Raisi Kikwete agawa noti, Salma Kikwete agawa noti! Siyo Rushwa hii?

Mzizi wa Mbuyu

JF-Expert Member
May 15, 2009
7,320
6,806
Ni utaratibu ambao sijawahi kuuona kwa hapa kwetu Tanzania. Imeripotiwa na vyombo vya habari nchi kuwa Raisi Kikwete aliwatuza pesa wacheza ngoma wote waliokuwa wanatumbuiza......na hali kadhalika imeripotiwa kuwa Mama Salma Kikwete aliwapa pesa tasilimu wagonjwa wote wodini kama 'eti' asante kwa mama mmoja kujifungua mtoto na kumuita Salma.
Jamani, utaratibu huu wa kugawa manoti wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu, siyo hongo hii kwa wapiga kura?
 
no doubt ni hongo!!! PCCB kamata mama salma na ahojiwe...na huyu naye mtoto wa kikwere bunge limjadili..yale yale nilisema huyu anasaini sheria hii anajua madhara yake..yaani kisha sahau kabisa kama hiyo ni rushwa....yaaani CCM bana,ukiwabana huku wanahamia huku hawa wanaweza hata kuwa wanahamishia vocha/salio kwenye simu za watu ili wawachague..
 
kugawa sh mia tano tano kwa watu wenye shida ni dharau - hii si njia mbadala ya kumsaidia mtu - kama wangekuwa na uchungu na watu hawa wangeshaweka sera safi za kuwasaidia - ningekuwa mimi bora nife kuliko kupokea hii mia tano.
 
Ni utaratibu ambao sijawahi kuuona kwa hapa kwetu Tanzania. Imeripotiwa na vyombo vya habari nchi kuwa Raisi Kikwete aliwatuza pesa wacheza ngoma wote waliokuwa wanatumbuiza......na hali kadhalika imeripotiwa kuwa Mama Salma Kikwete aliwapa pesa tasilimu wagonjwa wote wodini kama 'eti' asante kwa mama mmoja kujifungua mtoto na kumuita Salma.
Jamani, utaratibu huu wa kugawa manoti wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu, siyo hongo hii kwa wapiga kura?
Hoja kama hizi wakati mwingine zina divert some serious issues za kujadili kitaifa
 
Hiyo sio hongo. Wala sio rushwa. Pia sio mlungula. Ni takrima tu. Ukarimu wa Kitanzania.
 
Mi nisichoelewa hivi hawa viongozi wanapotoa hizi hela ni zao au za chama? maana utasikia leo JK katoa milioni ??kusaidia hospitali mara mkuu wa mkoa katoa laki sijui ngapi kuchangia wahanga mara mbunge sijui nae katoa hizo hela wanazirekodi mahala ili zifanyie audit au ndio kama mkuu hapo juu anavodai ni mwanzo wa kampeni. Inabidi waanze kuweka wazi haya mambo, najau ikulu wanayo bajeti ya michango lakini jinsi inavotumika ndo sielewi...
 
Hii ni zaisdi ya dharau ELNINO yaani haya ni matusi, anafikiri mia tano itampunguzia mtanzania machungu ya kukosa shule bora, huduma bora za afya, barabara bora na hata chakula. Well tuseme sawa kawapa mia tano, kwa maisha ya sasa ya Tanzania mia tano utanunua nini cha maana, yaani JK kaona waTZ ni wakuishi kwa mia tano kweli! nimeamini akutukanae akuchagulii tusi! kugawa mia tano maana yake ni kuwataka hawa waTz waendelee kuishi kwa kula kauzu na ugali wa unga robo, au kuwataka waTz waendelee kudhulika kwa kunywa kachaso, ndio maana mia tano ndio inatosha kununua kinibu kimoja cha kachaso! ooooh! nakukulia mama Tanzania, where the hell did we go wrong to deserve all these?
 
no doubt ni hongo!!! PCCB kamata mama salma na ahojiwe...na huyu naye mtoto wa kikwere bunge limjadili..yale yale nilisema huyu anasaini sheria hii anajua madhara yake..yaani kisha sahau kabisa kama hiyo ni rushwa....yaaani CCM bana,ukiwabana huku wanahamia huku hawa wanaweza hata kuwa wanahamishia vocha/salio kwenye simu za watu ili wawachague..

Aaah ushawapa namna.....subiri utaisikia.Believe me...
 
Mwaka huu tutasikia mengi na kuona faulu nyingi bila vyombo vya dola kufanya chochote.
 
Duh aibu!!!! Sh.500/-????? yote ni dharau tena hali ya juu hata aibu hana shs.500 hata pipi hupati.
 
Duh aibu!!!! Sh.500/-????? yote ni dharau tena hali ya juu hata aibu hana shs.500 hata pipi hupati.
Mama, hii post ilikuwa ni ya utani tarehe 1 April. Ilikuwa fool's day wengine tunaiita jokes' day. Angalia tarehe kwanza!
 
Back
Top Bottom