Raisi Magufuli avunja rekodi. Awafunika watangulizi wake wote ndani ya muda mfupi!

Wakati wa Kikwete kulikuwa na raha sana ya kuishi Tanzania.

Awamu hii ya tano unga wa mahindi umefikia kilo shillingi 800 na Magufuli alipoingia ulikuwa 1400. Ni hatua kubwa sana. Sema vyuma vimekaza.
Nenda kwa wakulima kawaambie maneno haya kama hujatoka na ngeu! Wakulima wanalia kilimo hakina faida wewe unashangilia!

Halafu kushuka kwa bei ya mazao inategemea uzalishaji wake ambao mwaka Jana ulikuwa mkubwa sana
Sent using Jamii Forums mobile app
 
yeye anakwambia kwa jinsi anavyo chapa kazi kawafunika awamu zote 1-4 hahaahhahahaha

naona alikuwa anazungumzia alivyo lipaisha deni la taifa amewazidi wote.

Anakwambia ni makusanyo ya ndani deni linapaa tu (anakopa mlango wa nyuma kujinufaisha kijanja)
 
Weka kwa dolar kwa madafu hauwezi kulinganisha hivyo, ukiweka kwa dolar unaweza kuta watangulizi wake waliacha deni kubwa kuliko la JPM.


Kumbe unafahamu halafu unajifanya hujui? Kama shilingi itakuwa imepanda dhidi ya dola basi hongera zake.

Kama imeshuka dhidi ya dola, unadhani uchumi unapaa au unaporomoka?
 
Huyu baba sio mzima ila akisikia Lissu anahutubia mahari lazima atafute kitu cha kuzindua hata choo atazindua
 
Deni linazidi kuongezeka na maisha yanazidi kua magumu alafu tunahimizwa tuwe wazalendo!!!ukweli kabisa naamini huyu mtu hayuko kwaajili ya wanyonge kama tunavyodanganywa.
 
umeamua kuandika kinyume nyume, CHADEMA mna matatizo sana
We jamaa unakumbukaga nilikuomba kazi miaka hiyooo...ukaniahidi kunipa kukawa kimya...dah maisha yanaenda kasi..nashukuru lakini kwa mwitikio wako.Mungu kaniwezesha saaana.....

Ila bado hujaacha unafki wa kuipenda sisiemu???
Dah ila we jamaa bana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Deni linazidi kuongezeka na maisha yanazidi kua magumu alafu tunahimizwa tuwe wazalendo!!!ukweli kabisa naamini huyu mtu hayuko kwaajili ya wanyonge kama tunavyodanganywa.

Tembea vifua mbere.. wi a on ze rait tirak
 
Huyu Jiwe atakuwa anakopa kwa jina la taifa lakini anazitumia yeye na watu wake, kama mobutu.
Kila mwezi makusanyo ni trilioni na ushei, anakopa pesa kibao, lakini bado mzunguko wa hela haupo mitaani. Kila sekta inalalamika.
Ndo mana yuko tayari kuua ili watu wasizungumze kuhusu mabaya yake na ufisadi wake.

Korosho, vitambulisho, standard gauge, dreamliner/bombardier/airbus, stieglers gorge.. Humu lazima kuna ulaji
 
Ndivyo tunaweza kusema! Raisi Magufuli amevunja rekodi kwa kupaisha deni la taifa ndani ya miaka takribani mitatu aliyokaa madarakani tofauti na watangulizi wake.

1. Raisi JK Nyerere 1961-1985 aliacha deni la taifa la shilingi trilioni 3.

2. Raisi AH Mwinyi 1985-1995 (miaka 10) alipaisha deni la taifa kutoka trilioni 3 hadi trilioni 18 sawa na ongezeko la trilioni 1.8 kila mwaka.

3. Raisi BW Mkapa 1995-2005 (miaka 10) alikuta deni la taifa ni trilioni 18. Akalipa na kulipunguza hadi trilioni 10 sawa na punguzo la bilioni 800 kila mwaka.

4. Raisi JM Kikwete 2005-2015 (miaka 10) alikuta deni la taifa ni trilioni 10 akalipaisha hadi trilioni 40 sawa na ongezeko la trilioni 3 kila mwaka.

5. Raisi JP Magufuli Novemba 2015- Novemba 2018 takribani miaka mitatu, deni hilo limepaa hadi trilioni 61.8 sawa na ongezeko la trilioni 21.8 (trilioni 7.2 kila mwaka)

Je, kwa ambao wamefanikiwa kuishi awamu zote hizi, wapi kulikuwa/kuna unafuu wa maisha kwa ujumla?

Hapa ni nani Raisi wa wanyonge(nomino) na nani Raisi wa wanyonge(kitenzi)?

Kwasasa kila mtanzania (hata mtoto anayenyonya) anadaiwa zaidi ya shilingi milioni moja ili kulipa deni hilo.

Awamu inayo kusanya kodi kuliko awamu zote ...

Deni la taifa juu,upinzani wataka CAG kufanya ukaguzi

Tusisahau zigo la deni la taifa

Deni la Taifa lafika Sh53 trilioni

Deni la Taifa Lazidi Kukua Lafikia Shilingi Trilioni 61.8 | UDAKU SPECIAL BLOG
INGEPENDEZA kama ungeuliza pia deni hilo limetumikaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa hisabati ya milinganyo:
Miaka 3=21.8
miaka 10=?

(10×21.8) ÷ 3= 72.7

Kwahiyo mpaka anatoka (kama atatawala miaka 10) atakuwa ameongeza deni la trilioni 72.7 +deni alilokuta trilioni 40 jumla trilioni 112.7
Nani atamkopesha hela zote hizo .
 
Back
Top Bottom