Raisi Magufuli, kwanini serikali yako isibadili katiba na sheria wanaohama vyama wahame na ubunge au udiwani wao kama kweli mna uchungu na kodi zetu?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Awamu hii ni awamu inayojiapambanua kama ni awamu ya kubana matumizi na ni awamu ya viongozi wazalendo na zaidi kucheza na hela za umma ni kujitafutia matatizo.

Swali langu kwa hii serikal ni kwanini spirit hii hatuioni katika hizi fedha za kugharimia chaguzi ndogo ambazo ni mabilioni ya hela za walipa kodi fedha ambazo zingeweza kuokolewa kwa kubadili tu katiba na sheria ya uchaguzi kuruhusu wanaohama vyama wahame na ubunge au udiwani wao na hivyo kuokoa mabilioni haya yanayotumika kugharamia chaguzi hizi za marudio?

Kama tumedili sheria kadhaa ndani ya kipindi hiki kifupi tu ikiwemo sheria ya takwimu hivi karibuni, kwani hatufanyi hivyo kwa sheria ya uchaguzi ili tuokoe mabilioni haya?

Je, ni kweli mna dhamira ya dhati ya kubana matumizi na kuokoa hela za walipa kodi wa nchi hii?

Au kulinda nidhamu na uti wa wanasiasa kwa vyama vyao ndio jambo lenye masilahi zaidi kwa nchi kuliko hili la kuokoa mabalioni haya yanayoteketea katika hizi chaguzi za kila siku?

Tusipojihurumia sisi wenyewe, nani mwingine wa kutuhurumia?

Wazungu wana msemo: "Charity begins at home."
 
Magufuli hana uchungu wowote na maisha ya mlalahoi zaidi ya kuwa na uchungu na madaraka yake ambayo anayalinda kwa gharama kubwa ikiwamo kufuja fedha za umma na kutumia vibaya vyombo vya usalama ili kudumisha madaraka yake

Kama kweli ana uchungu na maisha ya Watanzania basi atuletee katiba mpya itakayoweka mifumo imara ya uwajibikaji kwenye mihimili ya dola na katika taasisi zingine za umma, vinginevyo itakuwa ni sawa na kujificha kwenye shamba la karanga akijua kuwa haonekani

Mgombea binafsi ndio suluhu la ujinga wote huu
 
Hahaha mfano Chaumma tunahamia sisiemu na kugombea kwa tiketi ya sisiemu tukishinda tunarudi zetu chaumma huku tuna ubunge wetu na udiwani wetu.
Matokeo ya mwisho ni chaumma kua na wabunge na madiwani wengi kuliko chama chochote.

Hapo vipi?
 
Awamu hii ni awamu inayojiapambanua kama ni awamu ya kubana matumizi na ni awamu ya viongozi wazalendo na zaidi kucheza na hela za umma ni kujitafutia matatizo.

Swali langu kwa hii serikal ni kwanini spirit hii hatuioni katika hizi fedha za kugharimia chaguzi ndogo ambazo ni mabilioni ya hela za walipa kodi fedha ambazo zingeweza kuokolewa kwa kubadili tu katiba na sheria ya uchaguzi kuruhusu wanaohama vyama wahame na ubunge au udiwani wao na hivyo kuokoa mabilioni haya yanayotumika kugharamia chaguzi hizi za marudio?

Kama tumedili sheria kadhaa ndani ya kipindi hiki kifupi tu ikiwemo sheria ya takwimu hivi karibuni, kwani hatufanyi hivyo kwa sheria ya uchaguzi ili tuokoe mabilioni haya?

Je, ni kweli mna dhamira ya dhati ya kubana matumizi na kuokoa hela za walipa kodi wa nchi hii?

Au kulinda nidhamu na uti wa wanasiasa kwa vyama vyao ndio jambo lenye masilahi zaidi kwa nchi kuliko hili la kuokoa mabalioni haya yanayoteketea katika hizi chaguzi za kila siku?

Tusipojihurumia sisi wenyewe, nani mwingine wa kutuhurumia?

Wazungu wana msemo: "Charity begins at home."
Mkuu hapo kwenye kuhama na ubunge haiwezekani kabisa, kwasababu wanaogopa ipo siku watamwacha peke yake .na kuhamia upinzanii.
 
Magufuli hana uchungu wowote na maisha ya mlalahoi zaidi ya kuwa na uchungu na madaraka yake ambayo anayalinda kwa gharama kubwa ikiwamo kufuja fedha za umma na kutumia vibaya vyombo vya usalama ili kudumisha madaraka yake

Kama kweli ana uchungu na maisha ya Watanzania basi atuletee katiba mpya itakayoweka mifumo imara ya uwajibikaji kwenye mihimili ya dola na katika taasisi zingine za umma, vinginevyo itakuwa ni sawa na kujificha kwenye shamba la karanga akijua kuwa haonekani

Mgombea binafsi ndio suluhu la ujinga wote huu
Alafu utawasiki wamkifananisha na Nyerere!! Hawa watu hawana aibu kabisa!
 
Awamu hii ni awamu inayojiapambanua kama ni awamu ya kubana matumizi na ni awamu ya viongozi wazalendo na zaidi kucheza na hela za umma ni kujitafutia matatizo.

Swali langu kwa hii serikal ni kwanini spirit hii hatuioni katika hizi fedha za kugharimia chaguzi ndogo ambazo ni mabilioni ya hela za walipa kodi fedha ambazo zingeweza kuokolewa kwa kubadili tu katiba na sheria ya uchaguzi kuruhusu wanaohama vyama wahame na ubunge au udiwani wao na hivyo kuokoa mabilioni haya yanayotumika kugharamia chaguzi hizi za marudio?

Kama tumedili sheria kadhaa ndani ya kipindi hiki kifupi tu ikiwemo sheria ya takwimu hivi karibuni, kwani hatufanyi hivyo kwa sheria ya uchaguzi ili tuokoe mabilioni haya?

Je, ni kweli mna dhamira ya dhati ya kubana matumizi na kuokoa hela za walipa kodi wa nchi hii?

Au kulinda nidhamu na uti wa wanasiasa kwa vyama vyao ndio jambo lenye masilahi zaidi kwa nchi kuliko hili la kuokoa mabalioni haya yanayoteketea katika hizi chaguzi za kila siku?

Tusipojihurumia sisi wenyewe, nani mwingine wa kutuhurumia?

Wazungu wana msemo: "Charity begins at home."
Unaijua siasa kweli?,unajua mtaji wa chama cha siasa?,je hao wanaohama toka chama chako pendwa wangekua ndo wanahamia chama chako ,ungeleta huu utumbo?
 
Back
Top Bottom