Rais wetu Samia, turudishie Lukuvi Wizara ya Ardhi. Kwa sasa ni mateso, kiburi na rushwa iliyokithiri

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
18,620
20,954
Rais wetu mpendwa Mama Samia ikikupendeza tunakuomba sisi wananchi wako wanyonge uturudishie mnyonge mwenzetu Mh. Lukuvi, alipamudu alipanyoosha nidhamu ilikuwepo haki ilikiwepo heshima ilikiwepo uwajibikaji ulikuwepo usikivu ulikuwepo.

Aidha kama hili litakushinda tuwekee dawati hapohapo wizarani Dodoma na Dar es Salaam, maalum ambalo wananchi wataweza kutoa vinagaubaga vyao kwa dawati hilo ambalo litakuwa linamfikishia waziri aliyepo kipi kinafanyika hapo hivyo naye kusaidia kutoa maamuzi ya haraka.

WASALAAM.
N. B, NAPENDA KUTOA SHUKRANI KWA DR. ANGELINA MABULA HIS DOCTORATE HAS DONE SOMETHING EXCEPTIONAL, THANKS YOU MADAM.
KUMBE UNATUSIKIA, UBARIKIWE.
 
Rais wetu mpendwa mama Samia ikikupendeza tunakuomba Sisi wananchi wako wanyonge uturudishie mnyonge mwenzetu MH. Lukuvi...
Wenye Akili tunajua Waziri hapo ni Ridhiwani Kikwete na huyo Mabula ni Ceremonial Minister TU hapo.

Dogo (RK) kawekwa hapo Kimkakati ili kuhakikisha Miradi yote ya Baba (hasa ya Ardhi) ikamilike na ule mkubwa wa Bandari ya Bagamoyo ukamilike.

Ilikuwa ni lazima Waziri Lukuvi aliyefanya vyema katika Wizara hiyo aondolewe kwani alikuwa hataki Upuuzi ( hasa wa Wakubwa) katika Kujinyakulia Ardhi (Maeneo) na Kujitajirisha huku Watanzania Masikini wakiporwa hayo Maeneo na Kunyanyasika nao.
 
Mradi wa viwanja vya kata ya Pembamnazi (Kigamboni) eneo la Block 1 na 2 umetelekezwa. Hadi leo hakuna barabara zilizochongwa kwenye viwanja licha ya wananchi kuuziwa viwanja hivyo na wizara. Wizara hii imejaa utapeli. Watu waliuziwa viwanja Pembamnazi bila ya kuviona. Huu ni utapeli. Rahisi Samia safisha wizara ya ardhi
 
Wizara iliyoshindwa kazi na kubaki wizara ya wapiga dili.

Kuhusu teuzi sa100 analeteewa majina kutoka msoga gang...kama ulikua hujui hili basi tambua hivyo...wao ndio wenye maamuzi nani ateuliwe nani atenguliwe.

#MaendeleoHayanaChama
 
Unamjua vizuri Lukuvi lakini ila kwa kukusaidia CCM wote lao mmoja wapo kwa Ajiri Matumbo yao familia zao Rafiki zao ndio maana mara zote nasema Trump alikuwa sahihi juu yetu watu weusi...

Sawa pamoja na hayo makando Kando na u CCM na mengine mengi umeyasema lakini kwenye Wizara ya ardhi ametufanyia mengi mazuri. Ni katika kipindi chake upatikanaji wa hati umerahisishwa na watu wengi kupata hati zao.
 
Unyonge wa Lukuvi haswa ni upi ?

Tuseme hakuna mtanzania mwingine mwenye uwezo zaidi ya Lukuvu pekee ake ?
Tunatumiaga tu neno unyonge lakini si kweli ni wa nyonge, LUKUVI ALIPAMUDU, ALIPAWEZIE ULIKUWA UKIFIKA UNASIKILIZWA NA JAMBO LAKO LINAFANYIWA KAZI HARAKA SANA ENDAPO KAMA TARATIBU ZIMEKAMILIKA LEO HII KAMILISHA TARATIBU ZOTE, BADO LITACHELEWESHWA, ALIMRADI UWASOGELEE UWABEMBELEZE, INFACTS KUCHELEWESHA JAMBO KWA KIPINDI KIREFU NI NJIA YA KUTENGENEZA RUSHWA THATS FACTS,MAANA UNACHWISHWA KWANZA AKILI.,ULEGEE.
 
Rais wetu mpendwa Mama Samia ikikupendeza tunakuomba sisi wananchi wako wanyonge uturudishie mnyonge mwenzetu Mh. Lukuvi, alipamudu alipanyoosha nidhamu ilikuwepo haki ilikiwepo heshima ilikiwepo uwajibikaji ulikuwepo usikivu ulikuwepo aidha kama hili litakushinda tuwekee dawati hapohapo wizarani Dodoma na Dar Es Salaam, maalum ambalo wananchi wataweza kutoa vinagaubaga vyao kwa dawati hilo ambalo litakuwa linamfikishia waziri aliyepo kipi kinafanyika hapo hivyo naye kusaidia kutoa maamuzi ya haraka.
WASALAAM.
KUNA WIZARA ISIYO NA RUSHWA KWA SASA?
 
KUNA WIZARA ISIYO NA RUSHWA KWA SASA?
Ardhi pamezidi mkuu, "Wezi wa viwanja vya watu na matapeli wanapewa uzito wa juu kabisa na docs zao hazichelewi ili kufanikisha utapeli, that's mean kuna chains hapo wanayoitambua ya siri timu buglers, pia kwa utendaji bora nadhani kuwe na utaratibu wa kuhamisha wafanyakazi na watakapokuwa wamehamia wachanganywe na PCCB.
 
Rais wetu mpendwa Mama Samia ikikupendeza tunakuomba sisi wananchi wako wanyonge uturudishie mnyonge mwenzetu Mh. Lukuvi,
Kama kunatatizo mahali unatakiwa ulionyeshe, kwanini arudishwe mzee Likuvi wakati TZ inawatu tele, hakuna aliezaliwa kiongozi. Hii keki ya taifa wacha tugawane sote, sio kila siku walewale tu.
 
Ardhi kumekua kwa kingese sana sikuhizi bila hongo hupati huduma na mtu anaongea live hata haogopi hawa watu wa ardhi na Tra nina clip zao nyingi tu siku nitaanza kuziachia livelive maana wanaona rushwa ndo kilakitu na wanalipwa mshahara.

Anzisha uzi uanze kuziachia hizo clips na kila mtu atabandika aliyonayo na kwaujumla watapata aibu na huenda pia ikatusaidia kubadirisha mambo, na kila mtanzania sasa atakuwa anarecord na kupost kila tukio kwenye uzi huo.
 
Back
Top Bottom