Rais wangu mpendwa, waliokushauri kulihutubia taifa kwa gia ya kuzungumza na wazee wamekudanganya. Suala la Ma- dkt si suala la wewe kwenda kuhutubia wahuni wanaoshangilia kwa kuwaita kuwa ni wazee. Pale ulikuwa ukijimwaga na wana CCm na si wazee wa Dar. Kuzungumza na wazee si kuwaambia hayo uliyokuwa unasema! kumbuka ni wazee hao hao wanao lilia huduma ya afya kwani serikali yako imewatupa kabisa. je uliona wale wazee wa kule shinyanga wenye ukoma ambao nyumba zao zimekwisha anguka na sasa wanalala nje? Tungekuona bingwa wa kuwabeza madaktari kama ungekwenda kule makaoni pao na kuongea nao juu ya ma-dkt wetu.
Unajua kuwa Mhimbili haina mazingira mazuri ya kufanyia kazi pamoja na kwamba inaingiza mamilioni kwa usiku tu? Tazama sakafu zake, chakula cha wagonjwa,kitchen utensils, Vitendea kazi kama CT-Scanners, n.k kila siku vibovu. Who is liable for that if not the top most leaders/CEOs? Ebu anza na kuwawajibisha tuone kama TANESCO pia watakuwa wanachezea uchumi wa nchi kwa kukata umeme kama wapendavyo na bila maelezo.