Raisi apunguziwe madaraka – viongozi wathibitishwe na bunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Raisi apunguziwe madaraka – viongozi wathibitishwe na bunge

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Oct 28, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Oct 28, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  RAISI APUNGUZIWE MADARAKA – VIONGOZI WATHIBITISHWE NA BUNGE

  Samahani , Kuna jambo moja limetokea kunichanganya kidogo kwa kipindi hichi cha wiki 2 zilizopita kuhusu uongozi wetu na matendo mengine yanayoendelea ndani ya nchi .

  Moja ni hili la raisi kuteuwa viongozi wa serikali bila bunge kuithinisha uteuzi huo , kwanini hili jambo linakuwa hivi na wakati nchi hii ni ya democrasia ? kwa nini teuzi za raisi hazihojiwi mahala popote hata anapoenda bungeni kama alivyofanya mwanasheria mkuu ni kufanya mambo mengine tu ?

  Kama kweli tunataka utawala bora basi ni vizuri raisi apunguziwe madaraka aliyonayo ya kuchagua viongozi wa kiserikali bila viongozi hao kupitishwa na bunge kwa uwazi na uhuru kabisa bila kujali itikadi za kisiasa au aina nyingine za kufungwa midomo .

  Pia maamuzi mengine ambayo aliyafanya mheshimiwa raisi ya kuamua kuwasha mitambo ya IPTL , mimi ninavyojua mitambo hiyo iliwahi kuwa na mgogoro Fulani sijui kama umeisha wanaojua naomba wanisaidie , inaonyesha kuna vipengele vya sheria vimevunjwa katika kuwasha mitambo hii bila kuangalia athari ambazo zinaweza kutokana na uwashaji huu huko mbeleni , tunaoathirika ni sisi walipa kodi .

  Mimi naona raisi apunguziwe madaraka , inawezekana baadhi ya vitu vinakosa kufanyika au kutendeka kwa usahihi kutokana na rundo hili la kazi anazopewa raisi pamoja na wasaidizi wake wengine .

  Teuzi zote zipitishwe na bunge kwanza kabla ya kuamua kumpitisha kiongozi huyo , tumeona huko nyuma bunge limewahi kuwa na matatizo Fulani na mwanasheria mkuu aliyopita sio huyu tu hata baadhi ya mawaziri na viongozi wengine ambao waliteuliwa na raisi nao wamekuwa katika matatizo haya na bunge au vyombo vingine vya kiserikali
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  serikali ya kifisadi hii mkuu kila lililo jema kwa nchi na wananchi linapigwa vita na serikali. We fikiria anamteua Choya kuwa mkuu wa wilaya ambaye ni form IV leaver anawaacha watu wengi wenye sifa kisa choya alishiriki sana kuiba kura 2005 kule biharamulo magharibi. Inasikitisha sana, hatuna wabunge wala serikali ni upuuzi tu.

  najipa moyo tu kwamba hawatafia madarakani, JK anateua watu kwa kuwatazama usoni na siyo sifa. Nilishangaa sana alipomteua kawambwa ambaye hata kufundisha pale UDSM alikuwa ni kituko.
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  uteuzi unafanywa kisiasa, kidugu na kujuana. na ukiweza kujipendekeza
   
Loading...