Rais wetu usinyamazie suala hili la Corona litaharibu legacy yako vizazi vijavyo

Pearce

JF-Expert Member
Dec 15, 2018
577
1,381
Pole kwa majukumu yanayokukabili kila leo kuanzia usalama wa nchi, mahusiano na mataifa makubwa, pamoja maendeleo ya kijamii kiuchumi na kisiasa. Wakati mwingi sana hakuna ambaye hawezi ona juhudi zako ingawa na madhaifu ya hapa na pale, lakini kila mwanadamu hakosi mapungufu ni kawaida na hata yule anayejiona amekamilika pia huo ni udhaifu au mapungufu.

Lengo la barua yangu isiyo rasmi ni kukuomba sasa Rais wetu, Amiri jeshi mkuu pamoja na baba wa watanzania katika nyakati na majira haya, Mamlaka uliyonayo ni makubwa sana katika taifa hili sababu umeaminiwa kwa juhudi zako na maono uliyonayo juu ya Taifa letu, hasa kama mimi mkazi wa Dar es salaam tunaona uhimalishaji wa miundo mbinu barabara za lami na mengi tu, hadi huduma za kijamii.

Lakini Muheshiwa na kama mzazi wetu (umri wako ni sawa na baba yangu mzazi) hili suala la ugonjwa wa corona lisifumbiwe macho tena okoa wapiga kura wako, okoa wananchi wako ambao kwa usimamizi mzuri wa mamlaka yako hao ndio wanalipa kodi ambazo ndizo unazisimamia vizuri kwa usimamizi wako na nchi inaenda.

Haitakuwa na furaha tena ya maendeleo ambayo unatupatia ikiwa watu watashuhudia jirani zao, ndugu zao na rafiki zao wakiondoka katika uso wa nchi sababu ucheleweshaji wa kuifunga miji yenye maambukizi makubwa na watu wanaumia.

Kweli muheshimiwa Rais mfano tu tunamkumbuka Stalin ni kama mtu aliyeiinua Soviet kimaendeleo makubwa duniani lakini licha ya hivyo, alama aliyoiacha si nzuri kutokana na maamuzi aliyowahi yatekeleza na kuumiza wengi kwa sera tu ya mfumo wa uchumi mfano baa la njaa la Ukraine na mauaji yaliyotekelezwa na watu wa chini yake kama vile kina Beria dhidi wananchi wa Poland yanayojulikana kama Katyn massacre.

Leo hii na mema yote ya Bwana Stalin kuuinua Urussi kwa viwango vingi , imekuwa kila baya la zamani ambao serikali ya leo ikituhumiwa inajitetea kwa kumuoneshea kidole yeye Stalin alihusika mzigo ambao umebeba vizazi vyake pia.

Leo hii Dar es salaam ilivyo utadhani tupo katika state of emergence, huwa haipiti siku usisikie king'ora vya ambulance, mtu akianguka raia wanakimbiana, na watu wamepungua wengi nadhani wanaanza ondoka na kwenda mikoani. Wanaobaki ndio sisi ambao wazazi wamekutana na tumezaliwa mkoa huu.

Mzee wetu mkumbuke mwalimu Julius Nyerere Baba wa taifa hili aliwahi kutamka "Thamani ya maisha ya mtu haiwezi lingana na mafuta". Akampa Ghadafi raia wake wakarudi kwao Libya yaani kusema kuwa maisha ya watu yawe mbele kwanza kama ni uchumi tutaanza upya tu, hata kama ukivurugika namna gani.

Raia ndio waendeleza nchi yao kwa ajili ya kufaidi matokeo ambao ndio uchumi mzuri. Leo hii hata ikikamilika miradi mingi mizuri tulioiona unaitengeneza itakuwa na kumbukumbu ya majeraha juu ya wapendwa tuliopoteza sababu ya maamuzi kucheleweshwa kufungwa miji mikubwa katika hali ya hatari tunayoiona kwa sababu tu ya Uchumi wa nchi.

