha yetu kama watanzania. Lakini,inakuwaje pale ambapo Katiba na Sheria zetu hazitoi nafasi ya kuwarekebisha wenzetu wanaokuwa wameliumiza Taifa?

Vita ya kiuchumi inayoendelea sasa chini ya "Kamanda" Magufuli imetuonyesha wazi kuna baadhi ya "makamanda na maaskari" waliomtangulia Magufuli walifanya uzembe mkubwa sana ama kwa kupotoshwa au kwa makusudi! Kuibiwa kupindukia kwa rasilimali zetu kumewabainisha watu waliozembea sana:Mkapa na Kikwete kama watu waliokuwa na kila aina ya nyenzo ya kujua lolote katika nchi hii lakini hawakuchukua hatua stahiki.

Mtu kufikia kupewa zawadi ya jiwe la Almasi lenye thamani ya dola 200,000,000 na ukachekelea ni kielelezo cha ubinafsi uliokuwa umeota sugu. Ni kana kwamba ubinafsi huo ungekuwa unaweza kujitokeza nje ya miili yao kama yafanyavyo majipu basi miili ya ya viongozi hao ingelikuwa sasa imeenea makovu na madonda kila mahali.

Raisi Magufuli, Hatuwasakami viongozii hao Wawili na hatuna nia ya kudharau ombi lako la kuwaacha wastaafu hao wapumzike kwa Amani. Kwa ujumla wake, vita hii isingelikuwepo na au kuwa ngumu kiasi hiki(kama ambavyo inafikia hata kutuchonganisha sisi kwa sisi,kwa serikali yako kuhisiwa na jaribio la kutoa uhai wa wapinzani wako) kama watangulizi wako hao wangekuwa wamewajibika kikamilifu kama unavyofanya.

Sasa kama Injili inavyotualika leo kwa kututaka kuungamiana dhambi zetu sisi kwa sisi,kuelezana madhaifu yetu baina na miongoni mwetu, kama njia ya kutibu madonda ya Taifa letu yaliyosababishwa na watangulizi wako,nasi tunakualika ujue unalo deni kwa wakosaji hao wa watanzania.Unalo jambo la kufanya zaidi ya kuwatakieni mapumziko mema na yenye amani.

Watanzania wamepinda migongo huko mashuleni kwa kukaa chini na kwenye mawe.Watanzania wamekufa kabla ya umri wanaotakiwa kuuishi sababu ya umaskini. Wapo Watanzania pengine wameenda motoni sababu ya kuwaibia wenzao au kuwa na husuda kwa wenzao sababu ya tu umaskini uliowazunguka. Wamama walipoteza maisha wakati Wa kujifungua kisa hakukuwa na huduma bora za kujifungulia.Wako watanzania walipoteza Maisha kwa njia ya ajali za majini na nchi kavu sababu ya miundombinu mibovu.

Raisi Magufuli, kwa madhila hayo waliyoyapata watanzania huoni kama kuna jambo la ziada la kufanya kwa hao watangulizi wako? Huoni kama "repair" ya Kikatiba na Kisheria inayowawaruhusu kupumzika kwa amani haitoshi? Huoni kama watangulizi wako wanaugua nafsini mwao kwa haya madudu yanayoibuka dhidi yao kwa kila hatua ya vita yako hii katika uchumi? Hivi huoni kama Watangulizi wako wanateseka sana nafsini mwao wanapogundua jinsi walivyochangia uhai wa watanzania wenzao "kunyofoka" hata pale ambapo haikuwa lazima au haikutokea wakati muafaka?

Raisi Magufuli, mimi naiona shida mbeleni kwa watangulizi wako na familia zao. Ni bora mtu ukaugua kuharisha utatibiwa na kupona kuliko kuugua nafsi.Nafsi isononekayo muda wote huishia Kudhoofisha mwili na hata mauti huja kucheza karibu na mhusika. Haya ndio nayaona hapo mbele ikiwa hukuchukua hatua zaidi ya hii ya kuwaacha watangulizi wako wapumzike kwa Amani. Amani ni tunda la utulivu Wa kiakili na kisaikolojia.

Hebu sasa uazime Teolojia ya Injili ya Leo: watanzania waliokosewa na watangulizi wako wanatamani wazungumze na watesi wao.Watanzania wanataka kutibu majeraha ya mahusiano mabovu kati yao na hao watangulizi wako.Sote ni nchi moja.Sote ni watoto Wa Mama Tanzania.Wametukosea watanzania.Wametukosea sana.Watoke waje waungame mbele ya watanzania.Waje tusemezame.

Hebu zungumza nao na uwaambie waangalie namna ya kuwataka radhi watanzania.Haitoshi kujuta tu mioyoni mwao kimya kimya.Waje watueleze jinsi walivyoteleza katika kuwatumikia watanzania wenzao na watugawie mang'amuzi yenye mafundisho kwa ajili ya viongozi Wa vizazi vijavyo.

Raisi Magufuli,njia hii ya watangulizi wako kuja mbele ya watanzania wenzao kuridhiana pengine kwa Tume Maalumu italiacha Taifa limeshikamana.Maridhiano ndio OMO ya kuifua Tanzania baada ya kuchafuka na "kuharishiwa" namna hii.Maridhiano ndio njia ya kudumu ya watangulizi wako kuishi kwa Amani.

Unayo masikio,nadhani umenisikia na waelewe watanzania.
ndefu mno
 
ndefu mno

Hata ubongo wako ni mrefu sana sema tu hutaki kuuvuta! Maisha ni safari ndefu pia inayohusisha kuchoka wakati mwingine.Lakini pale,unapijihisi kuishiwa nguvu za kujisomea ndipo hapo mambo ya maana kwa ajili ya maisha yako yanapooanzia. Hakuna maarifa yoyote yasadikikayo kumfaa mwanadamu yasiyokuwa ya kina na mapana. Je,wataka mambo mafupifupi na machache? Wale watakao mambo mengi na ya kina hao uelewa na ujuzi wao nao huwa Wa kina na kinyume chake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom