Raisi atakayemrithi Magufuli ni yule atakayeturidhisha anazo sifa hizi....

mwengeso

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
6,797
2,000
Moja ya sifa ambazo kiongozi wa umma au nchi anapaswa kuwa nazo, ni uwezo wa kusahihisha mapungufu, madhaifu na mabaya ya uongozi ulimotangulia.

Waswahili husema siku hazigandi. Na ndivyo tunavyoweza kusema kuwa siku za Magufuli hazigandi na ukweli zinapita kama upepo. Kwa mantiki hiyo na ili kuepuka makosa yanayofanywa kipindi cha uchaguzi na kuwaacha watu wakilalamika, kusononeka na kulaani serikali yao kwa miaka mitano, ni vema watanzania wakaanza kujihoji kuwa wanamtaka kiongozi mwenye sifa zipi ataeendeleza mazuri ya utawala huu lakini zaidi kuyashugulikia madhaifu, mapungufu na mabaya yaliyosababishwa na utawala huu unaopita.

Kwa upande wangu, ninaona kiongozi ajaye apaswe kuwa na SIFA na UWEZO wa kushughulikia mapungufu yafuatayo:-

>> Kukufufua utawala bora unaoheshimu haki na uhuru wa binadamu (Watanzania) na bila ubaguzi.

>> Kufufua mahusiano yanayodorora na washirika wetu wa maendeleo wa kimataifa.

>> Awe muumini wa umoja wa kitaifa bila kujali rangi, dini, chama, kabila, umri au eneo mtu atokako.

>> Kusaidia kuinua sekta binafsi ambae ni mbia muhimu sana wa kuchochoea maendeleo ya Taifa na Watanzania.

>> Kufufua ari na morali ya wafanyakazi, wakulima, wafugaji na wavuvi wanaoonesha kukata tamaa kutokana ugumu wa maisha.

>> kufuta sheria zote za kikandamizaji kisiasa na kiuchumi.

>> Kukamilisha uandikwaji wa katiba mpya itakayoendana na mahitaji yetu ya sasa.

>> Kupunguza ukubwa wa bunge kama lilivyo sasa, ambao hauna tija. NK.

Naamini yapo mengi. Lakini the baseline ni kwamba, ni muhimu kwa wananchi kujiandaa kifikra mapema.
Moja ya sifa kuu ya kiongozi yeyote ni kujua na kutambua mabadiliko ya nyakati.

Kwa wakati huu hakuna kiongozi bora zaidi ya Magufuli ambaye ameweza kutafsiri kwa vitendo mabadiliko ya nyakati.

Baba wa Taifa alijenga utaifa na kuhamasisha siasa ya ujamaa na kujitegemea.

Rais Mwiyi, Mzee wa Rukhsa, alishawishika na wana mageuzi walioamini siasa ya ujamaa na kujitegemea isingewaondoa WaTz kwenye umaskini.


Rais Mkapa akatumbukizwa kwenye siasa ya kimataifa ya soko huria na kuruhusu ubinafsishaji hata njia kuu za kujenga uchumi imara wa nchi. Akajikita kwenye siasa ya utawala bora akiacha uchumi kujiendesha holela.

Rais Kikwete, bingwa "changanya yake na yako" akaicha nchi katika utawala wa walio nacho matokeo yake nchi ikawa soko la bidhaa za nje na kuzalisha kundi la machinga.

Rais Magufuli amekusanya yote hayo katika kapu moja kwa kaulimbiu yake "hapa kazitu". Naamini ni wachache wanaijua kwa kina kaulimbiu hiyo. Ila kwa tafsiri nyepesi "asiyefanya kazi na asile".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
K

kakolaki

JF-Expert Member
Apr 6, 2017
709
1,000
Kwahiyo baada ya kuwa na raisi kama JPM kwa hii miaka mitatu aliyokaa madarakani je wewe binafsi kimaisha umefikia wapi? Hali ya uchumi unaionaje kwa hii miaka mitatu? Kama miaka 3 amefail hata kuongeza mishahara kwa watumishi, miaka 20 si ndo atawaua watu huyu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna nchi inayowekeza huku mishahara na matumizi ya kila siku yakaachwa vilevile, ni lazima kizazi hiki kijitolee kuumia kwa ustawi wa vizazi vijavyo. Tatizo letu wengi tunataka tuenjoy sisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
K

kakolaki

JF-Expert Member
Apr 6, 2017
709
1,000
Kwahiyo baada ya kuwa na raisi kama JPM kwa hii miaka mitatu aliyokaa madarakani je wewe binafsi kimaisha umefikia wapi? Hali ya uchumi unaionaje kwa hii miaka mitatu? Kama miaka 3 amefail hata kuongeza mishahara kwa watumishi, miaka 20 si ndo atawaua watu huyu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna nchi inayowekeza huku mishahara na matumizi ya kila siku yakaachwa vilevile, ni lazima kizazi hiki kijitolee kuumia kwa ustawi wa vizazi vijavyo. Tatizo letu wengi tunataka tuenjoy sisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
gemplatnumz

gemplatnumz

Senior Member
Jan 24, 2017
135
500
Tusidanganyane ,Magufuli anachapa kazi kasoro alizo nazo ni za kibinadamu tu, kwa ilo namtetea, siwezi kusema nchi haina rais, yupo chuma
 
bush crazy

bush crazy

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
407
1,000
Mkuu P. Muta, kwanza asante kwa bandiko lako.
Jf, kama ilivyo nchi ya Tanzania ni ya wote, wakubwa kwa wadogo, walio soma na wasio soma, walio ishia darasa la 4, la 7, QT, MEMKWA, sekondari za Kata, hadi waliofika vyuo. JF ni ya wote Watanzania na watu wa majirani zetu wanao pose kama Watanzania, yaani JF ni ya wote, hivyo ukikutana na bandiko lenye makosa madogo madogo spelling, na panctuation, kwanza saidia kuonyeshea makosa, kisha saidia kurekebisha maana huwezi jua, hivyo katika kusaidia huku kunaifanya jf kuwa ni mtandao darasa, kama lilivyo shamba darasa kwenye kilimo. Hivyo karibu darasani.
Kwanza nimekuorodheshea spelling mistakes kwa numbers, sijaorodhesha panctuation mistakes, kisha nimekurekebishia.
Mimi nisingekuwa Mwandishi wa Habari, ningekuwa Mwalimu wa primary darasa la 3.
P
nimeipenda hiyo style ya ku edit! kuna programu au inakuwaje?
 
Top Bottom