Yapo mataifa mengi tu yalipoteza kila kitu, lakini linapokuja suala la wananchi wake na kuwalinda, huwa maamuzi yanabadilishwa lazima watetee watu wa kwao mfano Mzuri wapo wakina Edwin Von Rommel, Claus Von stauffernberg na wakina Albert Speer (Kipindi cha vita kuu ya pili ya dunia.)

Wakati bado Sera ya Ujerumani na wenye mamlaka wanajisahau wanaanza kutoka nje ya maono kwa ajili ya uchumi wa nchi lakiini kwa kuhatarisha maisha ya raia wa kawaida, hawa walisimama wakaenda hata kinyume na maagizo ya mamlaka zao.

Leo hii wana alama kubwa wameacha kwa maisha ya wajerumani, walipoweka maisha ya watu wao kwanza na hata wengine walidhurumiwa uhai wao. Nina rafiki yangu ni raia wa ujerumani siku nilipomuuliza kuhusu mmoja wa hao hapo juu alinijibu kwa ufahari sana ya kwamba ana ndugu yake ambae kaolewa na vizazi ya kutoka hiyo koo na kwa kuwafurahia kabisa na hiyo ndio tafsiri ya alama au Legacy nayoizungumzia majengo yatabomoka na vitu vitapita lakini maisha utaendelea kuishi katika fikra za watu.

Leo hata muheshimiwa ukiamua kukata mishahara kwa asilimia 30 tu kwa wafanyakazi wote wa serikali kuanzia ofisi yako tukufu hadi kwa mjumbe wa nyumba kumi, Na kuwaeleza kuwa Wananchi wangu kutokana na tatizo na hali inayoendelea tufanye haya naamini watakuelewa sababu kwa chochote unachosema una mamlaka juu ya wananchi wako basi tunakuombea Mungu akutie nguvu katika hilo.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu Bariki Viongozi wake
Mungu Bariki wananchi
 
"This is dona katri, kwann tukate mshahara wa mtumishi, ondoa hofu, we jifukize tu, tupo kwenye raiti traki.
Aliyekwambia hao wanaokufa wanakufia korona nani?
Kwani malaria imeacha kuua, typhodi na ukimwi je?
Vitisho hivyo ni vya wapinzani wetu.
Hata hao mnaona wanaanguka mabarabarani, ni njaa tu, hamjui kuwa mfungo unaendelea?
Wakipewa futari wanaamka na kuendelea na shughuli zao, ila wakiamka hamposti, mnapost wakianguka tu."
 
Duh, wee jamaa ni noma sana! Yaani utadhani umekamia vile kumbe!
"This is dona katri, kwann tukate mshahara wa mtumishi, ondoa hofu, we jifukize tu, tupo kwenye raiti traki.
Aliyekwambia hao wanaokufa wanakufia korona nani?
Kwani malaria imeacha kuua, typhodi na ukimwi je?
Vitisho hivyo ni vya wapinzani wetu.
Hata hao mnaona wanaanguka mabarabarani, ni njaa tu, hamjui kuwa mfungo unaendelea?
Wakipewa futari wanaamka na kuendelea na shughuli zao, ila wakiamka hamposti, mnapost wakianguka tu."

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais yupo kazini masaa 24 kuhakikisha corona inathibitiwa Tanzania

Msisikilize uzushi wa mtandaoni
 
Wale Watangazaji wa Citizen Tv hawakuwa wajinga wakipomuita MKAIDI! Mtu hasikii, haelewi, hashauriki, mbishi! Huyo ni mtu MKAIDI tu.
 
It will bring him down in the end. Acha ifike vijijini kwa wapigakura wa CCM uone. Na huu ni mwaka wa uchaguzi, ambao pia unaweza ahirishwa kwa vile corona inaelekea kutawala wakati Rais akiwa amejificha.
 
"This is dona katri, kwann tukate mshahara wa mtumishi, ondoa hofu, we jifukize tu, tupo kwenye raiti traki.
Aliyekwambia hao wanaokufa wanakufia korona nani?
Kwani malaria imeacha kuua, typhodi na ukimwi je?
Vitisho hivyo ni vya wapinzani wetu.
Hata hao mnaona wanaanguka mabarabarani, ni njaa tu, hamjui kuwa mfungo unaendelea?
Wakipewa futari wanaamka na kuendelea na shughuli zao, ila wakiamka hamposti, mnapost wakianguka tu."
Point of correction ni ''Dona Kantre''.

Tuendeleeni kuchapa kazi kwa DHATI kweli kweli...
 
nadhani corona mwenyewe ndo atatusaidia...apitie walau viongozi wakubwa maybe watashtuka na kujali
 
Pole kwa majukumu yanayokukabili kila leo kuanzia usalama wa nchi, mahusiano na mataifa makubwa, pamoja maendeleo ya kijamii kiuchumi na kisiasa. Wakati mwingi sana hakuna ambaye hawezi ona juhudi zako ingawa na madhaifu ya hapa na pale, lakini kila mwanadamu hakosi mapungufu ni kawaida na hata yule anayejiona amekamilika pia huo ni udhaifu au mapungufu.

Lengo la barua yangu isiyo rasmi ni kukuomba sasa Rais wetu, Amiri jeshi mkuu pamoja na baba wa watanzania katika nyakati na majira haya, Mamlaka uliyonayo ni makubwa sana katika taifa hili sababu umeaminiwa kwa juhudi zako na maono uliyonayo juu ya Taifa letu, hasa kama mimi mkazi wa Dar es salaam tunaona uhimalishaji wa miundo mbinu barabara za lami na mengi tu, hadi huduma za kijamii.

Lakini Muheshiwa na kama mzazi wetu (umri wako ni sawa na baba yangu mzazi) hili suala la ugonjwa wa corona lisifumbiwe macho tena okoa wapiga kura wako, okoa wananchi wako ambao kwa usimamizi mzuri wa mamlaka yako hao ndio wanalipa kodi ambazo ndizo unazisimamia vizuri kwa usimamizi wako na nchi inaenda.

Haitakuwa na furaha tena ya maendeleo ambayo unatupatia ikiwa watu watashuhudia jirani zao, ndugu zao na rafiki zao wakiondoka katika uso wa nchi sababu ucheleweshaji wa kuifunga miji yenye maambukizi makubwa na watu wanaumia.

Kweli muheshimiwa Rais mfano tu tunamkumbuka Stalin ni kama mtu aliyeiinua Soviet kimaendeleo makubwa duniani lakini licha ya hivyo, alama aliyoiacha si nzuri kutokana na maamuzi aliyowahi yatekeleza na kuumiza wengi kwa sera tu ya mfumo wa uchumi mfano baa la njaa la Ukraine na mauaji yaliyotekelezwa na watu wa chini yake kama vile kina Beria dhidi wananchi wa Poland yanayojulikana kama Katyn massacre.

Leo hii na mema yote ya Bwana Stalin kuuinua Urussi kwa viwango vingi , imekuwa kila baya la zamani ambao serikali ya leo ikituhumiwa inajitetea kwa kumuoneshea kidole yeye Stalin alihusika mzigo ambao umebeba vizazi vyake pia.

Leo hii Dar es salaam ilivyo utadhani tupo katika state of emergence, huwa haipiti siku usisikie king'ora vya ambulance, mtu akianguka raia wanakimbiana, na watu wamepungua wengi nadhani wanaanza ondoka na kwenda mikoani. Wanaobaki ndio sisi ambao wazazi wamekutana na tumezaliwa mkoa huu.

