Rais wetu tutue mizigo hii huku vijijni

mcoloo

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
918
1,401
Tumesikia kauli ya Rais wetu mpendwa akiwasihi viongozi wa vyama vya siasa hususa ni wa upinzani akiwaita wake ili chama chake liwatue na kuwapumzisha uzito wa mizigo walio nao. Hilo in jambo jema kwani kwa hao viongozi wa kisiasa mh Rais ameona wameelemewa na mizigo wa uchu wa madaraka na ndio maana kila anayekuja anarudishwa kwenye nafasi ile ile nakama hakuwa na wadhifa basis amewateua kuwa wakurgenzi ,wakuu wa wilaya, mikoa, na hats makatibu wakuu wa wizara, ni vema kwani wameelemewa na mizigo wa uchu wa madaraka kuliko kuwatumikia wananchi walio wapa ridhaa kupitia sanduku LA kura, na hii sijui kama ndio kuwa heshimu au ni kuwadharau wananchi walio kupigia kura. Tumeona nijambo jema analolifanya.

Sasa tunakuomba Rais wetu hata sisi wananchi tulioko huku vijijni tuna kuomba nasi pia ututue mizigo inayo tuelemea, tuna mizigo ya kupanda kwa gharama za maisha, vifaa vya ujenzi viko juu sana, saruji sasa haikamatiki ,na sababu kubwa tunasikia kuwa kuna viwanda vimesimamisha uzalishaji kwa ughali wa Mali ghafi, na kadri Sikuzinavyo enda tunaona kujenga kakibanda ndani ya nchi yetu pendwa itakuwa kama jambo LA anasa , ulituambia utatengeneza Tanzania ya viwanda tuna kuomba sasa imarisha nasi hats hivi vichache vilivyopo ili badala ya kuvifunga viazilshe natupate bidhaa hizo kwa gharama nafuu, ukifanya hivyo utakuwa umetutua mzigo.

Mh Raid wetu njoo uangalie mzigo ulio tuelemea kwenye sekta ya elimu, ulipo ingia madarakani tulishuhudia maboresho makubwa sana kwenye elimu ikiwa ni pamoja na utengenezaji wa madawati, ukarabati wa majengo, huwenda hata katika kuboresha maslahi ya waalimu. Lkn jambo linalo shangaza hayo sijui yalifanyika zaidi kwa maeneo ya mijini, ila ukweli ni kwamba kuna maeneo mengine ndani ya nchi hii bado wanafunzi wanasomea kwenye madarasa ya nyasi na kukalia vigogo vya vya miti na mawe, huu ni mzigo wetu huku vijijini tuna kuomba ututue.
Kwenye kilimo pia kuna mzigo wa masoko wanchi wamejitahidi kulima lkn masoko ni shida tunaomba mzigo huu na mtutue umetuelemea.

Madawa huu nao ni mzigo ,zahanati hata vituo vya afya ni mzigo huku vijijini.
Maji ni shida tena hapa ndio tumeelemewa mno hii nitoka Uhuru wa nchi hii mbona tumezungukwa na mito mikubwa na maziwa makubwa takriban matatu ukiachia mengine madogo madogo, lkn huku vijijini bado kuna maeneo tunachangia maji na mifugo hata na wanyama wa porini utadhani nchi yetu ilipata Uhuru Jana, huu ni mzigo tunaomba ututue.
MH Rais tunatambua malengo mazuri uliyo kuwa nayo wakati unaingia madarakani , lkn toka ulivyo anza kufanya teuzi hasa katika chama, walipo ingia akina Polepole mtizamo ukaanza kibadilika Yale mawazo mazuri ya huduma kwa jamii yakaanza kusogea mbali na sasa yako mbali kweli ukweli, matokeo yake imekuwa ni kupiga mark time, hakuna tena hata habari ya Tanzania ya viwanda ,matokeo yake wanakurudisha kwenye Tanzania ya kununua madiwani na wabunge tena kwa gharama kubwa na kuhafifisha mtizamo wako mazuri wa kubana matumizi, mh Rais ulipo ingia madarakani ulituambia kuwa wewe si maana siasa na ukaja na kaulimbiu ya HAPA KAZI TU.

Imekuwaje umeanza kuisahau hii kauli mbiu nzur kama hii na kurudishwa nyuma na hao walioingia kwenye siasa kama ajira na ndio maana badala ya kuna na mbinu za kukiimarisha chama wao wanakuja na mbinu za kukidhohofisha chama na kufanya chama kichukiwa na wanchi wote sio walioko upinzani Bali hata ndani ya chama na mbaya zaidi wamejielekeza kwenye matumizi mabaya ya fedha za hawa watanzania ambao mweshimiwa huwa unawaita kuwa na maskini, iweje Leo hujuma zifanyike kwenye kodi za hawa maskini badala ya fedha hizo kutumika kazi za kuwaletea maendeleo hawa watanzania maskini, ebu angalia mh gharama kubwa hizo zinazotumika kurudia chaguzi ungetengeneza barabara ngapi kama ile ya kutoka mwanza airport kuelekea mjini, kama ile ya Sam Nujoma mwenge.

Kwa mtizamo wangu kuna mzigo unaotakiwa kuwatua sana CCM kwa kuwaangalia tena upya watu kama akina Polepole na genge lake hawa wanakidhohofisha chama na wala hawakiimarishi angalia toka wameingia chuki ndio imezudi ndani na nje ya chama wananchi wamepoteza imani na chama,,na hasa kwa kupitia mbinu hafifu katika siasa.
Mh Rais ukweli ni kwamba watanzania wanayaona makandokando yanayofanywa na CCM katika chaguzi hizo na hawa furahi hata kidogo matokeo yake chama kina angamia.
Huo nao ni mzigo watue watanzania.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom