Raisi leksandar Vucic aongoza Waserbia katika kumbukizi ya mauaji yaliyofanywa na NATO 1998

Tushukuru kuwepo kwa Taifa la marekani na kusema thanks you America. Je urusi ingeshika hatamu ya Dunia vijana wangapi wangeswekwa kinguvu vijijini? Je uhuru wa kuabudu ungekuwepo?jamani muone uhweli wa mambo jinsi gani Urusi walitaka kusambaza sera za hovyo sana duniani. kwa nini wakimbizi wote duniani hukimbilia Ulaya magharibi, Israel na USA na hawataki kwenda Urusi? ushamuona msomali kakimbilia Urusi?
Kwani urusi hakuna uhuru wa kuabudu? Bila ya taifa la marekani hao wakimbizi wangetoka wapi? Usimsifu kwa kupokea watu aliosababishia shida. Watu kila siku huko Afrika magharibi wanakimbilia ulaya kwa njaa na umasikini wa nchi zao unaopelekea hali ya amani kutokuwepo. Bila serikali imara usalama na utulivu ni ndoto. Rasilimali zinalisha taifa kama Ufaransa kwa wizi... nchi zinabaki masikini wakipokelewa wakimbizi Paris utasema asante Ufaransa? Kongo na Afrika ya kati machafuko miongo kadhaa.. serikali zinachezewa na kilevi cha rushwa unaoletwa na hao wamarekani & co wanabeba mali govt zinashindwa kuhimili kuendesha nchi kwa usalama na utulivu. Wakongoman wakipewa uraia ubelgiji utasemz asante Belgium? Serikali za Ureno, Uswizi n.k. zinakubali hela za mafuta Angola kuwekwa kwao bila kuhoji wakipokea wakimbizi utasema asante Western Europe?

Hakuna wema duniani. Hizo nchi zisingeimport au kuruhusu mashirika yao kufanya wizi na rushwa nje ya mipaka yao kama wanavyobanana kwao ingekuwa ndio wema zaidi ya kupokea wakimbizi, kutoa misaada au mikopo.
 
Suala la kufikiria ni kwamba ubepari tandawazi (imperialism) lazima iwapelekee shida au manufaa madogo wale wanaopokea uchumi wa kigeni... makampuni ya kibepari yanatoka kwao kufata faida zaidi. Kwa anaelewa namna faida inavyopatikana lazima ajue zinapokuja Afrika ni kwamba kijachobaki ni kidogo, kinachotoka ni kingi. Kwa uwiano huu wa unyonyaji Russia na Western Europe nani mwema kwa Waafrika? Nani anaesababisha shida za mwafrika kati yao? Nani anyenyonya zaidi mali ya Afrika?

Vita ni matokeo ya huo mfumo wa ubepari. Ubepari bila kukua unaanguka. Ni hili hitaji la kukua kwa namna yoyote inayoleta shida. Taifa lolote hatimae lina kikomo cha kasi ya ukuaji wa uchumi. Hapo sasa ndio ubepari huvuka mpaka kuingia nchi zingne. Hakuna nchi duniani ambayo haijaguswa na hii kansa, kama yapo machache mno na madogo. Hata China ambayo iliachana na ujamaa imekuwa sana kiasi cha kuhitaji kutoka nje kupata zaidi ya kilichopo kwao. Lengo ukuaji uendelee. Sasahivi wametanda kila kona duniani kusaka ukuaji wa masoko na kupata rasilimali.

Taja taifa lisilo la kibepari lililovamia nchi au bara la mbali na kwao.
 
Back
Top Bottom