Rais Zelensky atoa ombi jipya la kuhutubia kikao cha Umoja wa Afrika

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,512
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametoa ombi jipya la kutaka ahutubie wakuu wa mataifa ya Muungano wa Afrika (AU), kulingana na Kamishna wa AU, Moussa Faki.

Katika ujumbe wake wa Twitter, Bw Faki alisema alipokea ombi wakati wa mazungumzo ya simu na Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine.

Wawili hao walizungumza kuhusu Rais Zelensky "kutaka kuendeleza uhusiano wa karibu na AU".

Bw Faki hakufichua iwapo ombi hilo litakubaliwa lakini akatuma ujumbe wa twitter kwamba "alisisitizia juu ya haja ya upatikaji wa suluhu ya amani kwa mzozo wa Ukraine

Mapema mwezi huu, Rais Zelensky alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Senegal Macky Sall, ambaye ni Mwenyekiti wa sasa wa AU, na akamuomba ahutubie viongozi wa Afrika.

Nchi za Afrika zilitawala orodha ya mataifa ambayo yalijizuwia kupijia kura azimio la Umoja wa Mataifa la kuiondoa Urusi katika baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa.

Azimio hilo liliidhinishwa kwa kura 93, 24 zipalipinga na 58 ziliepuka kupiga kura.

BBC:

Screenshot_20220429-121029_Facebook.jpg
 
Watuache. Kwanza Umoja wa Mataifa ni umoja wa kibaguzi na unaidharau Afrika kupita bara lolote lile. Afrika ina nchi 54 ila UN haijaona umuhimu wa Afrika kuwa mwanachama wa Baraza lake la Usalama wa kudumu kama mataifa mengine.

Sisi hatutaki kushiriki vita vyao. Kwetu hua likinuma wanatuona kama fursa na huwa wanajiona miungu watu. Acha mizungu iuane tu
 
Watuache. Kwanza Umoja wa Mataifa ni umoja wa kibaguzi na unaidharau Afrika kupita bara lolote lile. Afrika ina nchi 54 ila UN haijaona umuhimu wa Afrika kuwa mwanachama wa Baraza lake la Usalama wa kudumu kama mataifa mengine.

Sisi hatutaki kushiriki vita vyao. Kwetu hua likinuma wanatuona kama fursa na huwa wanajiona miungu watu. Acha mizungu iuane tu.
Mkong'oto wao wanataka tushee?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom