SANCTUS ANACLETUS
JF-Expert Member
- Mar 5, 2016
- 3,337
- 4,664
Ni hivi bila kupepesa macho tunataka kukusaidia kazi. Umejitoa mno kuliko hata tulivyotarajia ufanye.Tunataka sasa vita hii ya kiuchumi uliyoaianzisha ishike kasi.Ikolee na kila mtu akolee.
Mkapa na Kikwete walikuwa na macho lakini hawakuwaona hawa "maharamia Wa kisomali" Wa Madini yetu. Mkapa na Kikwete walikuwa na masikio lakini hawakusikia vilio vya watanzania kuwa tunaibiwa.
Naam hawakusikia wala kuona ndugu zetu wakifia hospitalini kwa kukosa matibabu kabisa au kucheleweshwa kwenye matibabu sababu ya ubovu au ukosefu wa miundombinu.
Hawa wenzetu Ben na JK hawakusikia wamama wajawazito wakifa kwa maumivu makali ya kukosa huduma bora za kujifungulia.Kisa nini? Maharamia ya kiuchumi ya kisomali hayakulipa kodi stahiki.Lakini cha ajabu na kukerehesha ni kwamba Ben na JK walikuwa wanasikia tu sauti za hao "wawekezaji" pale walipohitaji maeneo zaidi ya migodi ya kutuibia. Orodha ya ujinga wote uliofanyika kipindi chote hiki dhidi ya hao wezi na wengine ni ndefu kishenzi.
Sasa itoshe kusema kuwa Kwa mantiki hiyo sasa mwishoni mwa kushughulikia jambo hili tutawaomba Kikwete na Mkapa waje mbele ya watanzania waungame waziwazi toka nafsini mwao jinsi walivyoweza kuvumilia ushenzi Wa hao wawekezaji.
Waje waombe radhi kwa kuzembea kiasi cha namna hii hadi leo kuna maeneo tumeachiwa mashimo.Rais Magufuli aunde tume ya maridhiano ili hawa ndugu zetu watoke nao "walie" mbele ya watanzania kwamba hata mikopo anayohangaika Magufuli kukopa imeletelezwa na wao kutosikia ya watanzania licha ya kwamba walikuwa na taarifa zote ama toka kwa wanyetishaji wa serikali au raia Wa kawaida.
Lazima waje waungame kama kweli ni waungwana na wanajitambua na kwamba kwa kiasi kikubwa maisha yetu yameharibiwa nao.