Rais wetu tumia mamlaka yakovizuri.....Rais bila mamlaka hafai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais wetu tumia mamlaka yakovizuri.....Rais bila mamlaka hafai

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Haki Yetu, Feb 4, 2012.

 1. H

  Haki Yetu Senior Member

  #1
  Feb 4, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekua nikifuatilia baadhi ya mambo kuhusiana na bwana mkubwa (JK) na wasaidizi wake. Kwa kiwango fulani nawahurumia sana baadhi ya wasaidizi wake ambao kwangu mimi naona bado wana heshima japo kidogo kwa wananchi. Kuna baadhi ya matukio ambayo kwangu mimi naona RAIS WETU HAFAI.
  1. Mgomo wa madaktari
  Sakata la mgomo wa madaktari sio geni kwa watanzania. Katikati ya sakata hilo Mhe. Rais alikwenda kuhudhuria kikao cha uchumi nje ya nchi (Switzerland). Wananchi walidhurika kwa kushindwa kupata huduma muhimu za afya na pia baadhi walipoteza maisha. Rais alipewa tuzo ya kupambana na malaria wakati wananchi walikua wakiteseka na mgomo wa madaktari. Makamu wa rais nae alikua Tanga kwenye ziara iliyopoteza maisha ya askari wawili. Fedha za umma zilitumika kwenye ziara ya Uswisi na Tanga, wakati madaktari wanadai kuboreshewa maslahi yao. Pinda akapewa kazi ya kuongea nao, alichokisema wote tunajua, katika hili Pinda amekaangwa.

  2. Kuhusiana na posho ya wabunge
  Nimesikia kupitia vyombo vya habari kuhusiana na mkanganyiko wa hili suala. Utaratibu ni kwamba Rais alipaswa kuwa mtu wa mwisho kukubali au kukataa kuhusiana na suala hilo. Spika na Waziri Mkuu wanadai kwamba Rais aliridhia, na Ikulu wanadai hilo halikufanyika. Inadaiwa kuwa rais alirudisha suala hilo kwa Waziri Mkuu na kuagiza busara itumike katika kuamua suala hili. Kama kawaida katika hili Pinda na Makinda wamekaangwa.

  3. Ukubwa wa Msafara wa Rais kwenye safari za nje
  Nikasikia tena kuwa Rais amemuagiza waziri wa mambo ya nje kuwa apunguze msafara wa maafisa wanaoambatana nae kwenye ziara za nje ya nchi. Sababu kuu ikiwa ni kuwa eti fedha nyingi za umma zinatumika kwenye ziara hizo. Tokea ameingia madarakani leo ndo anaona kuwa ujumbe wake hua mkubwa? Kwa agizo lake anaonesha kuwa Waziri wa mambo ya nje ndo hua anachagua maafisa wa kuambatana na rais kwenye ziara. Katika hili inaonyesha kua tatizo sio rais bali waziri. Katika hili nalo, Waziri atakaangwa siku moja.

  4. Waathirika wa Mafuriko
  Tokea mwanzo Serikali ilisema kua wenye nyumba sehemu za mabondeni watapewa viwanja na si wapangaji. Suala hili lilikua la muda kidogo na Rais nae ni sehemu muhimu sana kwenye serikali. Malalamiko ya wapangaji yalisemwa sana na Serikali ilisimama kwenye msimamo wake wa awali. Bwana mkubwa alipokwenda kuwatembelea mabwe pande, aliagiza wapangaji nao wapewe viwanja. Katika hili nalo, Sadiq (RC Dsm) alikaangwa.

  Sasa ndugu zangu, kweli huyu rais anatufaa kweli? Mbona anashindwa hata kutekeleza majukumu ya kawaida kama kukataa au kukubali ongezeko la posho ya wabunge? Hayo niliyoweka ni machache tu kuna dowans, sakata la Lowassa na mengine mengi. Nahitaji michango yenu katika hili.
   
 2. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  wengine bado tunampenda msitusemee tuna midomo kama nyinyi
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  jk asikosee amekua mungu tangu lini
   
 4. B

  BMT JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  kumbe watu tnatofautiana sana kufikiri hee,mbona mleta mada kachambua vzr sana mwenzangu,kwel we pipijojo i mean akili huna
   
 5. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,635
  Likes Received: 4,743
  Trophy Points: 280
  Kwani nchii kuna rais?
   
 6. D

  DATOGA Member

  #6
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  nchi iko ktk AOTO PILOT
   
 7. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #7
  Feb 4, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  unampenda wewe unayenufaika na ufisadi wake yeye na magamba wenzie. Kwa sisi walala hoi tuna hasira naye ile mbaya oooh

   
 8. f

  frontline1 Member

  #8
  Feb 4, 2012
  Joined: Dec 4, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kwa hili la auto pilot me nimeliona kabisa nw yatupasa kuweka m2 mapema bse auto pilot ikifail itakuwa ni hatari sana kwa mustakabali wa taifa letu.

  me naomba tu watu wapate muamko wakutosha be4 2015.
   
 9. S

  Sting007 JF-Expert Member

  #9
  Feb 4, 2012
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hoja ya "busara itumike katika kuamua swala la posho za Wabunge" imedhihirisha kwa kiasi gani JK raisi wa Tanzania asivyokuwa na Msimamo katika Kutoa Maamuzi ya kiutendaji, alichotakiwa kusema "nyongeza ya posho kwa Wabunge Haikubaliki.....! Kwani nchi ipo katika ukata kiasi cha Halmashauri nchini kushindwa kujiendesha" kuliko kujing'atang'ata na kusababisha Malumbano nchini.
   
 10. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #10
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mkuu INVISIBLE, kama tungalikua na utaratibu wa JF nayo kuwa na hotuba yake ya mwisho wa mwezi na wajumbe kulipigia kura, mimi kura yangu iko naye huyu Mkuu HAKI YETU. Daaah, jama kaenda kwa pointi yale yanayotusibu kitaifa kwa wakati huu!!!

  HAKI YETU, hebu ongezea hapo pointi ya 5 kuzungumzia pia huyu mbunge wa jimbo la JF bungeni Mh Cynthia Ngoye na ujumbe wa kutaka forum hii ambayo hata JK ni memba isiwepo hewani. Kwa pointi ya sita katufahamishe sisi wananchi kwamba Blandina Nyoni anaondoka lini wizara ya afya, kisha ukamalizie na taarifa juu ya mkutano wa Davos na tija zake kwa mkulima Chunya.

  Big Up sana HAKI YETU!!!!!!!!!
   
 11. D

  Do santos JF-Expert Member

  #11
  Feb 4, 2012
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 470
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  wengi tunampenda acha kujishaua
   
Loading...