#COVID19 Rais Yoweri Museveni ametangaza Jumamosi kuwa siku ya kitaifa ya maombi kwa ajili ya COVID-19

Basi Nenda

JF-Expert Member
Jul 29, 2017
20,166
45,872
Rais Yoweri Kaguta Museveni ametangaza muda mfupi uliopita kwamba kutokana na kufuatwa na mtu fulani aliyedai ameoneshwa na Mungu maono kwamba amwambie Museveni aandae siku ya maombi ya Kitaifa kumshukuru Mungu kulitoa Taifa katika janga la Corona ameamua siku ya tarehe 29 /8/2020 kuwa siku ya maombi ya kitaifa kumshukuru Mungu

Aidha rais huyo amewasisitiza wananchi kubaki majumbani mwao huku wakifanya maombi.

2499035_IMG_5807.jpg
 
Rais wetu alipotangaza maombi kitaifa walimuona mjinga na mpumbavu Sana
Ila ashukuriwe Mungu ambaye ukimtegemea hawezi kukuaibisha pia hawezi kujiaibisha Mwenyewe.

Naona walikuwa wanaona Kama utani Corona kuisha Tz..wamebeza lakini baadaye akili imewakaa.
 
Ila mseven pamoja na udikteta wake bado anaiongoza Uganda vizuri sana sio kama huyu mnyapara amabae anatoa amri amabazo hazipo kisheria na eti ana PhD
 
Ila mseven pamoja na udikteta wake bado anaiongoza Uganda vizuri sana sio kama huyu mnyapara amabae anatoa amri amabazo hazipo kisheria na eti ana PhD
Si uhamie Uganda mkuu,ili uishi kwa amani kuliko kuishi na dikteta huku ukiishi kwa mashaka...!
 
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza Jumamosi kuwa siku ya kitaifa ya maombi kwa ajili ya Covid-19.

Rais huyo amesema kuwa alipata wazo kutoka kwa raia wa Ugandaambaye alikuwa na "maono kutoka kwa Mungu ".

"Mungu alikua amemuambia katika moano kwamba ninapaswa kuanda maombi, yaandaliwe kisayansi, ili Mungu atuponye na Covid-19...Ninatangaza tarehe 29 Agosti, 2020, siku ya maombi ya kitaifa na siku ya mapumziko ya umma. Kaeni majumbani mwenu au kwenye viwanja vya nyumba zenu na muombe," Bwana Museveni alisema katika ujumbe wake wa mtandao wa kijamii.

Hadi sasa Uganda imerekodi watu 2,679 wenye maambukizi ya virusi vya coronana vifo 28.

Serikali iliweka masharti ya kudhibiti maambukizibaada ya kuthibitisha kisa cha kwanza mwezi Machi.
 
Back
Top Bottom