Mzee wetu mkumbuke mwalimu Julius Nyerere Baba wa taifa hili aliwahi kutamka "Thamani ya maisha ya mtu haiwezi lingana na mafuta". Akampa Ghadafi raia wake wakarudi kwao Libya yaani kusema kuwa maisha ya watu yawe mbele kwanza kama ni uchumi tutaanza upya tu, hata kama ukivurugika namna gani.

Raia ndio waendeleza nchi yao kwa ajili ya kufaidi matokeo ambao ndio uchumi mzuri. Leo hii hata ikikamilika miradi mingi mizuri tulioiona unaitengeneza itakuwa na kumbukumbu ya majeraha juu ya wapendwa tuliopoteza sababu ya maamuzi kucheleweshwa kufungwa miji mikubwa katika hali ya hatari tunayoiona kwa sababu tu ya Uchumi wa nchi.

Yapo mataifa mengi tu yalipoteza kila kitu, lakini linapokuja suala la wananchi wake na kuwalinda, huwa maamuzi yanabadilishwa lazima watetee watu wa kwao mfano Mzuri wapo wakina Edwin Von Rommel, Claus Von stauffernberg na wakina Albert Speer (Kipindi cha vita kuu ya pili ya dunia.)

Wakati bado Sera ya Ujerumani na wenye mamlaka wanajisahau wanaanza kutoka nje ya maono kwa ajili ya uchumi wa nchi lakiini kwa kuhatarisha maisha ya raia wa kawaida, hawa walisimama wakaenda hata kinyume na maagizo ya mamlaka zao.

Leo hii wana alama kubwa wameacha kwa maisha ya wajerumani, walipoweka maisha ya watu wao kwanza na hata wengine walidhurumiwa uhai wao. Nina rafiki yangu ni raia wa ujerumani siku nilipomuuliza kuhusu mmoja wa hao hapo juu alinijibu kwa ufahari sana ya kwamba ana ndugu yake ambae kaolewa na vizazi ya kutoka hiyo koo na kwa kuwafurahia kabisa na hiyo ndio tafsiri ya alama au Legacy nayoizungumzia majengo yatabomoka na vitu vitapita lakini maisha utaendelea kuishi katika fikra za watu.

Leo hata muheshimiwa ukiamua kukata mishahara kwa asilimia 30 tu kwa wafanyakazi wote wa serikali kuanzia ofisi yako tukufu hadi kwa mjumbe wa nyumba kumi, Na kuwaeleza kuwa Wananchi wangu kutokana na tatizo na hali inayoendelea tufanye haya naamini watakuelewa sababu kwa chochote unachosema una mamlaka juu ya wananchi wako basi tunakuombea Mungu akutie nguvu katika hilo.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu Bariki Viongozi wake
Mungu Bariki wananchi
Yaani walaka wote huu unachotaka ni 'Lockdown' tu! We kweli akili zako ni za kushikiwa! Waliofanya lockdown wameshaona haisaidii na sasa wameamua kuachia watu waishi maisha yao japokuwa corona bado imo nchini mwao!
Eti ving'ola vya ambulance kila siku vinasikika! Kwani vimeanza sikika kipindi hiki cha corona? Fuateni maelekezo, tunakwenda vizuri! Corona tumeshaishinda hii! Mtaona sooon!
 
It will bring him down in the end. Acha ifike vijijini kwa wapigakura wa CCM uone. Na huu ni mwaka wa uchaguzi, ambao pia unaweza ahirishiwa kwa vile corona inaelekea kutawala wakati Rais akiwa amejificha.
Wishiful evil thinking! Mungu anailinda Tz!
 
nadhani corona mwenyewe ndo atatusaidia...apitie walau viongozi wakubwa maybe watashtuka na kujali
Ashaanza, sema wanasalitiana. Wakifa wanaitana kadhaa wanakurestisha in piisi wanaendelea kukaza shingo like no body's business
 
Back
Top Bottom