Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,278
.
Ifike wakati busara kubwa itumike kuliongoza hili taifa, Raisi na watu wake watambue tu kuwa taifa hili haliwezi kuongozwa kwa kutumia nguvu nyingi sana na vitisho.
Hata kama Watanzania ni wavivu, wajinga, wanafiki, ila hizi sifa zote haziwezi kufutika ndani ya siku moja au mwaka mmoja. Vitu vyote hizi vinahitaji uvumilivu, busara na hekima kuviondoa.
Hata mitume walipotumwa hawakuweza kuwabadilisha binadamu wote kwa siku moja, na hata pale walipokabiliana na hali kubwa ya upinzani hawakuwahi kuonyesha chuki na visasi kwa wale wote waliokengeuka na kuwapinga hadharani, bali waliwaombea kubadilika na kuwa wema.
Raisi asiwafundishe watu ukaidi na visasi, anatakiwa kuhubiri umoja kuanzia ndani ya nafsi yake.
Binadamu ni kiumbe cha ajabu sana kuliko Rais anavyofikiria, mazuri yote yanaweza futika kwa jambo moja tu ambalo angeweza kulizuia, wapo wana ccm ndugu zao wa kuzaliwa ni Chadema na vyama vingine vya upinzani, wapo wazazi watoto wao ni Chadema na Cuf , je kwa kauli kama hizi kweli familia hizi zitengane kwa sababu ya vyama?
Kama kuna mtu anahisi ataiweza Tanzania kwa kutumia nguvu afikiri upya.
Ukitaka kufanya tafiti zako hebu anzia 2015 mpaka leo,
====>>Je nchi hii imeacha kuwa ombaomba?
===>>Hakuna tatizo la ajira?
===>>Miundombinu yote ishakamilika?
===>>Elimu yetu ishakuwa bora kwa kiwango kinachokiwa?
===>>Kilimo kimekuwa na tija sasa?
===>>Migogoro ya ardhi imeisha ?
===>>Huduma za afya zote zinapatikana maeneo yote nchini?
===>>Viwanda vimejengwa kwa wingi nchini nzima?
===>>Mfumuko wa bei umepungua kwa kiwango kikubwa?
===>> Njaa hakuna tena Tanzania?
===>>Biashara zetu zimeimarika?.
===>>Nchi nzima hakuna ukandamizaji wa demokrasia ?
===>> Hali ya uchumi imekuwa nzuri?
==>>Ujambazi umeisha, hata kule Pwani hali ni shwari sasa?
Kama haya yote hayajaleta matumaini zaidi ya ahadi tu na kujenga kila siku, basi Rais na wale wote wenye dhamana ya uongozi wakae wakijua Tanzania itajengwa na Watanzania wote kwa kushirikishwa kwao na kuwa pamoja katika ujenzi huo na sio hulka ya mtu mmoja.
Na kama Watanzania wataamua kukataa kushiriki basi hatakuwepo mtu yoyote atakayeweza kuijenga nchi hii peke yake.