Moja ya sifa ambazo kiongozi wa umma au nchi anapaswa kuwa nazo, ni uwezo wa kusahihisha mapungufu, madhaifu na mabaya ya uongozi ulimotangulia.
Waswahili husema siku hazigandi. Na ndivyo tunavyoweza kusema kuwa siku za Magufuli hazigandi na ukweli zinapita kama upepo. Kwa mantiki hiyo na ili kuepuka makosa yanayofanywa kipindi cha uchaguzi na kuwaacha watu wakilalamika, kusononeka na kulaani serikali yao kwa miaka mitano, ni vema watanzania wakaanza kujihoji kuwa wanamtaka kiongozi mwenye sifa zipi ataeendeleza mazuri ya utawala huu lakini zaidi kuyashugulikia madhaifu, mapungufu na mabaya yaliyosababishwa na utawala huu unaopita.
Kwa upande wangu, ninaona kiongozi ajaye apaswe kuwa na SIFA na UWEZO wa kushughulikia mapungufu yafuatayo:-
>> Kukufufua utawala bora unaoheshimu haki na uhuru wa binadamu (Watanzania) na bila ubaguzi.
>> Kufufua mahusiano yanayodorora na washirika wetu wa maendeleo wa kimataifa.
>> Awe muumini wa umoja wa kitaifa bila kujali rangi, dini, chama, kabila, umri au eneo mtu atokako.
>> Kusaidia kuinua sekta binafsi ambae ni mbia muhimu sana wa kuchochoea maendeleo ya Taifa na Watanzania.
>> Kufufua ari na morali ya wafanyakazi, wakulima, wafugaji na wavuvi wanaoonesha kukata tamaa kutokana ugumu wa maisha.
>> kufuta sheria zote za kikandamizaji kisiasa na kiuchumi.
>> Kukamilisha uandikwaji wa katiba mpya itakayoendana na mahitaji yetu ya sasa.
>> Kupunguza ukubwa wa bunge kama lilivyo sasa, ambao hauna tija. NK.
Naamini yapo mengi. Lakini the baseline ni kwamba, ni muhimu kwa wananchi kujiandaa kifikra mapema.